SCENE 50: -
MAHAKAMANI:
-
SIKU
YA HUKUMU: -
(Watu wamekusanyika pamoja kwa
ajili ya kusikiliza hatma ya kesi inayomkabili Miriam)
Hakimu:
(anaingia)
Watu: (wanasimama ishara ya heshima)
Hakimu:
(anaketi)
Watu: (wanaketi)
Miriam:
(ameshafika na anaonekana ana wasiwasi
sana)
Mwansheria:
unatetemeka sana…hiyo sio nzuri kwa ujauzito wako
Miriam: (machozi yanamlenga) nini faida ya kuwa
na ujauzito huku leo hukumu inatoka kuwa nimeua na nitanyongwa mpaka kufa?
Mwanasheria:
tulia Miriam tafadhali niamini mimi basi kama sio mimi muamini Mungu basi
Miriam:
(anaangalia nyuma anawaona ndugu zake,
baba yake, mama yake, mama yake mlezi pamoja na baba yake mlezi, rafiki yake
kipenzi, mchumba wake, bibi na babu wake pamoja na mama yake mkubwa na Zaidi
dada yake wa kufikia) imagine hawa wote baada ya leo sitawaona tena… (machozi yanamtoka)
Mwansheria:
tulia Miriam nakuomba...
Mwendesha
mashtaka: leo ndo ile siku ambayo tumekutana hapa kusikiliza hukumu baada ya
kukusanya ushahidi kutoka pande zote (anamuinamia
hakimu) kwa heshima naomba mheshimiwa uendelee
Hakimu:
(anaangalia karatasi yake) mahakama
hii imekuta
Ariana:
(anatabasamu) ni wakati sasa Miriam
umekwisha…yuko wapi huyo Mungu wako mbona hatumuoni?
Hakimu:
mahakama imekuta
Miriam: (amejiinamia Analia sana)
Jeremy:
(anatetemeka)
Vanessa:
eeh Mungu huu ni wakati sasa Mungu simama mwenyewe rafiki yangu hajaua
Miriam:
nimekwi…
Sauti: (kutoka nyuma) subiri
(Watu wanageuka)
Mtu: (anakuja kwa kasi kubwa sana)
Watu: (minong’ono)
(La haula!!! Mtu mwenyewe sio
mwingine ni Colton yule yule iliyosemekana ameuliwa na Miriam)
Ariana:
(kwa mshangao) Colton???
Miriam:
Colton…?
Jeremy:
(anatabasamu) thank you man!!!
Mwansheria
2: (anatoa macho) mzimu…
Vincent:
(anatabasamu)
Miriam:
(kwa mwanasheria) muujiza…
Mwanasheria:
kuna mambo mengi sana utasikia kaa kwa utulivu
Miriam:
MUNGU MKUU… (Analia kwa furaha) iam
safe now
Colton:
(anaendea kizimba)
Mwendesha
mashtaka: umefufuka?
Hakimu:
umetokea wapi?
Colton:
sikufa na wala sikuzikwa… (kwa Miriam)
Miriam mdogo wangu kipenzi nisamehe
Miriam:
(anashangaa)
Ariana:
(anatoa macho)
Miriam:
mimi mdogo wako?
Colton:
ndio Miriam mimi ni mtoto wa bwana Vincent nilizaliwa mimi ndo ukazaliwa wewe…
Miriam: (anashangaa)
Colton:
kwa bahati mbaya nilijua hivi karibuni kweli hii dunia ndogo sana…baba yangu na
mama yako walikuwa mahawara baba yangu alikuwa ni mume wa mtu…wakati wapo
kwenye mahusiano mama yako alibeba mimba ambayo matunda yake ni wewe Miriam
Miriam: (anashangaa)
Colton:
sikujua mpaka baada ya kukufanyia unyama mdogo wangu (Analia) nisamehe mdogo wangu ni ujinga tu…ni mapenzi tu na ujana
ndo ulikuwa unanisumbua mpaka nikakubali huo ujinga
Ken: (anashangaa) Colton kaka yake Miriam kivipi?
