SCENE 19: -
(Jioni ya siku Kama tatu zimepita
mara baada ya Miriam kuvunja uhusiano wake na Jeremy, Jeremy anabisha hodi
kwenye malango ya nyumba ya kina Miriam)
Jeremy
:( anabisha hodi)
Miriam
:( anamfungulia anatoa macho kama mjusi
kabanwa na mlango mara baada ya kumuona Jeremy) He!! Wewe nae…mbona
umekuja?
Jeremy:
nakupigia simu hupokei sijakuona tangu siku ile nimekushusha chuoni kila nikija
wewe haupo umeshaondoka simu zangu unakata ulidhani Mimi ningefanyaje?
Miriam:
huo ni utoto Jeremy kwanini umekuja mpaka nyumbani au mmekuja kuongelea mahari
Jeremy
:( anacheka) mahari yako
Miriam:
acha utani wako tumeshazungumza na tayari tumeshavunja uhusiano wetu sasa
unanipigia simu ya nini?
Ken
:( anakuja) kuna nini Miriam mbona
umeganda mlangoni mama
Miriam
:( anajaribu kumsukuma Jeremy ili
aondoke)
Jeremy
:( analeta ubishi)
Miriam:
hamna kitu baba
Ken:
nani alikuwa anabisha hodi?
Jeremy
:( anajitokeza) shikamoo baba
Ken:
oh, baba marahaba mwanangu karibu ndani
Jeremy
:( anamuangalia Miriam huku anatabasamu)
Ken:
karibu Sana…
Jeremy:
Asante Sana baba…shikamoo
Ken:
marahaba hujambo? (Kwa Miriam) mama
embu njoo umletee shemeji yako hata kahawa…au juisi
Jeremy
:( anatabasamu)
Miriam
:( anaenda jikoni)
Ken:
enhe…baba karibu mmetususa Sana jamani kwani tuliwakosea wapi sie?
Jeremy:
hapana majukumu mzee wangu
Ken:
wazazi wako hawajambo?
Jeremy:
wote wazima baba sijui nyie hapa
Ken:
ah tupo tu ila Miriam ndo kidogo madonda ya tumbo yamemuibukia…
Jeremy
:( anashtuka) eeh Mungu wangu
Ken:
ila anaendelea vizuri si unaona mpaka anatembea…alikuwa anaumwa Sana
Jeremy:
oh God… (Anajisemea moyoni) ndo maana
labda hakuwa ananipokelea simu yangu na chuoni nilikuwa simuoni kumbe alikuwa
anaumwa jamani mtoto jasiri huyu…
Miriam
:( anarudi akiwa na glasi mbili za juisi)
karibuni (anazitenga kwa heshima)
Jeremy:
samahani chooni ni wapi?
Ken:
Miriam embu muonyeshe shemeji yako chooni
Miriam:
naomba unifuate… (Anamuongoza njia)
Jeremy
:( wanapofika mbali upeo wa macho ya watu,
anambana ukutani) mbona hukuniambia kuwa unaumwa Miriam…badilisha nguo
twende hospitali sasa hivi
Miriam:
kwanza unaniumiza, naomba usogee mbali…lakini pili nimeshapelekwa hospitalini
kwahiyo sihitaji kwenda hospitalini tena…
Jeremy:
sawa tuvunge umeshinda…kwanini hukuniambia kuwa unaumwa?
Miriam:
nikwambie ili iweje? Mimi ni shemeji yako
Jeremy
:( anamkazia macho) inamaana unataka
kuniambia kuwa umesahau wakati tuliokuwa nao pamoja wakati mzuri…beach,
migahawani
Miriam:
yamepita na wala sitaki kukumbuka maana itanipa shida tu mimi…usisahau kuwa
wewe ni mchumba wa dada yangu… (Anaona
mama yake anakuja) mama huyo...Haya shemeji chooni ni humu
Jeremy:(anageuka anaona ni kweli ni mama yao Ariana
na Miriam) okay asante Miriam (kwa mama)
shikamoo mama
Keddy:
marahaba baba hujambo?
