SCENE
8: -
(Edwin
yupo nyumbani kwake na anaonekana wala hana dalili ya kutoka nyumbani siku hiyo,
anavuta sigara huku anakunywa kinywaji kikali yaani pombe, na anaonekana ana
hasira sana na mawazo pia)
Edwin:
dah!!yule demu ni bonge la demu sijui Patrick alimtoa wapi kudadeki…demu mkali sana,
namtaka kwa udi na uvumba yaani sijawahi kuvutiwa na mwanamke kama
nilivyovutiwa na huyu dada sijui kwanini sikumuona mapema jamani, ila sio mbaya
ngoja nipate msaada kwa yule rafiki yake (anachukua simu yake kubwa aina ya
iphone na kumpigia Monica, inaita kwa muda kisha inapokelewa)
Monica:
hello…
Edwin:
Yes, mrembo…mambo.
Monica:
poa nani?
Edwin:
Edwin, rafiki yake Patrick
Monica:
aaah!!!Sawa vipi za toka Jana?
Edwin:
nzuri…za kwako?
Monica:
ah!!!Tunamshukuru Mungu Kwa wema wake tunaendelea vizuri
Edwin:
sawa kabisa…uko wapi?
Monica:
nyumbani kwangu
Edwin:
wapi?
Monica:
mkolani
Edwin:
mkolani?
Monica:
ndio...
Edwin: samahani
unaweza kupata nafasi ukaja nyumbani kwangu? nina mazungumzo na wewe kidogo
Monica:
mazungumzo gani tena jamani mbona unaniogopesha? ya kheri hayo?
Edwin:
ya heri kabisa kuwa na Amani
Monica :(
anaguna kidogo)
Edwin:
we njoo wala usijali sio mabaya Sana
Monica:
sawa…ila nakujaje? Maana sina hata nauli wala sipajui kwako
Edwin:
hiyo niachie Mimi usiumize kichwa mrembo namtuma dereva wangu sasa hivi
atakupitia hapo muda si mrefu
Monica:
poa…atanikuta
Edwin:
poa (anakata simu kisha anaenda nje kumuita dereva wake) Raphael…
Raphael:
naam…
Edwin:
njoo nikuagize
Raphael :(
anamuendea) nambie…
Edwin: nenda
mkolani…nakupa namba ya dada Fulani utaenda kumleta
Raphael:
shemeji nini?
Edwin:
hapana rafiki yake... (Anatabasamu)
Raphael:
wewe nae mtata…
Edwin:
kwanini?
Raphael :(
anachukua simu yake) haya taja namba
Edwin :(
anamtajia)
Raphael
:( anamaliza kuandika kisha anaweka simu mfukoni mwake kisha anaondoka)
Edwin :(
anarudi ndani, anakaa kwenye sofa safi, anawasha na runinga kubwa
iliyobandikwa ukutani kwake kisha anaanza kufurahia muziki)
BAADA
YA NUSU SAA
(Dereva
anamleta Monica katika jumba Safi la Edwin, Monica analishangaa sana jumba lile
ni kubwa zuri, kuna walinzi kuna watumishi mbalimbali anaonekana kuvutiwa)
Monica
:( anajisemea moyoni) bonge la jumba lakini ya Patrick ndo basi kabisa
Raphael:
karibu dada…boss yupo huku (anamuongoza njia)
Monica :(
anamfuata)
(Wanafika
alipo Edwin)
Edwin:
oh…Monica eeh
Monica:
ndio Monica
Edwin:
karibu nyumbani kwangu...Kwenye himaya yangu
Monica:
Asante Sana (anaangaza huku na huku) yeah…pazuri sana
Raphael
:( anatoka nje)
Edwin:
kadada…embu njoo umsikilize...Mgeni
Kadada :(
anakuja)
Monica:
Mimi juisi tu…mdogo wangu
Kadada:
sawa (anaelekea jikoni)
Edwin:
sawa nambie…rafiki yako hajambo? (Anang’ata midomo)
Monica :(
anacheka kidogo)
Edwin:
mbona unacheka sasa
Monica
:( anacheka kidogo) unaonekana umempenda Sana
Edwin:
siwezi kudanganya…ni kweli kabisa nampenda mno
Monica:
si mpenzi wa rafiki yako
Edwin: I
do not care
Kadada
:( analeta kinywaji anamkaribisha kisha anaondoka)
Monica:
Eddy?
