SCENE
45: -
RUMANDE
ALIPO MIRIAM: -
(Jioni
ya siku nyingine, Miriam yupo rumande pamoja na wafungwa wengine. Upole na
unyenyekevu wake unampa marafiki wapya sehemu hiyo, pamoja na kuwa na marafiki
wapya bado moyo wake unaumia sana kwa hali anayopitia)
Miriam: (Analia
sana)
Rafiki:
usilie umeshalia sana jamani kwanini usiache kulia?
Miriam:
naogopa…naogopa matokeo ya haya yote
Rafiki:
umeniambia kuwa hukuua Mungu anakujua na atakupigania
Miriam:
sijui rafiki yangu
Rafiki:
usilie yaani tangu umekuja wewe ni kulia tu
Miriam:
(anafuta machozi)
Rafiki:
embu tuachane na hayo…yule kaka mrefu aliyekuja kukuona na anakuja sana ee ni
nani yako?
Miriam:
(anatabasamu kidogo) ni mpenzi wangu actually ni mchumba wangu yeye ndo
chanzo cha haya yote…ndo maana nafikiria kuachana nae
Rafiki:
jamani kwanini? kaka wa watu alivyo
mzuri jamani mashallah
Miriam:
kwanza najua nitakufa tu hapa hukumu ikitoka nitakufa ni bora nimuachishe
tumaini la kuoana na mimi
Rafiki:
sio vizuri
Afande:
(anakuja walipo kina Miriam) Miriam njoo kuna mgeni wako
Rafiki:
amekuja tena…yaani anajitahidi kuja
Miriam:
(anaamka na kumfuata afande baada ya hatua chache anafika alipo Jeremy)
Jeremy
Jeremy:
baby
(Wanakaa)
Jeremy:
unaendeleaje?
Miriam:
salama shikamoo
Jeremy:
marahaba
Miriam:
bora umekuja nina jambo nataka kukuambia
Jeremy:
una mimba yangu? Baby najua utakuwa na mimba yangu nafanya juu chini utoke ili
tufunge ndoa tumlee mtoto wetu
Miriam:
sina mimba…
Jeremy:
lakini nilikuwa nina uhakika baada ya siku ile
Miriam:
mimi ndo najua by the way najutia kile kitendo
Jeremy:
kwanini?
Miriam:
tulizini
Jeremy:
ila si tuna mpango wa kuoana?
Miriam:
huo mpango umeisha
Jeremy:
hata sikuelewi Miriam
Miriam:
mimi na wewe basi
Jeremy:
you can’t be serious Miriam…
Miriam:
kwa bahati mbaya nipo very serious
Jeremy:
nimekukosea nini Miriam
Miriam:
nadhani ndoa yako na Ariana inabidi iwe
Jeremy:
simpendi Ariana and you know it
Miriam:
jilazimishe
Jeremy:
Miriam umesahau mapenzi yetu, ahadi zetu hata mipango yetu mpenzi wangu embu
niambie nakosea wapi nitajirekebisha ila tafadhali naomba usiniache
Miriam:
mimi ni mfu nasubiri tu siku ya hukumu na baada ya hapo sitakuwepo tena Jeremy
Jeremy:
we are doing our very best mimi na mwanasheria wako tunafanya kila kitu
Miriam:
(machozi yanamlenga) nielewe Jeremy bora uumie uzoee kuliko kuniona
nimekufa utaumia sana
Jeremy:
usiniache tafadhali Miriam wangu nipo chini ya miguu yako ni wewe pekee
ninayekupenda kwa dhati kabisa naomba usiniache Miriam
Miriam: (Analia)
ila nitakuacha hivi karibuni Jeremy
Jeremy:
Mungu wetu hatoruhusu nakuomba sana nipe nafasi mpenzi please (anamshika
mkono)
Miriam:
(Analia) Jeremy naomba uende nyumbani na usirudi tena
Jeremy:
Miriam that is not fair…
Miriam:
iam so sorry (ananyanyuka)
Jeremy:
Miriam…
Miriam:
(anaondoka)
Jeremy:
Miriam…Miriam usinifanyie hivyo tafadhali
Miriam:
(anaingia rumande)
Jeremy:
(anabaki anasikitika sana)

0 Comments