MUNGU MKUU 46


 

SCENE 46: -

KWENYE JUMBA BOVU LA KINA ARIANA: -

(Majira ya saa moja usiku giza totoro limetanda juu ya nchi, Ariana amesimama kwenye jumba ambalo aliwahi kumtekea Miriam, anaonekana kuna kitu au mtu anamsubiri kwa hamu. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye mtu yule anafika)

Mtu: boss nimefika

Ariana: nakuona (anatabasamu) Colton za kwako? Asante kwa kunisaidia kwenye hili

Colton: usijali

Ariana: tumefanya mambo mengi sana kuhakikisha Miriam anahukumiwa kufa…

Colton: sawa sawa boss

Ariana: unajua nimetembea na hakimu ili atoe hukumu nayotaka mimi

Colton: Duh wewe noma sana…uko vizuri lakini huoni ni dhambi unajichumia

Ariana: (kwa kejeli) wanasema Mungu ni wa huruma husamehe dhambi

Colton: acha kumkejeli Mungu

Ariana: hata mimi atanisamehe tu…ila nimekukubali sana umeiba nguo za Miriam kwa maumivu makubwa ukatoa damu yako na kuzipaka baada ya kufanya hivyo ukazirudisha ili uwe ushahidi aisee nimekupenda bure

Colton: nilikuwa nafata maagizo yako

Ariana: safi sana wewe kweli ni rafiki mwema yaani umesimama na mimi kwenye shida na raha…

Colton: nimefanya ulichotaka ingawa mara ya kwanza sikuona kama itakuja kunitesa hivi…mtoto wa watu atanyongwa kwa kosa ambalo sio lake na wala mimi sijafa

Ariana: (anacheka kidogo) huyo mtoto unayesema sijui unamuona huruma ni mtoto aliyenitesa mimi kwa asilimia mia…amechukua kila nilichokuwa nacho…namchukia sana

Colton: ungemuadhibu kivingine

Ariana: usinifundishe (anafyonza) huyu Malaya amenitesa mimi hata huyo Mungu wenu anajua

Colton: acha kumkejeli Mungu Ariana

Ariana: aende zake

Colton: Mungu hakejeliwi

Ariana: aende zake huko

Colton: (anatikisa kichwa) Mungu wangu hakejeliwi nimefanya kosa kubwa sana kuungana na wewe kumpoteza Miriam sasa yupo jela anasubiri hukumu

Ariana: na atanyongwa… (anacheka) maana kila kitu nimekipika na kikaiva kinasubiri kiipuliwe kiliwe (anacheka) Miriam akishakufa Jeremy atakuwa wangu na familia yangu itakuwa yangu peke yangu

Colton: sawa hongera…naomba uniache niende nikapate chakula kisha nipumzike…sijisikii vizuri

Ariana: hauendi popote baba

Colton: ukimaanisha?

Ariana: kwamba kitu pekee ambacho sijafanya ni ushahidi wa mwili wako…

Colton: unataka kufanyaje Ariana...?

Ariana: kukuua

Colton: (anatoa macho kama mjusi kabanwa na mlango)

Ariana: (anatoa bastola kutoka kwenye mkoba wake)

Colton: Ariana naomba usiniue tafadhali maana nimefanya kila ulichoniambia tena kwa uaminifu mkubwa sana

Ariana: najua hata mimi naona vibaya sana kukua ila unadhani nitafanyaje? Nataka Miriam afe sasa hatakufa kama wewe upo hai mtakutana ahela

Colton: Ariana please…

Ariana: iam so sorry my dear friend (anafyatua risasi moja)

Colton: (inamfikia kifuani Analia kwa uchungu kisha anaanguka chini)

Ariana: (anaweka bastola kwenye mkoba kisha kwa kiwewe anakimbia)

BAADA YA DAKIKA TAKRIBANI THELATHINI

Colton: (ananyanyua mkono kwa maumivu makubwa sana) aah nina bahati sana (anachukua simu na kumpigia mtu Fulani)

(Simu inaita)

Sauti: enhe...nambie

Colton: kama uliota ni kweli amejaribu kuniua…nakushukuru sana kwa kuniandaa

Sauti: usijali...toka hapo sasa…kwani yeye yuko wapi?

Colton: ameondoka nahisi… ila nina maumivu

Sauti: ni uoga tu sidhani kama imefika popote…nimekuvalisha hii bullet proof

Colton: ulijuaje atanipiaga maeneo ya kifuani?

Sauti: hata mimi nashangaa…nilijuaje…anyways toka hapo njoo moja kwa moja tulipopanga, pole lakini kwa maswaibu uliyopata

Colton: sawa, usijali

(wanakata simu)

Colton: (kwa kuugulia ananyanyuka na kuondoka mahali hapo)

Post a Comment

0 Comments