I KILLED MY LOVER 48

 


SCENE 48: -

MTAANI KWA KINA ROBERT: -

(Majira ya saa saba mchana hali ya hewa ni ya mawingu kiasi, Liliana anafika katika nyumba kubwa tena inaonekana ina wapangaji wengi sana)

Mama mwenye nyumba: oh, binti ndo umekuja?

Liliana: ndio nimekuja...natumaini chumba changu kipo tayari

Mama: kabisa mimi sina ahadi za kijinga au za uongo nimekuwekea chumba kizuri kama ulivyotaka

Liliana: asante (anacheka kidogo) nilitaka chumba chenye utulivu si unaona hali yangu hii?

Mama: naiona

(Wanacheka)

Mama: usijali (anamfungulia chumba) sasa mbona hujaja na kitu chochote utakuwa unalala wapi?

Liliana: nitavileta tu

Mama: oh sawa

Liliana: asante (anaangalia mazingira ya chumba kile) nimekipenda ni kizuri (anafungua dirisha anaona nyumba ya Robert) na ni kizuri sana naiona nyumba ile kwa uzuri kabisa

Mama: yule ni Robert tajiri mkubwa sana hapa mtaani kwetu ni mtu mzuri anapenda watu ila ubaya wake anapenda sana wanawake

Liliana: oh, anapenda sana wanawake ee

(Wanacheka pamoja)

Mama: sana

Liliana: atakufa

Mama: na UKIMWI au?

Liliana: (anajichekesha)

Mama: hapo alipo nasikia anao (anacheka) mimi nami mmbea

Liliana: wala hata sio mmbea unasema tu

Mama: (anacheka)

Liliana: kwani hana familia?

Mama: nasikia anayo watoto watatu na mke

Liliana: wanaishi wapi?

Mama: Canada

Liliana: sasa yeye anafanya nini huku?

Mama: ana miradi baba ana miradi baba tajiri huyu mpaka sio poa haki ya nani

Liliana: eti ee ndo anawadanganyia wanawake pesa zake

Mama: wanawake nao wanataka wenyewe…mimi mwenyewe ningekuwa siogopi UKIMWI ningemuendea nikajipendekeza

(Wanacheka)

Liliana: unaogopa UKIMWI siku hizi mbona Malaria tu hiyo?

Mama: pamoja na kwamba ni hivyo bado ni tishio

Liliana: hamna wewe tulia mbona watu wanaishi nao miaka 20,30 inategemea tu unajilinda vipi na unatumiaje dawa

Mama: (anaguna) haya bwana nitajipendekeza

(Wanacheka)

Mama: mama chumba chako ndo hiki

Liliana: asante

Mama: haya acha nikuache ila ndo huna hata pa kukaa

Liliana: usijali kuhusu mimi

Mama: (anatoka)

Liliana: (anachungulia dirishani kwa mbali anamuona Robert) muone alivyo hana hata haya huyu mwanaume ambae sijui alitapikwa au alifanywaje? Ona anavyowaua watoto wa watu kwa maradhi kwa kuwalaghai kwa pesa na zawadi ndogondogo baada ya hapo akutane na mama zao awatamani pia wale mama wamkatae awaue kama alivyofanya Kwa mama yangu sasa kabla hajafanya huu ujinga lazima nimuue hawa watu hawatakiwi katika hii dunia

Robert: (anamshika kiuno mrembo aliyekuja nae mahali hapo) mrembo tamba mama tamba leo zamu yako

Mrembo: (anajichekesha) Robert pedeshee

Robert: ewaaaaaaa

Liliana: (akiwa chumbani kwake) tamba tu wewe tamba tu mwisho wako unakuja sijui utanijibu nini

Robert: (anaonekana kufurahia maisha na mrembo)

Mrembo: daddy una nyumba nzuri

Robert: mimi ndo Rob mapesa mama sema utakacho mimi nitakupa

Liliana: (anachungulia dirishani) wewe unafurahi wakati mama yangu amelala mauti tena hata maiti yake hatukuipata ilikuwa ni majivu (anatokwa machozi) nakuchukia sana Robert ile nguvu niliyokuwa nayo ya kukupenda imebadilika kuwa chuki mbaya sana najuta hata kwanini nilikuwa mpenzi wako sikukujua wewe ni mwanaume mbaya sana na Mungu akusamehe nakuchukia sana

Robert: (anaendelea kufurahia maisha kama kawaida) napenda wanawake wembamba tena wenye mironjo kama wewe

Mrembo: jamani daddy mbona unanitukana tena jamani

Robert: no baby sikutukani (anacheka)

Liliana: (anang’ata meno) cheka Robert cheka sana tena kazana kucheka maana umeamua kucheka furahia ila nakuhakikishia majira kama haya na wewe utabaki majivu utalala mauti (Analia sana) mama yangu (anakumbuka matukio muhimu aliyofanya na Bianca kuanzia alipochukuliwa kutoka mitaani mpaka kusomeshwa na kulelewa vizuri bila shida, mapenzi yote aliyoonyeshwa na Bianca) mama yangu... wewe Mungu uliyenipokonya wazazi kisha nikaishi kwa dhiki kubwa kisha ukanipa mama aliyenilea vizuri kwa upendo na kwa mapenzi yako ukamchukua naomba ujibu kwa moto this time sitasamehe nilimsamehe shangazi na mjomba wangu kwa kunifanya kijakazi ndani ya nyumba ya wazazi wangu naomba unisamehe sitasamehe

Robert: (anaendelea kufurahia maisha na mrembo)

Mrembo: daddy naomba basi uninunulie gari

Robert: sema aina gani mrembo hapa ni kwa mapesa ni wewe tu jitahidi kunipa mapenzi ya kweli leo hii wallahi utaondoka na gari unaweza kuchagua hapa au tukaenda show room

Mrembo: (kwa madeko kidogo) nataka show room daddy

Robert: imekuwa mrembo (anambusu mdomoni)

Liliana: (anafyonza) lione

Robert: (hana habari kama Liliana anamuangalia)

Mrembo: twende ndani daddy nikakupe mambo adimu

Robert: mmmmh hamna jipya na uzee huu unadhani sijawahi kupata mambo yote?  

Mrembo: (anabaki anashangaa)

Robert: (anacheka kwa nguvu) nakutania ila siku nyingine usiseme kuwa unataka kunipa mambo adimu nitakushangaa sio mimi tu bali mtu yeyote anayepita hapa atabaki anakushangaa

Mrembo: sawa daddy

Robert: usiniite daddy hilo jina linanikumbusha mtu mmoja ambae tulimaliza vibaya sana kitoto kilikuwa kinanilia pesa kidogo kinifilisi (anamkumbuka Liliana) anyways sitaki kukumbuka alinisababisha nikamfanyia kitu kibaya sana mwanamke nimpendae kwa dhati namchukia ilikuwa kwasababu yake yule mwanamke alinikataa kabisa (anamkubuka Bianca) alikuwa ni mwanamke mrembo sana (anakumbuka tabasamu la Bianca)

Mrembo: daddy                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                

Robert: (kwa ukali) get out…toka

Mrembo: (anashangaa huku anaondoka)

Robert: (anamkumbuka Bianca sana) oh my God nilifanya nini?

Liliana: (anamuangalia anavyohangaika) mzimu wa mama yangu hautakuacha kirahisi Robert

Robert: nilimpenda sana Bianca nilifanya vile kwa hasira na wivu maana alikuwa anaolewa na mwanaume mwingine

Liliana: suffer Robert suffer (anatabasamu)

Post a Comment

0 Comments