SCENE 44:
CHUONI KWA KINA LILIANA: -
(Majira ya saa sita adhuhuri,
Liliana pamoja na binamu zake wamekaa katika moja ya migahawa ya chuoni kwao
wakipata chakula huku wanaongea mambo mbalimbali yahusuyo maisha. Wanaonekana
wana furaha sana na maongezi yao yanaonekana ni ya Amani)
Anna:
nani angejua kuwa Bianca na baba wangependana na kuoana
Bella:
wanatarajia
Anna:
ni kile kile bwana
Liliana:
(anacheka kidogo) na shangazi alikuwa
anawahisi kuwa wanatoka kimapenzi
Anna:
kwa kipindi kile hawakuwa wanatoka
Liliana:
ni vile tu mama yangu anajua kuheshimu watu
Bella:
kabisa
Anna:
halafu naona ile kuwahisi na kukaa kuwaambia ambia kuwa wana mahusiano ndo
kiliwaleta pamoja
(Wanacheka)
Liliana:
ndio
(Robert anakuja kwa mbali)
Anna:
eeh yule si shemeji?
Liliana:
Robert?
Anna:
ndio
Robert:
(anawafikia)
(Wanamsalimia)
Robert:
(haitikii)
(Wanashangaa)
Robert:
(kwa Liliana) wewe mwanamke…
Liliana:
(anamshangaa)
Robert:
ukiachwa achika
Liliana:
bado sijakuelewa kwani mimi nimekufata tena baada yaw ewe kuniambia maneno
makali kama yale?
Robert:
nimempenda Bianca na nipo radhi kumuacha mke wangu na kumuoa Bianca
Anna:
shemeji
Robert:
(kwa hasira) mimi sio shemeji yako unikome
Liliana:
umeongea nimekusikia sasa mimi nimekuzuia nini?
Robert:
kila nikiongea nae anakutaja wewe inamaana wewe ndo unamzuia…kwanini lakini?
Bella:
Liliana hazuii chochote yeye wala haongei na mama yake kuhusu wewe…topic yako
kwenye nyumba ya kina Liliana haipo baba…Bianca hakutaki maana anatarajia
kufunga ndoa na baba yangu
Robert:
wewe mtoto wewe...shika adabu yako
Bella:
wewe ndo ushike adabu yako wewe baba mtu mzima usiye na haya kazi kuharibu
maisha ya watu lione lizomeeni
Anna:
Bella acha
Liliana:
(anasikitika) Robert nilikupenda sana
ila umeniumiza sana pamoja na hayo mimi sikutaka kitu chochote kutoka kwako ila
wewe bado unaendelea kutaka kitu maishani mwangu
Robert:
kitu gani maishani mwako huku hata huyo mwanaharamu uliyembeba tumboni kwako
simtambui na wala simjui
Liliana:
(anasikitika) bado unanifata fata
kisa mama yangu...Robert kwanini usituache tu tukae kwa Amani jamani
Robert:
siwezi kukuacha kwa Amani maana nampenda sana Bianca
Liliana:
sawa haina shida mwambie tu
Robert:
hawezi kukubali maana anahofia wewe utamuonaje sijui
Liliana:
nitamuonaje
Robert:
sijui
Liliana:
Robert listen nilikuwa nipo hapa na binamu zangu tunapanga harusi ya mama yangu
naomba uondoke ili tuendelee na mipango yetu
Anna:
umekuja kutuharibia wakati wetu mzuri
Bella:
kwanza amejuaje tupo hapa?
Liliana:
alihisi tu maana huwa napenda kukaa sana hapa
Robert:
naomba nikutume wewe Liliana ya kwamba mwambie mama yako kuwa nampenda sana na
asiolewe na kama hatakuwa wangu basi hatakuwa wa mtu yeyote
Anna:
aisee
Bella:
mtu mzima hovyoooo (anafyonza) hana
hata aibu lione
Liliana:
(kwa Robert) ujumbe wako nitaufikisha
usijali
Robert:
good (anaondoka zake)
Anna:
huyu baba zinamtosha kweli?
Liliana:
yaani sijui ni mkosi gani nilionao mwenzenu (machozi
yanamlenga) sijawahi kufurahia maisha yangu
Anna:
no usikumbuke ya zamani mdogo wangu huna mkosi wowote wewe ni Baraka Liliana
kwanza una roho nzuri embu kumbuka mambo yote tuliyokufanyia mwanzoni lakini
bado ulitusamehe hata Mungu alipokupa nafasi ya kuishi vizuri ulituita na
tukaishi maisha mazuri Liliana baba alikufanyia unyama lakini umemsamehe na leo
hii tunatarajia kuishi pamoja kama familia…wewe ni Baraka huna mkosi Liliana
Liliana:
(anashusha pumzi) najua ila ikija
suala la mahusiano sijawahi kufurahia maisha mwenzenu
Bella:
come down cousin jamani
Liliana:
(anashusha pumzi) yaani sijui
Anna:
cheer up na tuendelee kuongea kuhusu harusi yaani kwanza mmeona gauni la
Bianca?
Bella:
nimeliona…yaani yule mwanamke ameenda age lakini bwana ana mvuto loh lile tako
vipi?
Liliana:
(anacheka) jamani
Bella:
mimi nawaambia
Liliana:
ndo maana Robert amedata
Anna:
naomba usimuwaze yule mwanaharamu
Liliana:
mwanaharamu amemuita mwanangu… I swear nitailea hii mimba na vyovyote
Anna:
tupo sisi na mama yako atakuwa tu
Liliana:
nimeathirika pia mwenzenu
Anna:
it doesn’t matter kwani kuathirika ni nini mwenzangu? Utaishi tu
Liliana:
sawa (anashusha pumzi) asanteni kwa
kunipa moyo nawapenda sana
Anna:
nasi tunakupenda sana
Liliana:
(anatabasamu)
Anna:
you are so beautiful Liliana
Liliana:
(anatabasamu) asante sana
Bella:
(anatabasamu pia)
Anna:
twendeni nyumbani?
Bella:
ofcourse hapa ni nyumbani tu
Liliana:
okay twendeni kwa bibi harusi
(Wanacheka kisha wananyanyuka na
kuondoka zao)
Anna:
twendeni kwanza kwenye icecream
Bella:
na wewe utasema una mimba
(Wanacheka
huku wanaondoka mahali hapo)
0 Comments