SCENE 17: -
(Mchana mtulivu, jua linawaka kwa
mbali, upepo unavuma vyema ndege wanapita mawinguni na kila kitu kinaonekana
katika hali nzuri, Miriam amekaa peke yake chini ya mti mmoja uliopo chuoni
kwao akiwa anajisomea mwenyewe. Wakati anajisomea anakuwa ana mawazo Fulani)
Miriam:
yaani mimi sijui nani aliniambia nikubali huu ujinga ona sasa nampenda Jeremy
na sipo tayari kuachana nae…
Vanessa:(anakuja anakaa pembeni yake)
Miriam:(kwa kuwa anakuwa na mawazo hasikii)
Vanessa:(anamgusa) Miriam?
Miriam:(anashtuka) abee
Vanessa:
unawaza nini?
Miriam:(anashusha pumzi)
Vanessa:
nini?
Miriam:
nampenda Jeremy
Vanessa:
(anacheka kwa nguvu) eh bwana dah!!!
Mambo sio ndo hayo… (anacheka kidogo tena)
sasa kuna shida gani ukimpenda?
Miriam:
Vanessa wewe unajua kabisa tangu mwanzo inshu ilikuwa ni kujifanya kuwa nae ili
asijidhuru lakini sasa kila siku zinavyozidi kwenda ndo nataka kuendelea kuwa
nae…nampenda nipo serious nae, yaani hivi unadhani wazazi wa pande zote mbili
watanionaje mimi?
Vanessa:
wataelewa kuwa penzi kikohozi jamani kinampata mtu yeyeote wewe tulia na
uchukulie poa tu...kwani wewe ulipenda si imejitokeza tu?
Miriam:na
wala sikupanga kuwa nitampenda imetokea tu
Vanessa:
sasa je…wewe tulia tu na uendelee kula good time…zikiisha unaongeza… (anapiga vigelegele)
Miriam:
hivyo vigelegele vipi?
Vanessa:
nachukulia picha siku mnaoana na baby Jeremy…
Miriam:
yaani hiyo itasubiri sana maana (anaguna)mpaka
nimalize shule
Vanessa:
wewe si ulisema Jeremy anataka kuoa ndo maana aliwaambia wazazi wake kuwa
wamtafutie mchumba
Miriam:(anacheka kidogo) mimi aliniambia kuwa
yupo tayari kusubiri…nikimaliza kusoma na nikawa tayari kwa ndoa basi tutafunga
ndoa
Vanessa:
mmeshapanga mpaka ndoa
Miriam:
yeye ndo huwa anazungumzia sana
Vanessa:(anacheka) by the way yaani mnapendezeana
sio yeye na Ariana sema siku Ariana akijua wewe ndo unamchukulia bwana na hivi
hakupendi sijui itakuwaje
Miriam:
yaani mimi mwenzenu sijui itakuwaje…
Vanessa:na
Ariana ana gubu yule sijui tu…hivi siku hizi ameacha kwenda club
Miriam:
hajaacha yaani mama na baba wanaona kuwa akiolewa atatulia maana sio kwa sifa
mbaya anazoiletea familia
Vanessa:na
ni mhuni juzi tu nilimuona anaingia gesti na baba Fulani hivi
Miriam:(anashangaa) wewe, enhe ikawaje?
Vanessa:
sasa iweje? mi nikapita zangu nikaondoa nilikuwa napita tu
Miriam:(anasikitika kidogo) yaani sijui ndo
stress zenyewe za kuachwa na Jeremy
Vanessa:
wala…wewe unamjua Ariana na usivunge humjui dada yako…na sio kwamba anataka
kuolewa bado anataka kula ujana, ndo maana mimi naona wewe na Jeremy mnaendana
maana wote mnajiheshimu
Miriam:(anatabasamu) yaani nampenda Jeremy na
ile rangi yake
Vanessa:(anacheka sana) angalia usije ukawa
chizi…
Miriam:
usimwambie mtu lakini…yaani iwe siri yetu rafiki yangu
Vanessa:
usijali mami
(Kwa mbali anakuja kijana mmoja)
Vanessa:
Fredrick huyo hapo
Miriam:
yuko wapi
Vanessa:
anakuja utamuona tu…enhe!!unajua kuna kipindi ulianzaga kumpenda Fredrick sema
nay eye sasa akawa anakuletea pozi
Miriam:
hilo ndo kosa lake yaani kunitongoza anitongoze yeye halafu aanze kuniletea
pozi utasema sijui ni mwanamke Fulani
(Wanacheka)
Vanessa:(kwa kunong’ona) amefika
Fredrick:(anawafikia)
we Miriam…mbona hata simu zangu hupokei una shida gani?
Miriam:(anacheka)
sasa hapo nikujibuje? okay sijisikii kuzijibu
Fredrick:
wewe mtoto siku hizi umeota mapembe ee
Miriam:
sikiliza nikwambie wewe sijui Fredrick sijui Fred huna mamlaka ya kuniongelesha
jinsi unavyoniongelesha sasa hivi…yaani ni kwanini unaniongelesha kama umenizaa
au una mamlaka na mimi?
Vanessa:(kimya)
Miriam:
wewe ni nani kwani?
Fredrick:
mimi ni nani kivipi inamaana hujui mimi ni nani?
Miriam:
wewe ni Fredrick
Fredrick:
mimi ni mpenzi wako
Miriam:
hakukuwahi kuwa na mahusiano kati yetu na wala hayatawahi kuwepo
Fredrick:(anamfyonza) unajifanya mtoto wa
mchungaji huku unabadilisha wanaume kama nguo
Miriam:
una uhakika na unachokisema?
Fredrick:
sasa kama umeniruka si inamaana una mwanaume mpya tena katika maisha yako
Miriam:(ananyanyuka) Vanessa twende (anataka kuondoka)
Fredrick:(anamvuta) unaenda wapi
Miriam:(anamsukuma) niache
Fredrick:(anamvuta kwa nguvu)
(Sauti ya Jeremy inatokea nyuma
yao)
Jeremy:
kuna nini kinaendelea hapo?
Vanessa:(anageuka) eh bwana ee kama staa kwenye
muvi…(anacheka)
Jeremy:(anawaendea walipo) kuna nini?
Fredrick:
hayakuhusu…
Jeremy:
sikuulizi wewe...namuuliza Miriam (kwa Miriam)
honey kuna nini?
Miriam:(macho yamekuwa mekundu sababu ya hasira)
Jeremy:
Miriam!!???
Miriam:(kwasababu ya hasira machozi yanamtoka)
Fredrick:
oh, kumbe haka ndo kamwanaume ambako kamekufanya unikatae mimi na kusahau
tulipotoka
Vanessa:
muongo hawakuwahi kuwa na mahusiano
Jeremy:(kwa Miriam na Vanessa) twendeni
(Wanaondoka)
Fredrick:
unadhani mtafika mbali basi tunawahesabia siku tu…shenzi nyie mtaachana tu (anaondoka)
Jeremy:
(anamgeukia Fredrick anamsikitikia)
Miriam:
(amejaa kifua kwa hasira)
Jeremy:
baby take it easy (anafika alipoegesha
gari lake na kutoa chupa moja ya maji) kunywa maji kidogo, tulia baby (anamuangalia Vanessa) si mmemaliza
vipindi…twendeni mkale kisha nitawapeleka nyumbani
Vanessa:
okay shemeji
(Wanapanda
kwenya gari kisha wanaondoka mahali pale)
Jeremy: (kwa Miriam) relax baby
0 Comments