MUNGU MKUU 56


 

SCENE 56: -

BAADA YA MIEZI MITATU: -

HARUSI YA MARY NA VINCENT: -

(Miriam anamuandaa mama yake kwa ajili ya ndoa itakayofanyika muda mchache baadae)

Mary: oh, Mungu wangu

Miriam: umependeza sana…(anatabasamu) mama yangu wewe ni mrembo sana

Mary: (amependeza sana) jamani Miriam (anatabasamu)

Miriam: mama

Mary: mmmh…

Miriam: una furaha?

Mary: sana mwanangu kuna mtu ambae aliota kuolewa na mwanaume Fulani nae akamuoa akaacha kufurahi kweli?

Miriam: ulikuwa unaota kuolewa na baba?

Mary; (anakaa kimya kidogo) Vincent ni mwanaume wa ujana wangu…alikuwa ni mume wa mtu wakati tunakupata wewe, aliniacha na kwenda kwa familia yake na mimi nyumbani nikafukuzwa sikuwa na msaada mwingine Zaidi ya kukuweka mlango kwa baba na mama Ariana…nina furaha wazazi wale walikulea kwa upendo na kukupa kila kitu ulichohitaji…(anatabasamu) nimekaa miaka 20 bila kumuangukia mwanaume yeyote maana nilikuwa nampenda sana Vincent –ila sio kwamba sikuwa na mahusiano ila tu muda wote huo nilkuwa nampenda sana Vincent

Miriam; oh mama

Mary: sikuwahi kujua kama Mungu atafanya muujiza wa kunileta karibu na Vincent na baada ya masaa machache naingia kanisani kwenda kuungana na mwanamume niliyempenda maisha yangu yote

Miriam: utapenda kuzaa?

Mary: hapana Miriam nimeshazeeka sana

Miriam: miaka 37?

Mary: ndio

Miriam: mama watu wanazaa mpaka miaka 41 mpaka miaka 45 mama—usiwe mchoyo mama mi nataka mdogo wangu

Mary: (anamshika bega mwanae) haya hayo tumuachie Mungu

Mama Mary: (anakuja) nyie bado mnapiga stori muda umeisha

Mary: mama

Miriam: bibi hujaenda tu kanisani

(simu ya Miriam inaita)

Miriam: baba Glory anapiga…ataanza kunigombeza

Mama Mary: wanaume ndivyo walivyo shoga yangu…

Miriam: (anapokea) shikamoo baba glory

Jeremy: marahaba mama Glory !!!mpo wapi jamani?

Miriam: tunakuja…tupo saluni bado kwani mmeshaanza?

Jeremy: hapana tutaanzaje huku bibi harusi hajafika?

Miriam: ngoja nimnyonyeshe Glorify nakuja

Jeremy: msichelewe mama Glory…

Miriam: hatuchelewi

(wanakata smu)

Mama Mary: ulikuwa unaogopa bure mbona hajakugombeza

Miriam: sipendi kumuudhi maana akichukia muziki wake sio wa kitoto

Mary: naelewa mama

Miriam: nampenda baba Glory

Mama Mary: hata yeye anakupenda sana…yaani napenda mnavyoheshimiana na hicho ndo kitawawaongoza na kutunza mahusiano yenu

Mary: kweli kabisa

Miriam: jamani tusiongee sana…twendeni

(wanatoka wanapanda gari lililopambwa vizuri)

Mary: (ameshika ua kubwa)

Miriam: (anamchukua mwanae na kumnyonyesha) hivi Vanessa yuko wapi?

Mama Mary: katangulia kanisani

Miriam: oh

(Safari ya kwenda kanisani)

Mary: (anashusha pumzi)

Miriam: usiwaze mama utakuwa sawa

Mary: najua kila kitu kitaenda vizuri

Miriam: (anacheka)

(Baada ya mwendo wa muda mrefu kidogo wanafika kanisani)

Mary: kuna watu wengi sana

Miriam: unaishi na watu vizuri sana…karibu mama twende ukaungane na mpenzi wa moyo wako

Mary: ndio mwanangu

(wanashuka)

Miriam: (anatangulia kama kusafisha njia kabla ya bibi harusi kuingia)

Keddy: (anatabasamu anapomuona Miriam)

Jeremy: (anampokea na pamoja wanaelekea altareni)

Vincent: (anasubiri kwa hamu kubwa) sikutarajia kama Mary atakuwa mke wangu maisha bwana…ni fumbo zito sana

Colton: (anatabasamu wakati anamsubiri Vanessa)

Vanessa: (anakuja)

Colton: (anampokea mpenzi wake)

Mary: (amesimama tayari kabisa kwa ajili ya kuingia kanisani)

(Wapiga picha wako tayari kabisa kumpiga picha bibi harusi)

Mary: (anapiga hatua huku anatabasamu)

(watu wamesimama kumkaribisha kwa shangwe nyingi)

Miriam: oh (kwa Jeremy) mama yangu amependeza sana jamani

Jeremy: ni mrembo kama wewe

Miriam: oh, honey asante kwa kunipamba

Jeremy: usijali (anamuangalia usoni kisha anatabasamu)

Mary: (anafika altareni anashikwa mkono na Vincent kisha kwa pamoja wanamuangalia mchungaji)

Keddy: hongera sana Mary…hatimaye na wewe umepata wa kwako…wa maisha

Mary: (anatokwa machozi ya furaha)

Vincent: (anatabasamu)

Miriam: wazazi wangu

Jeremy: najua

Mchungaji: (anaanza ibada kwa kukaribishwa waumini kisha anafanya mahubiri kidogo) sasa tunaingia ibada ya ndoa takatifu

Mary: (anamshika mkono mume wake mtarajiwa)

Mchungaji: (anaanza ibada na mwisho anawatangaza kuwa mume na mke) sasa mmekuwa mwili mmoja sasa ni mke na mume

(watu wanawapongeza kwa hatua hiyo kubwa)

Post a Comment

0 Comments