SCENE 1: -
(Ni
usiku mmoja wa giza totoro,na mvua kali inanyesha,katika mtaa mmoja wa pembeni
ya mji anapita mama mmoja anayeonekana
kubeba mtoto mchanga na kwasababu ya mvua kali anaonekana kukimbia na kutafuta
nyumba ya kujikinga na mvua hiyo,baada ya kuhangaika kwa muda mrefu hatimaye
anafika kwenye nyumba moja ya kifahari,kwakuwa mageti yamefungwa,anaamua
kutandika khanga yake kisha anaondoka huku anamuacha mtoto mahali pale,lakini
kabla ya kuondoka anabonyeza kengele ya geti ya nyumba ile ya fahari,anabonyeza
mara kadhaa kisha kwa mbali anasikia kama kuna mtu anafungua mlango kwa ndani
anakimbia na kujibanza sehemu huku akiangalia hatima ya mtoto wake mchanga,wakati
huo amejificha anatoka mwanamke mmoja pamoja na mwanaume wawili hao wanaonekana
ni wanandoa na wamiliki halali wa nyumba hii)
Mwanamke :( anaonekana ana usingizi Sana) jamani nani tena amegonga geti
tumetoka hatumuoni
Mwanaume: sijui nani? (Anamuita mlinzi) Edson…
Edson :( anatoka) naam boss…
Mwanaume: unaweza ukawa unajua
mtu aliyekuwa anatugongea?
Edson: hapana boss, sijamuona …
Mwanamke: ah…sawa, Kennedy
umeshajua kuwa hakuna mtu embu turudi ndani bwana mi nina usingizi…
Kennedy :( anacheka) Kedness, kwa usingizi jamani unataka kuzidi haya twende
(Kabla
hawajapiga hatua kwenda popote wanasikia mtoto kwa pembeni Analia na wakati huo
wote mama mzazi wa mtoto huyo yupo sehemu pembeni amejibanza akiangalia hatima
ya mtoto wake)
Mama :( anaonesha masikitiko) nisamehe mwanangu, unadhani nitafanyaje?
sina uwezo wa kukulea…baba yako amenikataa na kunitukana matusi mengi na mabaya
unadhani hata mimi napenda kukuacha hapa? baba yako kakukataa, bibi na babu
yako hawakutaki, waliniambia hata kabla sijakuzaa kwamba inanipasa nikutoe
mwanangu lakini mimi kiubishi nimekuzaa ila sina uwezo wa kukulea mwanangu,
namuomba Mungu hawa watu wakuchukue tu uwe mtoto wao…
(Wakati huo Keneddy na mkewe Kedness wanashangazwa na mazingira aliyopo
kichanga hicho)
Kedness: maskini, na baridi lote
hili…mwanamke gani mwenye roho ngumu kamuacha mtoto hata kumfunika?
(Mama wa
mtoto Analia kwa uchungu)
Kennedy: yaani dah
Kedness :( anamnyanyua yule mtoto) halafu kazuri kweli…
Keneddy:ni wa jinsia gani?
Kedness :( anamfunua kidogo) ni wa kike…
Kennedy: kwanzia leo atakuwa mtoto
wetu
Kedness: wewe ni bora tukatoe
taarifa polisi ili kusije kukawa na kesi, anaweza kuja mama yake na mtoto na
kusema kuwa tumemuiba na tukapata kesi kubwa mume wangu
Kennedy: sawa haina shida ila
polisi wakikosa mama yake Ariana wetu atapata mdogo wake
Kedness: ama hakika Ariana
atafurahi sana maana alitaka sana kuwa na mdogo
Kennedy: mvua naona inazidi
unaonaje tukaingia ndani?
Kedness: kwanza tumpe mtoto wetu
mpya jina...
Kennedy: wewe umesema kuwa mpaka tukatoe
taarifa polisi
Kedness: sawa ila polisi wanaweza
wakatupa tumlee kwahiyo tunachotakiwa kufanya ni kumpa jina tu sio kwa ubaya…
Keneddy: sawa Keddy…tukisoma
kutoka tunaona Mussa alizaliwa na kuwekwa katika mazingira haya haya
tuliyomkuta huyu mtoto
Keddy: Ken, unamaanisha tumuite mtoto
Mussa?
(Kwa
pamoja wanacheka)
Ken: hapana mama Ariana, Mussa
alikuwa ana dada yake tumuite mtoto Miriam...
Keddy: Safi…Miriam linafaa
(Mama wa
mtoto anaonekana kuridhiana na jina la mtoto)
Mama: Miriam…jina zuri sana…hata
mimi nimelipenda...
