MUNGU MKUU 8

 


SCENE 8: -

(Miriam anafika chuoni anatembea taratibu kuelekea darasani, wakati anaendelea kutembea anasikia honi ya gari nyuma yake haraka anageuka kuangalia ni nani)

Miriam :( anageuka) nani?

Jeremy: Mimi (anasogeza gari karibu na Miriam kisha anashusha kioo)

Miriam: oh…shemeji

Jeremy: Jeremy…

Miriam :( anatabasamu)

Jeremy: za toka siku ile?

Miriam: nzuri tu…

Jeremy: njoo ukae nikusindikizie mpaka darasani

Miriam: nimefika shemeji...

Jeremy: nakuomba sana Miriam

Miriam:(anaingia kwenye gari) haya…umefurahi?

Jeremy:(anatabasamu) nimefurahi sana…

Miriam:(anacheka)

Jeremy:(anaanza kuendesha gari) wewe ni mrembo sana…una umri gani ulisema?

Miriam: miaka 18…

Jeremy: umesoma harakaharaka sana upo chuo na una umri mdogo sana

Miriam: nilianza shule mdogo sana

Jeremy: naomba namba yako kabla ya yote usije ukashuka bila kunipa namba yako (anatoa simu yake aina ya iphone 14 na kumpa Miriam aandike namba yake) naomba namba yako please

Miriam: sasa mimi namba yako ya nini?

Jeremy: naomba… (anaacha kuendesha gari) nakuomba…Miriam

Miriam:(anacheka na kubadilisha mada) dada amekupenda kweli na amesema kuwa utafaa kuwa mumewe

Jeremy:(anamuangalia usoni bila kusema kitu)

Miriam: hivi una umri gani shemeji samahani lakini shem…

Jeremy: bila samahani…nakuzidi miaka 12 kwahiyo nina miaka 30

Miriam: mnalingana na dada

Jeremy:mi nataka kukuoa wewe

Miriam: wewe shem hata usiongee hivyo hata kimasihala

Jeremy: kwanini?

Miriam: wewe ni mchumba wa dada yangu na naomba ubaki hivyo…

Jeremy:(anacheka) nakutania tu Miriam

Miriam: najua unanitania… (anaangalia alipoweka mkono wake anaona gazeti lenye picha ya Jeremy mbele ya gazeti hilo) na mimi mpelelezi…na hii picha inafanya nini kwenye hili gazeti

Jeremy: soma si unajua kusoma?

Miriam: wewe Mohamed Dewji?

Jeremy:(anacheka)

Miriam: upcoming young business icon of the year

Jeremy:(anacheka) yes…

Miriam: wewe ni mfanyabiashara eeh…

Jeremy: nina hotel Dar es Salaam, Mwanza na Arusha…nina supermarket Dodoma na nina filling station kama tatu hapa Dar

Miriam: wow…hongera

Jeremy: asante na zinafanya vizuri…kinachokosekana maishani mwangu ni mwanamke tena simaanishi mwanamke tu…natafuta true love

Miriam:(anacheka) si umempata dada yangu

Jeremy:(anacheka) ninaishi peke yangu na mwisho wa siku nikaona nimwambie baba anitafutie mchumba ila katika hilo nikaona ua lililonipendeza sana na ninataka nilichume

Miriam: kwahiyo kwa lugha nyingine hutaki tena kumuoa dada yangu?

Jeremy: kwa bahati mbaya…ndio…

Miriam: kwanini…ulikuja nyumbani…

Jeremy: hapo ilikuwa kabla ya kuona ua langu

Miriam: yaani wanaume

Jeremy: hapana usituchukulie hivyo...

Miriam: sasa unadhani dada yangu atajisikiaje akijua kuwa wewe humtaki na yeye anakupenda sana...tangu mmeondoka amekuwa akiongea sana kuhusu wewe yaani anakupenda sana shemeji kwanini unafanya hivyo…?

Jeremy: iam sorry…okay tumeongea sana na ninajua kuwa unahitaji kwenda darasani…naomba namba yako

Miriam: ya nini huku unasema una ua lako? kama ni hivyo naomba uwaambie wazazi wangu kuwa hutamuoa dada yangu ili waache kupanga hii harusi…

Jeremy: nitafanya hivyo…

Miriam:(anajikuta anamuonea huruma dada yake) shemeji jamani usifanye hivyo tutachekwa maana mlipokuja tu wazazi wetu wakaanza kuwaambia watu ya kwamba dada Ariana anatarajia kufunga ndoa

Jeremy: but I don’t love her na ndoa yetu haitakuwa na Amani maana hakuna upendo baina yetu

Miriam: utampenda tu…

Jeremy: hamna…embu naomba simu yako

Miriam:(anatoa simu aina ya iphone 6 PLUS) ya nini?

Jeremy:(anaichukua na kuweka namba yake)

Miriam: simu yangu haina salio

Jeremy: itakuja tu

Miriam:(anatabasamu)

Jeremy:(anajaribu kujipigia na haraka namba ya Miriam inaingia kwenye simu yake) asante Miriam

Miriam: sawa…

Jeremy:(anatoa pesa kama elfu hamsini) chukua hii utanunua vocha

Miriam: mbona nyingi?

Jeremy: ya kawaida bwana…najua una mahitaji mengi kama vocha na sio kila kitu utamwambia baba na mama…

Miriam: asante lakini…ubarikiwe

Jeremy: usijali…

Miriam:mi naenda sasa

Jeremy: naomba nikupigie simu baada ya masomo tuonane

Miriam:(anaguna) sidhani kama nitaweza

Jeremy: usijali…tunaenda kunywa tu soda halafu nakurudisha nyumbani

Miriam: baba huwa anakuja kunichukua na kunileta chuoni

Jeremy: ah…hiyo ni mbaya…kwahiyo tufanyaje?

Miriam: hata sijui…

Jeremy: okay nenda nitajua cha kufanya siwezi kukosa cha kufanya ili nionane na wewe

Miriam: lakini kwanini unataka kuniona?

Jeremy: basi tu…

Miriam:(anashuka kwenye gari na kwenda darasani)

Jeremy: I love you Miriam nakupenda sana…nimepata mtu wa kukaa nae my life partner…I love you najua itakuwa ngumu sana kwetu ila tutapata tu njia my love… (anawasha gari na kuondoka zake)

Post a Comment

1 Comments

  1. Miriam na ariana into conflict😅🙌

    ReplyDelete