Mwansheria
1: embu tusimulie maana hata hatuelewi naamini hakuna anayeelewa wewe ni kaka
wa Miriam kivipi ulijua lini saa ngapi…ulijua kabla au baada ya kujua kuwa una
mdogo anayeitwa Miriam?
Colton:
ilikuwa baada ya kufanya haya
Mwanasheria
1: mlifanyaje mpaka polisi wakaamini kuwa umekufa?
Colton:
tulipanga vizuri kabisa na Ariana
Keddy: (anashangaa) Ariana???
Colton: Ariana
hakuwahi kumpenda Miriam tangu siku ya kwanza anamuona...aliniambia kuwa Miriam
alimuibia kila kitu tangu siku ya kwanza amefika…Miriam ni mtoto wa kufikia wa
wazazi wa Ariana…mara ya kwanza hakujua maana wazazi wale walimpenda kama mtoto
waliyemzaa…hicho hakikumpendeza Ariana hata kidogo…wivu ukajenga chuki na kila
siku ulizidi wakati Miriam akiwa bado mdogo sana alimchukua na kwenda kumficha
porini ili wanyama wakali wamtafune ila Mungu alikuwa upande wa Miriam
alipatikana
Watu: (wanashangaa)
Colton:
walipokuwa wakubwa Miriam akiwa na umri wa miaka 18 mchumba alikuja nyumbani
kwa lengo la kumchumbia Ariana ila kwa bahati sijui mbaya sijui nzuri mchumba
akampenda Miriam kama mnavyojua penzi kikohozi mchumba akamwambia ukweli Miriam
juu ya hisia zake kwa moyo mzito Miriam alikubali wakaanza mahusiano na bwana
yule
(Watu wanasikiliza kwa makini)
Colton:
mahusiano yale yalijulikana kwa Ariana alichukia sana akamteka Miriam na
kumtesa sana
Ken: (anashangaa) kumbe adui alikuwa ndani
kwangu
Colton: Miriam
alipatikana kwa msaada wa mpenzi wake ambae sasa ni mchumba na baba wa mtoto
wake aliye tumboni kwake…Ariana hakuridhika akanituma niende nyumbani nijifanye
ni mchumba wake lakini pia hawara wa Miriam…nilikubali
Keddy: (anashangaa) kumbe mipango yote alikuwa
anayafanya Ariana?
Colton:
nikajifanya bwana wake nikamuharibia Miriam kwa wakwe zake yaani wazazi wa
mchumba wake…hilo lilipita alipoona ameshindwa kabisa Ariana aliijifanya
amepatana na Miriam akiwa na mpango mwingine kichwani mwake
Watu:
Mungu wangu
Colton:
mpango wa mimi kujifanya nimeuliwa na Miriam ni kweli ile damu ni rangi tu…nguo
zake tulikuja kuziiba na nikazipaka damu yangu…nikisaidiwa na baadhi ya
maaskari
Askari
1: (anaangalia chini)
Colton:
baada ya tukio la kuiba nguo nilichoka nikaona nirudi nyumbani kwa baba yangu
maana nilikuwa nimekimbia nyumbani kwa sababu ya ujinga wangu…(Analia)
Watu: (wanasikitika)
Miriam:
(Analia)
Jeremy:
MUNGU MKUU sana acha niziimbe sifa zake God did it my love…
Ariana:
(amekaa kimya huku anaangalia chini kwa
aibu)
Miriam: (anamgeukia Jeremy)
Jeremy:
Jesus did it my love
Mwanasheria
1: tuambie ulijuaje kuwa Miriam ni dada yako na ulifanyaje baada ya hapo…
Colton:
okay nitasimulia kisa kizima naombeni muda kidogo
FLASHBACK
0 Comments