SCENE 60: -
FINALE: -
BAADA
YA MIEZI 10: -
(Ni asubuhi nyingine njema Kama ilivyokusudiwa
na Mungu muumbaji, Liliana akiwa katika hali ya ujauzito tena uliofikia hatua
ya kujifungua, anaingia katika moja ya supermarkets za mumewe kufanya manunuzi
ya nyumbani, wakati anaingia simu yake ya mkononi inaita)
Liliana:
(anaipokea) baby
Raphael:
nimekuja nyumbani mara moja kukuona haupo umeenda wapi na hii hali baby?
Liliana:
nipo Ra-Li supermarket baby
Raphael:
okay nakuja hapo usiondoke
Liliana:
(anacheka kidogo) baby bwana iam okay
nanyoosha viungo tu jamani
Raphael:
no baby unatakiwa upumzike bwana nakuja hapo (anakata simu)
Liliana:
(anatikisa kichwa kisha anatabasamu)
ila huyu kaka (anacheka)
(Anakaribishwa Kwa heshima zote)
Liliana:
asanteni jamani hamjambo? (Anaanza
mahemezi ya hapa na pale)
(Sauti ya kiume kutoka nyuma yake
inamuita)
Liliana:
(anageuka kuangalia ni nani) nani?
King:
Mimi hapa shemeji
Liliana:
oh, Shem za siku?
King:
nzuri Sana (anatabasamu) hongera Kwa
harusi lakini pia naona mambo sio mabaya
Liliana:
(anaangalia tumbo lake) eeh shemeji
King:
hongereni Sana na samahani kwa yote
Liliana:
oh, shemeji hayo ni ya kale tuachane nayo sio lazima kukaa kukumbushiana
King:
kwakweli ila lile jambo limeharibu urafiki wangu na Rapha
Liliana:
hana kinyongo tena namjua mume wangu habebi vinyongo
King:
eti eeh basi Kama ni hivyo safi sana
Liliana:
kuwa na Amani
King:
basi sawa acha niendelee na mahemezi ya hapa na pale
Liliana:
karibu Sana shemeji
King:
nipo na wife nay eye yupo kama wewe
(Wanacheka)
Mrs.King:
(anaugulia) baby
King:
(anakuja anakimbia) vipi baby
Mrs.King:
tumbo
Liliana:
(anakuja kuwasaidia ile anapiga hatua nae
anasikia uchungu ghafla)
Wafanyakazi:
(wanakimbia kuwasaidia)
Raphael:
(anafika) nini kinaendelea hapa
Mmoja
wa wafanyakazi: queen anaumwa
Raphael:
oh My God (anakimbia kumuona anakutana na
King) aisee na wewe, mkeo amepata uchungu
King:
yes
Raphael:
(anambeba mkewe) lets go twendeni
hospitali
(Haraka wanapanda gari kuelekea
hospitali baada ya mwendo kidogo wanafika hospitali na kama kawaida manesi
wanawapokea vizuri, wanawake wale wawili wanapelekwa leba wakati wanaume
wanabaki nje kusubiria habari njema)
King:
(Kwa Raphael) hatujaonana mwaka sasa
ndugu yangu
Raphael:
ni kweli
King:
nisamehe Sana Kwa lile tukio halafu sio hilo tu hata la kumchukulia mkeo Malaya
kutembea na baba na mwana
Raphael:
oh, King Hilo limepita ndugu yangu tugange yajayo rafiki yangu…nimekusamehe
ondoa shaka
King:
(anampa mkono)
Raphael:
(anamvuta) come here (anamkumbatia)
(Wakati wamekumbatiana ndugu zake
Liliana pamoja na Raphael wanafika mahali pale)
Bella:
shemeji?
Rphael:
naam Shem
Anna:
huyu vipi?
Raphael:
ah bado tu ndugu yangu
Gabriel:
don’t worry she will be fine
Michael:
Na King Anafanya nini hapa?
King:
kaka
Raphael:
it is okay (Kwa Michael) yupo hapa
maana na yeye mke wake kaingia leba na mke wangu
Lydia: (anafika hospitali hapo)
Wote:
(wanamsalimia)
Lydia:
marahaba
Raphael:
Bianca yupo wapi?
Lydia:
shule
Gabriel:
mbona umekuja umetoa macho hivyo?
Lydia:
(anacheka) nimeambiwa bibie kapata
uchungu vipi anaendeleaje?
Raphael:
ndo tunasubiri hapa
Lydia:
she will be fine
Raphael:
I know mama but iam very nervous
Michael:
tunaelewa bwana ndo mara ya kwanza kuwa baba ni lazima uwe na mhaho wa adabu
(Wanacheka)
Raphael:
yaani nyie mnanichanganya tu bwana
Gabriel:
wewe nae tusicheke
Lydia:
unajua mwenzenu yupo serious amechanganyikiwa
Michael:
mama take it easy jamani mbona hivyo?
Gabriel:
mama is going to be a very sexy granny
(Wote wanacheka)
Raphael:
let’s get serious guys
Michael:
hey chill nini mbaya jamani?
Raphael:
akili yangu haipo
Gabriel:
then….
(Sauti ya kichanga inasikika
kutoka katika chumba walichopo mke wa King na liliana)
Raphael:
(anafurahi Sana) Oh My God mwanangu
King:
(anafurahi pia)
(Vilio vya watoto vinasikika, vilio
vile vinaleta furaha Kwa watu wote waliokuwepo hapo)
Raphael:
wow…iam a father
Gabriel:
(huku anatabasamu) yes, my little
brother
Raphael:
Asante Mungu
Lydia:
(anafurahi Sana mpaka anajikuta anatoka
machozi)
Anna:
aunt vipi mbona machozi?