(kwa
Kennedy na mkewe)
Ken: bwana akamfanye kuwa
mtumishi wake (anamshika na kumuinua juu)
Miriam ukawe faraja katika familia yetu, nakutamkia mema katika maisha yako,
Mungu aliyewakumbuka waisraeli jangwani akakukumbuke hata wewe na maisha yako,
bwana akakutendee yaliyo mema na hila zote za shetani zikakupite mbali mwanangu,
nakukaribisha nyumbani kwangu na hata kama si mwanangu, nitakulea na kukupa
kila kitu, elimu nzuri na kila kitu utakachohitaji katika maisha yako
Keddy: amina mume wangu sasa
tumepata binti mwingine
Mama wa mtoto :(akiwa bado amejificha) amina (anajikuta anatokwa na machozi)
Ken: twende ndani mke wangu bwana
ametupa mtoto wa pili katika njia zake alizopanga mwenyewe
Keddy: Amina mume wangu
Mama :( anaondoka zake na kwenda pasipojulikana)
(Ken na
mkewe wanaingia ndani na kumuamsha binti yao mwenye mkubwa mwenye kati ya miaka
kumi au kumi na mbili)
Ken: Ariana…unamuona mdogo wako
anaitwa Miriam
Ariana :( anafikicha macho na anaonekana ana usingizi sana) mmetoa wapi?
Keddy: Mungu katuletea
Ariana :( anaguna) amewaleteaje?
Ken: tumemkuta hapo nje mwanangu
yaani ni miujiza tu ya mungu mwenyewe
Ariana :(anamuangalia mtoto) sawa ni mzuri…
Ken :( tabasamu linapotea usoni mwake) mbona unaonekana huna furaha?
Ariana: nataka mdogo wangu wa
kiume?
Keddy: mwanangu ni jambo la
kumshukuru Mungu kuwa ametuletea mtoto na sisi familia yetu iwe kubwa tafadhali
usiwe hivyo.
Ariana: samahani mama
Ken: usijali mama, we lala kesho
shule tutazungumza kesho asubuhi
Ariana: sawa (anajifunika blanketi)
(Ken na
mkewe wanatoka chumbani humo wanazima taa kisha wanaenda chumbani kwao,
wanapofika wanamvalisha baadhi ya nguo za Ariana za utotoni maana walizitunza
na kumfunika mtoto vizuri kisha wanamlaza pembeni yao)
Keddy: kile kitanda cha Ariana tulikigawa,
itabidi tumnunulie kitanda chake mwenyewe
Ken :( anacheka) naona jinsi unavyopanga utasema mtoto keshakuwa wa kwako,
itakuwa kesho kama mama yake atatokea?
Keddy: Mungu ametupa mtoto baada
ya kumtafuta mtoto Zaidi ya miaka kumi kila mara tulijaribu kupata mtoto
mwingine Zaidi ya Ariana ilishindikana leo hii kwa namna ya pekee mtoto
ameachwa nje ya geti letu Mungu alikuwa anajua kuwa tunahitaji mtoto ndo akatupa
huyu mtoto kwa njia ya ajabu kweli mungu ni mkuu na njia zake hazichunguziki…
Ken: amina mke wangu kesho
asubuhi tutaenda polisi na kutoa taarifa juu ya huyu mtoto
Keddy: sawa, ila kuna kitu
kingine kinanitatiza, Ariana mbona hajafurahi huku alikuwa anahitaji mdogo wake?
Ken:mpe muda si unajua kuwa
imekuwa ghafla sana, tusubiri kesho tuone itakuwaje?
Keddy: tusubiri…tu (anamuangalia mtoto aliyekuwa kalala fofofo)
yaani sijui akikojoa usiku tutamvalisha nepi gani hatuna pampers wala nepi…
Ken:(anacheka) mpaka unatamani Mungu angekuotesha kuwa utapata mtoto
usiku kwahiyo jiandae
Keddy:(anacheka) yaani nimempenda Miriam ana sura nzuri kweli (anamuegemea
mumewe kifuani)
Ken: naomba mtu yeyote asijue
kuwa Miriam sio mtoto wetu, tutamlea kama vile mtoto tuliyemzaa wenyewe…
Keddy: sawa mume wangu
sitamwambia yeyote, ila watu hawakuniona na mimba(anacheka)
Ken:(anacheka) Mungu atatutetea
Keddy:(anatabasamu) haya mume wangu…usiku mwema baba
Ken:na kwako pia
(Kila
mtu anageukia upande wake na kulala, wakati huo na mtoto nae kalala fofofo)
2 Comments
Hope mnaenjoy..endeleeni kunisapoti..nawapenda
ReplyDelete❤️🔥
ReplyDelete