Edwin:
yaani nampenda Olivia kupita kiasi na kitu kilichonifanya nikuite hapa leo ni
hicho…unanisaidiaje nimpate Olivia?
Monica
:( anacheka)
Edwin:
ukinisaidia nitakupa pesa na kukupangia chumba kizuri na hata biashara nisaidie
tu kumpata Olivia
Monica:
hata Mimi namtaka Patrick
Edwin :(
anatabasamu huku anatikisa kichwa ishara ya kukubali) hapo sasa umenena…
Monica:
namtaka Patrick kuliko hata unavyomtaka Olivia…
Edwin:
hapo sasa ndo tunaongea lugha moja rafiki yangu
Monica
:( anacheka kidogo)
Edwin:
nini kifanyike?
Monica:
nakusikiliza
Edwin:(anatabasamu
kidogo) tuwagombanishe wachukiane milele, yaani tutafute kitu ambacho
hawajawahi kuambiana kwa mfano mimi nina kitu kimoja ambacho nakijua kuhusu
Patrick na nina uhakika hajawahi kumwambia olivia nina uhakika
Monica:
nini hicho?
Edwin:
hapa sasa ndo nahitaji msaada wako, Patrick aliwahi kuwa muuza madawa ya
kulevya miaka mingi iliyopita na aliwahi kufungwa South Africa, wazazi wake
walimtoa na alipotoka hakuwahi kuyauza tena ndo wazazi wake wakafanya mpango wa
kumpa biashara ya madini
Monica
:( anashangaa) aisee…
Edwin:
ndo hivyo ulikuwa bonge la msala sema pesa za wazazi wake zilimuokoa…yaani
angenyongwa yule
Monica
:( anashangaa)
Edwin:
Nina uhakika hajawahi kumwambia Olivia…na ni vitu vya muhimu sana hasa pale
unapoanza mahusiano na mtu…ni vyema ukamwambia
Monica:
sasa mimi nitamwambiaje Olivia?
Edwin:
si katika stori…unajifanya nimeshakuwa mtu wako…kwamba nikakwambia ukweli juu
ya maisha yangu tukajikuta tunamzungumzia Patrick ndo tukaongea hayo…ila
mwambie asitutaje kwa Patrick
Monica:
sawa…Hilo ni wazo zuri sana…
Edwin: yes,
na ninavyojua wanawake huwa hawapendi kufichwa kitu na wapenzi wao
Monica:
kabisa na hivyo basi…nitaenda kesho kwa Olivia
Edwin:
akivunjika moyo Mimi ndo nitamtuliza Kwa kisingizio cha shemeji, shemeji…halafu
mwisho wa siku ataingia tu mkenge, wakati huo na wewe jitahidi kuwa karibu na
Patrick halafu mwisho wa siku atakuwa wako
(Kwa
pamoja wanagonga glasi na kufurahi sana)
Monica:
hatimaye, Patrick atakuwa wangu
Edwin:
na Olivia atakuwa wangu…yaani hawataamini kuwa wanaachana kizembe hivyo
Monica:
wanajifanya kupendana sana utasema wao ndo wa kwanza kuwa na mahusiano
Edwin:
kumbe na wewe sio mtu wa mchezomchezo eeh…
Monica:
sio kidogo rafiki yangu
Edwin:
cheers
Monica:
cheers… (Wanagonga glasi)
Edwin:
oh…Patrick my brother, Olivia sio wako tena nishamchukua
Monica:
Olivia, Patrick sio wako tena ni wangu na nishamchukua
(Kwa pamoja wanacheka Sana na kushangilia ushindi
ambao bado haujawa, wanaendelea kunywa na kucheka kwa muda mrefu sana)
Monica:
hii ni kwa ajili ya ushindi wetu…
Edwin:
yes…
Monica
:( anacheka)
Edwin:
yes…
Monica:
kumbe Patrick ana dark past
Edwin:
yaani halafu alikuwa anauza na kuyatumia, amehenyesha watu yule kuwabebesha
watoto wa watu madawa matumboni mwao
Monica:
sipatii picha Olivia atakavyochukia
Edwin:
Nina uhakika kuwa atakasirika sana
Monica:
Sana maana ni mlokole huyo atahisi labda bado Patrick anayauza yaani itakuwa
mtafaruko
Edwin:
si ndo tunaoutaka kwao
Monica:
wewe sio wa mchezo baba
Edwin:
usinichezee
(Wanacheka huku wanagonga glasi)

0 Comments