SCENE 58: -
HOSPITALINI: -
(Raphael anafika hospitali akiwa
amembeba mpenzi wake mikononi mwake na anaonekana akiwa amechanganyikiwa kwa
hali ile)
Raphael:
nesi naomba msaada wako
Nesi:
(anamjia) amefanyaje?
Raphael:
sijui nesi nimemkuta amelala sakafuni
Nesi:
(anaenda kuchukua machela na kurudi nayo)
Raphael:
ameumia Sana na wala haongei wala kufumbua macho
Nesi:
atakuwa sawa usijali (anamuita daktari)
naaomba utusaidie huyu mgonjwa yuko very critical
Raphael:
please msaidieni
Nesi:
hakuna kitakachoharibika kaka punguza presha
Raphael:
Ni mwanamke nimpendae Kwa dhati na ameishi maisha ya mateso sana sitaki
aendelee kuishi maisha ya mateso
Nesi:
atakuwa sawa…she will be fine you will see
Daktari:
(anakuja kutoa msaada na haraka anaamuru
mgonjwa apelekwe katika chumba cha wagonjwa mahututi) haraka mgonjwa
akimbizwe ICU
(Wauguzi na wasaidizi wao wanahangaika na
hali ya Liliana wakati huo raphael anaonekana kuchanganyikiwa kupita kiasi)
Raphael:
dear God I hope atakuwa sawa (anachukua
simu yake mfukoni kwake na kubonyeza namba ya kaka yake mkubwa)
(Simu inaita)
Gabriel:
oyaaa bwana harusi
Raphael:
kaka Liliana yupo hospitali
Gabriel:
(anaishiwa tabasamu) kwanini?
Imekuwaje? Amefanya nini?
Raphael:
sijui yaani I can’t explain kaka hali yake sio nzuri
Gabriel:
oh my God nambie uko wapi tunakuja
Raphael:
(anamuelekeza)
Gabriel:
okay tunakuja (anakata simu kasha
anamgeukia Anna, Bella na Michael) Liliana yupo hospitali
Anna:
what do you mean yupo hospitali? Amekuwaje?
Gabriel:
Rapha ahajaniambia vizuri ila najua tu hana hali nzuri
Bella:
sasa tunasubiri nini twendeni
(Haraka wanatoka nje wanapanda
gari moja na kuondoka zao)
HOSPITALI: -
(Raphael amekaa amejiinamia hana
raha ya maisha machozi yanamdondoka na anaonekana ana mawazo sana, wakati
amejiinamia anashtuliwa na sauti ya kaka yake mkubwa)
Gabriel:
Raphael?
Raphael:
(ananyanyuka na kumkumbatia kaka yake kwa
nguvu)
Gabriel:
it is okay she will be fine my brother
Raphael:
(anafuta machozi) asanteni Kwa kuja
Anna:
NO, it is okay shemeji, Liliana anaendeleaje? Na mtoto yuko wapi?
Raphael:
yupo na mama
Bella:
how is my cousin?
Raphael:
madaktari wameingia nae ICU bado hawajatoka yaani mwenzenu sielewi
Michael:
kwani imetokea nini mpaka yupo hapa? Ameugua ghafla?
Raphael:
nimemkuta sakafuni kazimia sasa sijui aliteleza yaani sielewi
Gabriel:
My God hiyo ni mbaya
Anna:
let’s hope for the best Nina Imani atakaa sawa
Raphael:
namuwazia mgongo asije akawa kilema
Bella:
no shemeji usiwaze kote huko ukiwaza hivyo ndo unazidi kuchanganyikiwa wewe
amini tu kuwa Mungu atamtendea liliana is very good woman…moyo wake upo so pure
anasamehe na anawapenda watu wote she is very good jamani kwakweli namuombea tu
apone
Raphael:
amina shemeji yangu
(Wanaendelea kupeana moyo na
Imani ya hapa na pale)
Daktari:
(anatokea chumba cha wagonjwa mahututi)
Raphael:
(haraka ananyanyuka na kumfuata)
daktari
Daktari:
come down
Raphael:
anaendeleaje?
Daktari:
ah
(Wote wanamuangalia Kwa umakini
na wasiwasi mkubwa)
Daktari:
haikuwa mbaya Kama tulivyodhani naona wote tulipaniki wakati analetwa
Bella:
kwahiyo
Daktari:
anaendelea vizuri na amezinduka pia anaendelea vizuri
Raphael:
naweza kumuona?
Daktari:
yes, sure ila ngoja tumtoe humu tumpeleke chumba cha mapumziko
Raphael:
saa ngapi sasa?
Daktari:
ona ni sasa hivi tu
(Machela inapita ikiwa imembeba
Liliana)
Raphael:
oh, baby you gonna be fine my love
Liliana:
(kimya hasemi kitu ila anatabasamu)
Raphael:
yes... (Anafurahi Sana)
Gabriel:
nilikuambia kuwa kila kitu kitakuwa sawa
Raphael:
sawa Asante Sana my brother
Gabriel:
usijali
Nesi:
mnaweza kumuona sasa
(Wanaingia chumba alichopo
Liliana)
Raphael:
oh, Mama Bianca wangu
Liliana:
(anaongea Kwa shida kidogo) ye…sss
Michael:
pumzika Kama hujisikii vizuri shemeji
Gabriel:
uliteleza?
Liliana:
(anatikisa kichwa kuashiria kukataa)
Michael:
mtu alikusukuma?
Liliana:
(kimya)
Raphael:
nani amekufanyia hivyo baby? Answer me please
Liliana:
(Kwa shida) ki…ng
Raphael:
hapohapo huyu mshenzi atajua hajui Leo ngoja
Bella:
tulia shemeji it is not worthy it…akae anajua tu amekukosa wewe Kama rafiki
hayo mengine achana nayo
Anna:
kabisa shemeji tumshukuru Mungu tu Kwa kila jambo maana hata kupona Kwa mpendwa
wetu ni jambo la kushukuru sana
Gabriel:
kabisa achana na King tupange harusi
(Wanacheka)
Raphael:
(anashusha pumzi Kama mtu aliyechoka
Sana)
0 Comments