Lydia:
sikuwahi kufikiri Kama hata siku moja nitawahi kufurahia furaha ya Liliana
nilimuona Liliana Kama ni shetani aliyekuja kuharibu furaha ya familia yangu (anasikitika) Liliana ni shujaa
ameteseka sana katika maisha yake nimesikia hadithi ya maisha yake na nimeelewa
ule usemi unaosema hata kama usiku ukiwa mrefu vipi lazima papambazuke naona
kwa Liliana pameshapambazuka (kwa Raphael)
hongera mwanangu kwa kuwa baba
Raphael:
Asante mama (anamkumbatia)
(Wote waliopo pale wanakumbatiana
huku kila mmoja anaonekana kuwa na furaha isiyo na kifani)
Dokta:
(anatoka anawakuta wamekumbatiana)
naona mmeshapata jibu
Lydia:
yes tumepata
Dokta:
Mrs.Liliana amejifungua mtoto WA kiume na Mrs. King amejifungua mtoto wa kiume
pia hongereni sana
(King Na Raphael wanakumbatiana)
Lydia:
Asante Mungu finally everyone is happy
Anna:
tunaweza kumuona I mean kuwaona?
Dokta:
yes, sure please go ahead
(Wanaingia Kwa pamoja kumuona Liliana pamoja
na mke wa King)
Raphael:
oh, my wife
Liliana:
it’s a boy
Raphael:
(huku anatabasamu) I know baby I know…hongera
Sana my love
Liliana:
hongera kwetu sote mpenzi
Anna:
hongera Sana cousin
Liliana:
thank you cousin
(Watu wote waliopo hapo
wanawapongeza wazazi Kwa kuleta furaha kwenye familia hizo mbili)
Lydia:
hongera Sana
Liliana:
Asante Sana mama
Liliana:
(anaongea mwenyewe moyoni) all is
well…it ended well and iam so proud…yes nilipitia magumu sana tangu wazazi
wangu walipofariki nilitukanwa nilifanyishwa kazi kwenye nyumba yangu mwenyewe,
nilibakwa nilinyimwa chakula lakini pamoja na yote Mungu hakunitupa nikampata
mama yangu Bianca (anatabasamu kidogo)
mama yangu Bianca akanilea akanisomesha niliishi maisha mazuri ghafla nikaona
usemi uliosema baada ya dhiki faraja nikafarijika sana nikamtukuza Mungu sana
lakini siku moja tu nikaamua kupenda hapo ikawa mwanzo wa mateso yangu bwana
yule aliniharibia maisha yangu kwa kunipa gonjwa ambalo ni tishio lakini pamoja
na hayo Mungu hakuniacha nikaendelea kufurahi sana kwasababu mama yangu
alikuwepo kunipa moyo lakini furaha yangu haikudumu hawara yangu akamuua mama
yangu sikukubali na mimi nikawa na kisasi moyoni mwangu kilichopelekea kumuua
hawara yangu sitasahau mateso niliyoishi nayo nikafungwa miaka ila ndani ya
miaka minne nikatoka silalamiki nilipotoka ndo furaha ikanizidia maana nilipata
tulizo la moyo…(huku anamuangalia mumewe)
mume wangu Raphael mtoto wa hawara yangu pamoja na kwamba watu walimwambia
asinioe hakuwa sikiliza hata mimi mwanzoni niliona kuwa haitakuwa vizuri mimi
kuwa nae yeye alitumia nguvu nyingi sana kunishawishi kuwa kila kitu kitakuwa
sawa na leo kweli kila kitu kipo sawa nimezaa na baba na mtoto and all is well
ndo Mungu alivyopanga asante sana jehova kwa upendo wako sina cha kukurudishia
ila nitaziimba sifa zako siku zote za maisha yangu
Bella:
(anamshtua) wewe binamu unawaza nini?
Liliana:
hapana siwazi kitu just nafurahi ukuu wa Mungu
Gabriel:
Mungu wetu ni mzuri sana
Michael:
kabisa
Raphael:
hakika
King:
hakika
Anna:
kabisa
Lydia:
kila kitu kipo sawa (anambeba mtoto
mchanga) anaitwa nani mtoto?
Raphael:
bado hatujamuita jina lolote hatukupanga
Gabriel:
au hamkupanga mtoto wa kiume
Liliana:
(anacheka kidogo) hapana shemeji sisi
tulijiandaa kwa ajili ya mtoto yeyote
Raphael:
yes
Lydia:
ataitwa Robert
(Wanashangaa)
Raphael:
mama
Lydia:
au?
Anna:
Mimi naona sawa tu
Liliana:
(anacheka)
Lydia:
msamhee Robert Liliana mwanangu
Liliana:
(anatabasamu) sawa nimemsamehee na
mwanangu ataitwa Robert
(Wanafurahi Sana)
Bianca:
(anakuja akitokea shuleni) mama
Raphael:
(anambeba) umepata mdogo wako
mwanangu
Bianca:
(anafurahi Sana)
(Wote walipo hapo wanafurahi Sana na kila
mmoja anaonekana kuridhika na hali ile ya wakati ule)
Raphael:
all is well
Gabriel:
tungekuwa na shampeni sasa
(Wanacheka na kufurahia maisha
kwa ujumla)
THE END
0 Comments