MUNGU MKUU 20

 


SCENE 20: -

(Asubuhi mpya iliyojaa matumaini mapya Kwa viumbe vyote, Jeremy yupo ofisini kwake akiwa anafanya shughuli mbalimbali yeye na wafanyakazi wake, wakati huo anaendelea na kazi zao, simu ya Jeremy inaita kwa kuwa iko mbali nae anaomba msaada wa kuletewa simu hiyo)

Jeremy: embu Anita nipe simu ila angalia nani anapiga?

Anita: my lady

Jeremy: wewe…ikimbize haraka hiyo simu

Anita :( anaiwahisha) boss kwani my lady ni nani?

Jeremy :( anatabasamu huku anaichukua simu kutoka kwa anita) wifi yako...Haya kaendelee na kazi zako

Anita :( anaondoka)

Jeremy :( anapokea simu) my lady nilijua tu kuwa utanipigia mara baada ya kukuta missed calls

Miriam: kwanini ulikuwa unapiga kwa mfululizo?

Jeremy: jamani kwani wewe hujui kwanini nafanya hivyo? Si nakupenda?

Miriam: tufanyeje sasa…maana Mimi nakupenda pia...Tena Sana ila naipenda sana familia yangu nampenda dada yangu na mama na baba yangu wakisikia huu utakuwa usaliti...

Jeremy :( anatoka nje) No baby hakuna mtu anayeweza kulazimisha moyo umpende mtu ambae haumtaki…Mimi nakupenda wewe hata iweje siwezi kumpenda Ariana maana yeye sio chaguo langu

Miriam: kiukweli Mimi sijui cha kufanya Zaidi Jeremy

Jeremy: ufuate moyo wako...Hayo mengine tutakuja kujua mbele ya safari tu jamani Miriam

Miriam: kwakweli sijui nipo dilemma…ma mdogo ananiambia ukweli kuwa kumchukua mchumba wa dada yangu sio vizuri lakini moyo wangu hautaki kusikia kabisa moyo wangu hautaki kuelewa kuwa sio vizuri kumchukua mchumba wa dada yangu

Jeremy: kwasababu sio vibaya kupenda Miriam

Miriam: ila ni vibaya kuisaliti familia yako...

Jeremy: tutawaambia…na kumbuka sio kwamba nilipanga kuwa nikifika kwenye nyumba ya mchumba ambae wazazi wangu wamenitafutia nitampenda mdogo wa mchumba wangu huyo…hapana ilikuja tu bila mimi mwenyewe kujua wala kutambua…wala kutarajia

Miriam :( anashusha pumzi) kwahiyo tufanyeje?

Jeremy: tupendane…ukiwa tayari Kwa ndoa maana Mimi nipo tayari wakati wowote

Miriam :( anaguna)

Jeremy: ukiwa tayari basi tutawaambia wazazi wetu

Miriam: sikutegemea Kama ningekupenda Jeremy…nilifata tu kutaka kutimiza ombi la baba yako la kusema kuwa unaweza kujiua…na pia nilifata ushauri wa Vanessa ningejua hata nisingejaribu kukaa karibu na wewe

Jeremy: Mungu alitupangia tu kuwa pamoja na wala sio wanadamu...Nakupenda Miriam naomba usiogope kunipenda mpenzi wangu

Miriam: okay tupendane mpenzi wangu ila sasa siku Ariana akijua itakuwa msala…

Jeremy: tutajiandaa kwa hilo...Tutakuwa pamoja wakati hili linatokea

Miriam: usinidanganye…nakuomba

Jeremy: hapana…sikudanganyi mpenzi wangu 

Miriam: okay

Jeremy: Asante Kwa kunielewa…by the way uko wapi?

Miriam: bado nipo nyumbani…

Jeremy: Leo huendi chuo?

Miriam: Leo Nina vipindi saa tano mpaka saa Saba

Jeremy: nitakupitia tukale lunch pamoja…

Miriam: okay

Jeremy: lakini natamani nije nikuchukue nikupeleke chuo ila nimebanana kweli nitapata muda mchana

Miriam: usijali baba atanipeleka

Jeremy: au nikununulie gari?

Miriam: hapana ukininunulia gari nitaulizwa Sana nyumbani

Jeremy: nakununulia gari natafuta na dereva mwanamke anakuwa anakupitia kila ukitaka kuzunguka labda sokoni, chuoni, supermarket kwa marafiki na kadhalika

Miriam :( anacheka) hata usijisumbue

Jeremy: please sipendi ukipita njiani Kwa miguu…wanaume watakutamani una umbo na una sura nzuri watakuona

Miriam :( anacheka) umeanza wivu wako sasa    

Jeremy :( anacheka pia) lazima niwe na wivu…wewe mke bwana

Miriam :( anacheka) ngoja nikate simu naona mama anakuja

Jeremy: I love you

Miriam: I love you too… (Anakata simu haraka)

(Upande wa Jeremy anarudi ofisini akiwa ana furaha Zaidi)

Anita :( anamtania) wacha we wifi amekufurahisha nini

Jeremy:(anatabasamu) acha tu mwenzangu(anacheka)embu   kafanye kazi acha umbea

Anita:(anaondoka huku anacheka)

Jeremy:(anabaki anaangalia picha ya Miriam kwenye simu yake, anatabasamu mwenyewe)

Post a Comment

0 Comments