SCENE 16: -
(Asubuhi ya siku nyingine Miriam
yupo chumbani kwake anaonekana ana maumivu Fulani kwani anaugulia sana na
Analia sana, Mary anasikia kilio hicho kwa mbali)
Mary:
mwanangu Analia nini tena jamani? (Anaingia
chumbani kwa Miriam) Miriam…mwanangu nini mama?
Miriam
:( anashika tumbo lake) naumwa tumbo ma mdogo
Mary:
limeanza tena…(anaguna)hata mimi nilipokuwa msichana nilikuwa naumwa sana tumbo
pole sana mwanangu
Miriam:
asante
Mary:
ngoja nikamuite mama yako (anatoka)
(Baada ya muda Mary na keddy
wanakuja)
Keddy:
mwanangu nini tena?
Miriam:
naumwa tumbo la hedhi mama
Keddy:
pole…ngoja nikuletee dawa angalau litulie kidogo
Miriam
:( anaitikia kwa kichwa akimaanisha
kukubali)
Keddy
:( anatoka anaelekea sebuleni)
(Kengele ya mlangoni inalia)
Keddy:
nani tena? (Anaenda kuufungua mlango)
oh Jeremy baba karibu
Jeremy:
Asante… (Anaingia)
Keddy:
Ariana bado kalala Nina uhakika umekuja kumuona yeye…si ndio baba
Jeremy
:( hajibu kitu anabaki anatabasamu)
Keddy:
karibu uketi nikamuite mchumba wako
Jeremy:
hapana mama usimsumbue kwani mama siruhusiwi kuja kuwasalimia hata nyie?
Keddy:
unaruhusiwa baba…anyway ngoja nikampe shemeji yako dawa anaumwa tumbo
Jeremy
:(anasema moyoni) nimekuja kumuona Miriam
na sio Ariana, mpenzi wangu alinipigia simu akaniambia anaumwa sana sikuweza
kuvumilia nikaona nije tu nimuone…hapa natakiwa kutafuta kisingizio nimuone Miriam
wangu, sijui nisemeje(anawaza)
Keddy
:( anapiga hatua)
Jeremy:
mama naweza kumuona Shem…
Keddy:
sawa ngoja nimwambie akae vizuri
Jeremy:
Asante mama... (Anamfuata nyuma)
Keddy
:( anatabasamu) wewe nae nimekuambia
ukae hapa nimuone Kama amekaa vizuri ndo uje
Jeremy
:( anacheka) haina sawa mama
Keddy
:( anaingia chumbani kwa Miriam) ebu
kaa vizuri shemeji yako anakuja
Miriam
:( anatabasamu kisha anajisemea moyoni)
amekuja yaani hana uvumilivu huyu… (Kisha
anajiweka vizuri)
Mary
:( anamuangalia Miriam usoni) mbona
kama umefurahi Fulani kusikia shemeji yako anataka kukuona?
Miirriam:
hamna kitu ma mdogo jamani…kwanini nifurahi?
Keddy
:( anamuita Jeremy)
Keddy:
Jeremy?
Jeremy:
naam mama
Keddy:
haya njoo
Jeremy
:( haraka anaingia ndani)
(Miriam na Jeremy wanatabasamiana
mara baada ya kuonana)
Jeremy:
shemeji…
Miriam:
abee…shikamoo?
Jeremy:
marahaba shemeji yangu…unaendeleaje?
Miriam:
vizuri kidogo
Keddy
:( anampa dawa na maji) haya kunywa
Miriam
:( anapokea) asante mama (anazinywa)
Keddy:mi
narudi kulala…shemeji yako huyu hapa
Miriam:
sawa mama
Keddy
:( anatoka)
Mary
:( anagundua kitu) mpo sawa kweli
nyie
Miriam:
ndio ma mdogo kwanini unasema hivyo?
Mary:
sijui nawaonaje tu Kama vile kuna kitu Fulani
Jeremy:
hamna kitu ma mdogo
Mary:
(anaguna kidogo) haya bwana ila
shauri yenu… (Anatoka)
Jeremy
:( anambusu Miriam shavuni) pole mke
wangu…umeanza usiku?
Miriam:
ndio nimeanza usiku yaani sijalala sidhani Kama nitaenda chuo leo
Jeremy
:( anatoa chocolate mfukoni)
nimekuletea chocolate
Miriam:
Asante… (Anapokea)
Mary
:( amejibanza anawaangalia) Mungu
wangu hawa watoto wana mahusiano na ndo maana Jeremy kaja watakuwa wamepigiana
simu…Miriam anamsaliti Ariana nah ii sio nzuri… (anasikitika sana)
Miriam:
sasa nani kakuambia uje? Inamaana sitakiwi kukuambia kitu nikikuambia
unakuja…si unajua mahusiano yetu ni siri? Ukifanya hivyo tena watatugundua
mapema sana
Jeremy:
samahani sitafanya tena lakini Miriam unajua kabisa jinsi ninavyokupenda yaani
nimeamka nataka kujiandaa niende ofisini kila kitu kinagoma…nimekuona hivi sasa
mambo yataenda
Miriam:
Jeremy…
Jeremy:
nivumilie...Nafanya hivi kwasababu nakupenda sana Miriam si unajua kuwa
nakupenda sana
Miriam:
nami nakupenda Sana, tunachotakiwa kufanya ni kuwa makini ikijulikana itakuwa
kesi kubwa sana
Jeremy
:( anambusu tena shavuni) usijali
nitakuwa makini baby
Ariana
:( anafungua mlango ghafla)
(Wanashtuka)
Ariana:
vipi? mbona mmeshtuka? oh Jeremy…vipi umekuja nyumbani mapema hivi? una shida
gani?
Jeremy
:( anashikwa kigugumizi) nimekuja
kuwasalimia
Ariana:
saa moja?
Jeremy
:( anajichekesha) yeah saa moja
nilikuwa naenda ofisini
Ariana:
hujavaa kiofisi
Jeremy:
ah sometimes huwa naenda hivi
Ariana:
okay… (Kwa Miriam) dogo vipi?
Miriam:
poa shikamoo dada
Ariana:
marahaba (huku anaondoka) anyways
natoka ma mdogo ameniambia unaumwa ndo nikaona nije nikuone pole (anaondoka)
Miriam
:( kwa Jeremy) kwani hujamwambia dada
kuwa humtaki tena?
Jeremy:
Nilimwambia ILA hakukubali ingawa aliniambia kuwa atawaambia wazazi wenu ila
nilimuona kabisa hajalipokea vizuri
Miriam:
sasa itakuwaje? Mimi sina mamlaka kuwa na wewe kama hujaachana na Ariana
Jeremy:
Miriam, nitakuja na wazazi wangu tuombe radhi tutauvunja uchumba kati yangu na
yeye…nakupenda na nitakuoa wewe…hata wazazi wangu wanajua kuwa nakupenda wewe
Miriam:
dah…najua itakuwa vigumu sana kwa wazazi kukubali penzi letu
Jeremy:
watakubali kuwa na mani mke wangu… (Anaibusu
mikono na Miriam)
Miriam:
sawa Nina Imani kuwa kila kitu kitakuwa sawa
Jeremy:
ofcourse baby… (Anambusu kwenye paji la
uso)
(Wanakumbatiana
huku kila mmoja wao anaonekana amezama kwenye dimbwi la mahaba mazito)
Mary: (bado anawachungulia kwa mbali) Mungu wangu hawa watoto
1 Comments
🔥🔥🔥
ReplyDelete