SCENE 59: -
BAADA YA MIEZI MIWILI
SIKU YA HARUSI YA
MIRIAM NA JEREMY: -
(Asubuhi
ya siku muhimu sana ambayo ilikuwa inasubiriwa na sio miriam na Jeremy tu bali
kwa kila mtu aliyekuwa anawafahamu wawili hao. Miriam na rafiki zake wamekaa
katika chumba maalumu wakijiandaa kwa ajili ya kwenda kanisa. Miriam amevaa
gauni malumu la kujiandaa kwa ajili ya vazi maalumu kwa ajili ya harusi)
Miriam:
(anakunywa kinywaji chake)
(kila
kitu kinaonekana ni cha gharama sana ni kwasababu ya uwezo mkubwa wa kifedha alionao
Jeremy yaani mume mtarajiwa wa Miriam na baba yake mzazi Miriam)
Miriam:
oh, Mungu wangu asante kwa kunionyesha UKUU wako kila wakati katika maisha
yangu…kila mara ulitembea na mimi asante sana Mungu wangu
Mtoto
wa kiume: (kati ya umri wa miaka 5 mpaka 7 anakuja) hodi
Dada1:
oh, karibu nini tena?
Mtoto:
(anampa mfuko mdogo) nimeambiwa nimpe mama G
Miriam:
nipo hapa nani amekupa (ananyanyuka na kumfuata)
Mtoto:
nimepewa na baba G
Miriam:
oh, asante sana (anauchukua anafungua ndani) kuna nini?
Ariana:
fungua sasa...
Vanessa:
fungua tuone
Miriam:
tulieni sasa
Mary:
angalieni tusichelewe kanisani
Miriam:
(anafungua anakutana na mkufu wa dhahabu wa thamani na saa ya gharama sana)
oh My God
Ariana:
wow
Mary:
wacha we
Miriam:
(anaangalia ndani) kuna karatasi kama barua ya mapenzi sijui (anacheka)
(wanacheka)
Mary:
hiyo soma mwenyewe
Vanessa:
naomba nikiri wifi kuwa natamani uisome kwa nguvu lakini acha niseme tu mama
yupo sawa kabisa kwamba ni lazima usome peke yako
Miriam:
okay ngoja nisome basi (anaifungua) oh Jeremy (ananza kuisoma)
mama G, kipenzi changu, jina la bwana lihimidiwe na acha Mungu aitwe Mungu na
nitamtukuza Mungu siku zangu zote za maisha yangu kwa sababu ya UKUU
wake…nilipokuona kwa mara ya kwanza miaka kama miwili iliyopita nafsi yangu
ilikiri wazi kuwa ni wewe na wewe pekee ndo chaguo langu…penzi letu lilikuwa
sio lenye kuwezekana ila kwa UKUU wake alitupigania mpaka tukawa wapenzi tena
kwa Baraka za baba na mama na mama mzazi na wazazi wangu lakini shetani
aliingilia kati hatukukata tamaa tulipambana hata magumu yalipotufika ulitaka
kukata tamaa lakini penzi letu lilishinda mpenzi wangu…kwa UKUU wake tulimpata
mtoto wetu…mtoto ambae ni matunda ya penzi letu…asante mpenzi kwa kukubali
kusafiri pamoja na mimi kwenye hii safari tuendelee kumsihi Mungu atembee
na sisi..nakupenda sana Miriam nitakuona
kanisani ambapo tutaunganishwa mpaka kifo kitakapotutenganisha.,nakupenda sana
my love…I cant wait to spend the rest of my life with you baby.
Ariana:
oh Miriam
Miriam:
(anafurahi sana) yaani hamjui baba G ameniambiaje kwenye hii barua
Mary:
kasemaje mbona unatuogopesha
Miriam:
oh mama
Mary:
nini?
Miriam:
ananipenda…
Ariana:
jamani tunajua hilo…
(wanacheka)
Keddy:
(anakuja) jamani (anamuona Miriam) usiniambie lile gauni la
Uturuki ndo hilo…
Miriam:
no mama…(anacheka) hilo hapo
(Gauni
la gharama tena lenye mkia mrefu limening’inizwa juu)
Keddy:
Oh My God…
Miriam:
vipi?
Keddy:
it is so beautiful…utapendeza sana…
Miriam:
ngoja nivae
(wanamsaidia)
Mary:
wow…haya twendeni
(wanaondoka)
Miriam:
(amependeza sio utani)
(Baada
ya dakika kadhaa wanafika kanisani ambako tayari kuna watu wameshafika na
miongoni mwa watu wale yupo Jeremy yaani bwana harusi)
Vincent:
(kwa Ken) naomba umsindikize Miriam kwa mumewe
Ken:
wewe ni baba yake…
Vincent:
wewe ndo baba yake naomba umpeleke mtoto wetu kwa mumewe
Ken:
sawa…asante sana...
