SCENE 57: -
NYUMBANI KWA LILIANA: -
(Liliana
yupo nyumbani kwake peke yake anaonekana kufurahi ukimya wa mahali pale)
Liliana:
(anashusha pumzi kama mtu aliyechoka sana)
asante Mungu kwa haya…(anatabasamu)
maisha yangu ni hadithi ila pamoja na hayo nakushukuru Mungu wangu kwa
yote…asante hata kwa kuniruhusu kujisamehe mimi mwenyewe kwa kosa la kumuua Robert(anakunywa kahawa yake) asante hata kwa
kuniruhusu kupenda tena ingawa mara ya kwanza nilikuwa naogopa juu ya kupendana
na mtoto wa baba wa mwanangu ila ukaruhusu mimi na Raphael kuwa pamoja asante
Mungu…kwenye huu ukimya napenda kukushukuru sana Mungu wangu kwa fadhili na
wema ulionitendea asante hata kwa kunikutanisha na mama yangu Bianca akanilea
nikasahau ya kale yote (anasikitika
kidogo) asante pia kwa maisha ya Bianca Mungu wangu…asante pia hata kwa
maisha ya wazazi wangu walioniacha nikiwa mdogo nikapitia yale yote naamini
hiyo yote ilikuwa ni kwa makusudi yako ili ujitwalie utukufu,asante Mungu wangu
jina lako lihimidiwe Asante sana
(Kengele ya mlango wake inalia)
Liliana:
itakuwa Raphael (ananyanyuka na kwenda
kufungua mlango) kari… (anasahangaa
sio Raphael bali ni yule rafiki yake Raphael aliyepinga uhusiano wa Raphael na
Liliana) shemeji?
Rafiki
2: naweza kuingia?
Liliana:
yes, sure… (anaufungua mlango kuruhusu
rafiki huyo kuingia)
Rafiki
2: hivi unanijua jina langu?
Liliana:
hapana (huku anaenda jikoni)
nikupatie nini juisi, kahawa, maji au nini?
Rafiki:
no thanks
Liliana:
(anarudi alipo rafiki)
Rafiki
2: naitwa King
Liliana:
sawa shemeji
King:
niite King tu
Liliana:
sawa
King:
(anamuangalia kwa uchu) mnafunga lini
hiyo ndoa?
Liliana:
baada ya miezi mitatu
King:
(anaguna kama mtu aliyekasirishwa na
taarifa hiyo)
Liliana:
(anagundua) are you okay?
King:
ofcourse (anakaa kimya kidogo) hivi
umempendea nini Raphael
Liliana:
(kwa kuhoji) excuse me?
King:
utatembeaje na baba na mtoto huku tupo sisi wanaume tunaojitambua na kujielewa?
Liliana:
kwani Raphael hajielewi?
King:
ndio
Liliana:
kivipi?
King:
anajua kabisa wewe ni mama yake halafu anapita mulemule alipopita baba yake mtu
kama huyo unaona anajielewa
Liliana:
nitajifanya sijasikia maneno yako
King:
Liliana I love you nakupenda sana nataka uwe mpenzi wangu yaani natamani sana
kampani yako hata sasa hivi na nimekuja kwa ajili hiyo
Liliana:
what are u talking about?
King:
wewe ni mtu mzima na unajua fika kabisa nachoongelea
Liliana:
najua ndio unachoongelea ila sikuelewi basi ndo maana ulikuwa unatukana siku
ile kumbe una lako jambo?
King:
siku ile nilisema ukweli mtupu
Liliana:
get out of my house now
King:
(anajaribu kumshika) sijawahi
kukataliwa na mwanamke
Liliana:
una upuuzi mwingi sana ndo maana uko hivyo
King:
nipoje?
Liliana:
just get out right now sitaki hata kukuona
King:
nakupenda na nimekuja kula tunda hakuna atakayejua kama nimekuomba na ukanipa
Liliana:
Tokaaaa
King:
(anamlazimisha kumvua nguo)
Lilian:
we kichaa nini? (Anamsukuma kisha anapata
upenyo kukimbilia chumbani kwake anapanda ngazi haraka Sana anafika chumbani
kwake anafunga mlango kwa ndani)
King:
acha utoto bwana unaogopa mwanaume kwani wewe ni bikra?
Liliana:
nampigia Rapha simu
King:
(anacheka kwa kejeli) unadhani
namuogopa?
Liliana:
naomba uondoke jamani sikutaki
King:
jamani unadhani kuna mtu atajua kuwa tumepeana? na tutaendelea hata ukiolewa na
huyo Rapha
Liliana:
sina mpango wa kumsaliti mume wangu siolewi na Raphael ili nije nimsaliti
King:
acha kujifanya mtakatifu huna jipya unataka pesa hata mimi ninazo nitakutunza
mimi hata sikuoi maana nina mtu wangu nampenda sana yaani mimi na wewe tutakuwa
tunapeana mambo mazuri tu unajua kukaa na mtu mmoja inaboa ee utaona tu hata
wewe utakavyokuwa unaboreka na huyo Rapha
Liliana:
nasema hivi naomba uondoke sitaki na wala sipenda upuuzi wako
King:
please baby allow me to enjoy your body mtoto una figa tamu mpaka nikiiongelea
tu najaa mate ndo maana baba na mtoto wamedata hapo
Liliana:
Oh God please help me
King:
jamani Liliana si ufungue tena humo chumbani ndo pazuri kweli
Liliana:
(anaanza kulia) Raphael where are you
my love…uko wapi mpenzi wangu
King:
hayupo yule nae si fala
Liliana:
wewe sijui King Sijui nani naomba uende zako
King:
duh haya bwana Kama umekataa jamani ila natamani tamuuuu
Liliana:
ondoka (anafyonza)
(Kuna ukimya kwa muda)
Liliana:
(anafungua mlango Kwa uangalifu) afadhali
ameondoka
(Ghafla King Anamshika mkono)
King:
nimekukamata (Anacheka Sana)
Liliana:
niache (kwa bahati mbaya anateleza na
kuanguka vibaya kwenye ngazi, anabiringita mpaka chini anapofika chini
anajibamiza kichwa na kuzimia)
King:
(anaduwaa) He! Kafaa? (Anashuka ngazi haraka anafika anashika
mapigo ya moyo) hakuna mapigo ya moyo au amekufa? Mungu wangu nisije nikawa
nimemuua Mimi (anaguna) yaani
kateseka huko ndo nije nimuue Mimi? Eeh Mungu wangu ngoja niondoke kabla ya
sijaonwa na mtu yoyote (anakimbia)
BAADA YA DAKIKA 20: -
(Raphael anafika nyumbani hapo akiwa amebeba
maua mazuri anabonyeza kengele ya mlango mara kadhaa bila majibu)
Raphael:
huyu yuko wapi? (Anaita) mama Bianca?
(Kimya)
Raphael:
(anasukuma mlango unafunguka, anaingia
ndani anakuta Liliana amelala sakafuni na damu zinatoka kichwani anachanganyikiwa
anaangusha maua na kumkimbilia mpenzi wake) baby… nini mama
Liliana:
(anafumbua macho kwa shida)
Raphael:
nani? Kafanya haya mama?
Liliana:
(anapoteza fahamu tena)
Raphael: (anambeba na kumpeleka kwenye gari lake anamlaza anapanda kwenye gari
kisha analiondoa kwa kasi sana) you will be fine my love I promise you…you
gonna be fine I swear (anaendesha gari
kwa kasi sana) Everything will be fine my love...Mungu yupo
Liliana: (hali yake sio nzuri kabisa)
0 Comments