Jeremy:
sijambo… (Anaingia chooni)
Miriam
:( anaondoka)
Keddy
:( anapita na kuondoka zake)
Jeremy:
(anafungua mlango wa chooni na kutoka)
Miriam…
Miriam
:( anamgeukia) jamani si uniache…
Jeremy:
my lady usinifanyie hivyo….
Miriam:
jamani fanya tu kuniacha bwana unajua unanitesa Sana bwana ee
Jeremy:
wewe ndo unanitesa Sana bwana, kwani bado unajisikia vibaya Sana? Naomba basi
nikupeleke hospitali
Miriam:
usiniletee matatizo...Bwana naomba uniache tu
(Wanakutana na Mary njiani)
Mary:
vipi nyie mbona mnafatana nyuma kama kumbikumbi?
Miriam:
shemeji ametoka chooni
Mary:
ndo umempeleka kwani yeye amekuwa mtoto anahitaji kusindikizwa?
Miriam:
alikuwa hapajui
Mary
:( Kwa Miriam) huyo ni shemeji yako
sijui unaelewa hilo?
Miriam:
ndio naelewa na sitasahau kuwa ni shemeji yangu
Jeremy
:( anajisemea moyoni) dah huyo maza
ananiharibia kweli na swaga zake za ushemeji hapa mi nahangaika huyu mrembo
anielewe kuwa yeye kwangu ndo wa muhimu huyu maza anazingua dah...
Mary:
nendeni sebuleni walipo wengine sio vizuri kujibanza
Miriam:(anaenda sebuleni)
Jeremy:(anamfuata nyuma)
Mary:(anamshika mkono Jeremy) acha kumletea
matatizo mwenzio sawa ee
Jeremy:
kivipi ma mdogo…
Mary:
najua una mahusiano nae…wewe hujui hiyo itamletea shida…mtoto mwenyewe… (ananyamaza ghafla)
Jeremy:
mtoto mwenyewe nini ma mdogo…
Mary:
anaaminika sana kwa wazazi wake kwahiyo usije ukamharibia mwenzio uaminifu
wazazi wake wakaona kama hana adabu
Jeremy:
nashukuru umejua kuwa nampenda Miriam, ma mdogo ni kweli nampenda sana Miriam
yaani Miriam ndo mwanamke wa maisha yangu
Mary:
wewe mtoto acha kabisa huo ujinga acha kabisa na umuoe huyu uliyemchumbia
mwanzo
Jeremy:
siwezi…nitaoa ninayemtaka…samahani kwa kukujibu vibaya ila nitamuoa ninayemtaka
na huyo ni Miriam (anaondoka na kuelekea
sebuleni)
Mary:(anajisemea moyoni) huyu kijana atamletea
mwanangu shida jamani si amuache? watoto bwana wakiwa wadogo wanasumbua wakiwa
wakubwa ndo usiseme sasa hapo Ken na mkewe wakijua kuwa Miriam anamuibia mume
mtoto wao sijui itakuwaje (anaguna kisha
anaenda kuendelea na kazi zake)
(Huku sebuleni)
Jeremy:
jamani naomba niwaage mi naenda
Ken:
haya baba karibu… (kwa Miriam) we Miriam
mtoe shemeji yako
Miriam:(anatii
kisha anatoka nje yeye pamoja na Jeremy)
Jeremy:my
lady…I love you so much
Miriam:
Jeremy...sijui nikwambieje ila hatuna ruhusa ya kupendana…
Jeremy:
kwani hao ni Mungu? wakikufukuza nitakujengea nyumba nzuri nitakuoa haki ya
Mungu sikudanganyi
Miriam:
hapana familia ni muhimu kuliko hivyo vyote
Jeremy:
jamani Miriam usinifanyie hivyo
Miriam:
nenda tu nyumbani (anarudi zake ndani)
0 Comments