Vincent:
hapana wewe ndo asante sana…asante kwa kumlea mwanangu kwa miaka 19 Mungu
akubariki sana
Ken:
usijali ndugu yangu (anamkumbatia)
Mary:
(kwa Keddy) haya mshike mkono mwanao...umsindikize kwa mumewe
Keddy:
(anamshika mkono Miriam)
Miriam: (anatabsamu) G yuko wapi?
Mary:
yupo na mjomba wake usijali
Miriam:
okay…twendeni sasa
(mlango
unafunguliwa)
Miriam:
(akiwa ndani ya gauni matata anaachia tabasamu ang’avu mara baada ya kuwaona
watu)
Watu:
(wanafurahia uzuri wa Miriam)
Jeremy:
wow…this is the woman that I want to spend the rest of my life with…my dearest
little mama
Miriam:
(anatabasamu mara baada ya kumuona Jeremy wake)
Jeremy:
(anang’ata midomo) God made my woman just like the way I imagined
Miriam:
(akiwa sambamba na wazazi wake wa kufikia taratibu wanaekekea alipo Jeremy)
Jeremy:
come my love…come and make the world believe in the existence of God of amd that everything is possible with God
Miriam:
(anajongea alipo Jeremy)
Jeremy:
(anatabasamu)
David:
(anatabasamu)
Mama
Jeremy: mwanangu hatimaye umepata yule uliyemtaka mwanangu nah ii ulifanya
mwenyewe ulituomba tukutafutie mke siku umeenda kumuona mke ukakutana na
mwanamke wa maisha yako na sasa unaenda kumfanya kuwa mama wa familia yako (anatabasamu)
Miriam:
(anafika alipo Jeremy anamshika mkono)
Ken:
(anamkumbatia Jeremy) take care of our princess…
Jeremy:
she is my queen papa I will always take care of her…
Keddy:
(anatabasamu)
Mary:
(amekaa walipo waumini wengiine) mwanangu… (anatabasamu)
Vincent:
(anamuona) mwenzetu vipi mbona unatabasamu mwenyewe?
Mary:
nimefurahi…mwanangu kapendeza jamani…asante kwa yote mume wangu
Vincent:
hapana mimi mbona sijafanya kitu?
Mary:
Vincent…
Vincent:
ona wameanza tulia
Jeremy:
(anamshika mkono Miriam)
Miriam:
(anamshika mkono pia)
(kwa
pamoja wanamgeukia mchungaji)
Mchungaji:
(anatania) mbona mmependeza sana
Watu:
(wanacheka)
Jeremy:
(anacheka pia)
Mchungaji:
bwana Yesu asifiwe kanisa
(wanaitikia)
Mchungaji:
leo tumekusanyika hapa kushuhudia muungano wa wawili hawa Jeremy David na
Miriam Vincent Mshana
Watu:
(wanasikiliza kwa umakini)
Mchungaji:
(kwa Jeremy) Jeremy je unamchukua Miriam kuw mke wako wa maisha kwamba
utamtunza, kumpenda na kumthamini siku zote za maisha yako mpaka pale kifo
kitakapowatenganisha?
Jeremy:
kwa moyo wangu wote ndio
(watu
wanashangilia)
Mchungaji:
(kwa Miriam) Miriam je unamchukua Jeremy kuwa mume wako kwamba utampenda
na kumheshimu katika shida na raha mpaka pale kifo kitakapowatenganisha
Miriam:
kwa moyo wangu wote ndio
(watu
wanashangilia)
Mchungaji:
basi kwa ukiri wenu naomba pete ili zoezi hili likamilike
(zoezi
la pete linaendelea na hatimaye wawili hao wanatangazwa kuwa mume na mke)
Mchungaji:
na sasa ni bwana na bibi Jeremy David
(Watu
wanawapongeza sana, maharusi wanasaini vyeti vya ndoa wanapomaliza
wanavionyesha kwa watu ili waone)
Colton:
(anampeleka Glory kwa mama yake)
Miriam:
oh, my baby...
(wanapiga picha za ukumbusho
na kila mmoja wao anaonekana kufurahia yale yanayoendelea mahali hapo, wale
wapenzi waliopitia magumu mengi n abado wakasimama imara sasa ni wanandoa na
wazazi wa mtoto wa kike kweli MUNGU MKUU akiamua kwa ukuu wake inatokea kama
ilivyo wa Miriam na Jeremy.Picha zinaendelea kupigwa na watu mbalimbali na
Miriam anaonekana kufurahi sana lakini furaha yake haishindi ile ya mumewe
mpenzi)
Jeremy: we did it my love (anamkumbatia
mkewe)
Miriam: yes my love with God’s
greatness we did it (anamkumbatia)

0 Comments