SCENE
57: -
BAADA
YA WIKI MOJA: -
HOSPITALI
YA WENYE CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI: -
(Miriam
na Vanessa wanafika katika hospitali ya vichaa kwa lengo la kumuona Ariana
aliyekuwepo hapo kwa mwaka mzima)
Miriam:
(kwa nesi wa zamu) habari dada?
Nesi:
safi karibu
Miriam:
asante
Nesi:
enhe…
Miriam:
nimekuja kumuona dada yangu
Nesi:
anaitwa nani?
Miriam: Ariana
Kennedy
Nesi:
sawa nifuateni…
(wanamfuata)
Nesi: (anawaongoza
njia mpaka katika bustani nzuri iliyopo nje kidogo ya wodi hizo) yule pale
anapenda kukaa peke yake hapendi kuongea na mtu yeyote…karibuni
Miriam:
asante (kwa Vanessa) twende wifi
Vanessa:
twende
(wanamfuata
mpaka alipo)
Miriam: (kwa
sauti ya utulivu) dada?
Ariana:
(anageuka anawaangalia kwa huruma huku afya yake inaonekana kuzorota sana na
amekonda sana)
Miriam:
dada yangu
Ariana:
(kimya)
Miriam:
shikamoo dada
Ariana:
(anaitikia kwa kichwa)
Vanessa:
shikamoo dada
Ariana:
(anaitikia kwa kichwa)
Miriam:
tumekuja kukuona
Ariana: (kimya)
Miriam:
baada ya miezi miwili Colton na Vanessa watafunga ndoa…
Ariana: (kimya)
Miriam:
mama na baba yangu tayari wameshafunga ndoa wameenda Sweden kwa ajili ya
fungate
Ariana: (kimya)
Miriam:
dada bado umenikasirikia?
Ariana:
(kwa huzuni huku machozi yanamtoka) hapana nimejikasirikia mwenyewe
Miriam: (kwa
huzuni kidogo) dada
Ariana: MUNGU
MKUU na ukuu wake nilikuwa ninauona kwako kwa kila tukio baya
nililokuwa nakufanyia
Miriam:
(anasikitika) lakini bado sikukubali ona alivyoniadhibu
Vanessa:
(anashangaa) kwani wewe ni mzima sio kichaa?
Ariana:
(machozi yanamtoka) hapana mimi sio kichaa wala nini naogopa kwenda jela
(Analia sana)
Vanessa:
dada Ariana
Ariana:
mimi ni mtu mbaya ona watu wote wazuri sasa hivi mna maisha mazuri mimi naishi
kwa uoga sijui kwanini…nilimdhihaki Mungu wangu nikakataa kuuona ukuu wake ona
ninavyohangaika mimi jamani
Miriam:
hapana dada usiseme hivyo na pia huendi jela dada Ariana
Ariana:
(anafuta machozi) kivipi?
Miriam:
umekuja utetezi unaosema kuwa ukifanya kila kitu ukiwa una tatizo…la (anashusha
sauti kidogo) la kiakili hivyo watakusamehe na mimi nimefuta
Ariana:
(kimya kidogo) ndo maana Mungu alikuwa anakupigania una roho nzuri sana
nilikutesa sana Miriam
Miriam:
najua ila yamepita natamani umjue Mungu na ukuu wake
Ariana:
(anatabasamu) nilikataa kukukubali kama mdogo wangu na tatizo langu
lilianzia hapo
Miriam:
usijali dada hayo yameisha…kesho majira kama haya utakuwa unarudi nyumbani kuna
mambo mawili matatu utafata kama utaratibu na baada ya hapo kila kitu kitaisha
Vanessa: natumaini umejifunza
Ariana:
ndio…mdogo wangu Vanessa nimejifunza kuwa Mungu ni mkuu na ni yeye ndo mwenye
mamlaka ya dunia hii…nilifanya kosa kubwa sana kumkejeli
Miriam:
umekiri kosa na umejitahidi kumkaribisha maishani mwako yeye ni mwenye huruma
atakaribia maishani mwako
Ariana:
enhe nambie mabadiliko yoyote huko?
Miriam:
Colton na Vanessa watafunga ndoa
Ariana:
habari njema sana hiyo na mimi ningetulia na mimi ningekuwa kwenye mstari wa
kuolewa ila kwasababu ya roho yangu mbaya na mipango mingi isiyo kuwa na faida
nipo hapa sina mbele wala nyuma
Miriam:
Mungu wetu ni Mkuu na njia zake hazichunguziki hata kwa macho gani usijali
Mungu amekuwekea wa kwako wewe mkaribie kaa nae na mkumbushane nae atakupatia
kila hitaji la moyo wako
Ariana:
amina mdogo wangu naamini itakuwa hivyo…kwa mara nyingine Miriam nisamehe
Miriam:
nimeshakusamehe wewe ni dada yangu na ninakupenda sana
Ariana:
pamoja na kwamba nilikutesa Miriam?
Miriam:
hata hivyo still wewe ni shoga yangu (anatabasamu)
Ariana:
oh Miriam… (anamkumbatia)
Miriam:
(anamkumbatia pia)
Vanessa:
(anatabasamu)
Ariana:
njoo wifi yetu
Vanessa:
(anaungana nao)
Ariana:
asanteni kwa kuja yaani imenipa Amani nilikuwa sina Amani nilikuwa nalia tu
Miriam:
ulikuwa umekata tamaa?
Ariana:
kabisa
Miriam:
hairuhusiwi kukata tamaa hata iweje…wanasema hata kama usiku ni mzito vipi ni
lazima pakuche maana yake hata iweje kwamba unapitia shida nyingi Mungu anakupa
tumaini ya kwamba patapambazuka na hayo matatizo yataisha tu dada yangu ni
mwaka umekuwa kwenye matatizo sasa pamepambazuka na yote hiyo sifa na utukufu
mrudishie yeye sifa na utukufu kwa UKUU wake na kwamba amefanya makuu
Vanessa:
Miriam alikuwa dada yao Mussa na Haruni na unajua sifa ya Miriam?
Ariana:
mimi sijui
Miriam:
hata mimi…
Vanessa:
Miriam alikuwa ni mwana sifa…nakuona na wewe unavyompa Mungu sifa zake
Miriam:
ni kwasababu nimeuona mkono wake na matendo yanayodhihirisha kuwa yeye ni
MKUU…oh Namapenda Mungu wangu sijui nimrudishie nini kwa mambo makuu
aliyonitendea
Vanessa:
kwakweli hata utoe nini hautaweza kumrudishia Mungu…hatuna budi kuendelea
kusema UKUU wake kwa vizazi na vizazi
Ariana:
hakika…(anatabasamu) na mimi nitakuwepo kwenye harusi ya Colton na Vanessa
Miriam:
bila shaka kabisa
Vanessa:
kwa uwezo wa Mungu wetu nitaka kuona watu wakifurahi sana siku ya harusi yangu
Miriam:
na itakuwa hivyo dear wifi
(wanacheka)
Ariana:
(anatabasamu na anaonekana ana tumaini jipya)

0 Comments