ON MY WEDDING DAY 09


 

SCENE 9: -

(Monica anafika nyumbani kwa kina Olivia, anapofika nyumbani hapo anagonga mlango na haraka Olivia anafungua mlango)

Olivia:(anafungua mlango, anatabasamu mara baada ya kumuona rafiki yake) Monica, karibu shoga yangu…

Monica:(huku anaingia) asante shoga yangu…

(wanafika sebuleni, wanakaa kwenye sofa za gharama zilizopo sebuleni hapo)

Olivia: nambie unatumia kinywaji gani?

Monica: maji tu shoga yangu

Olivia:(anatabasamu) poa… (anaenda jikoni)

Monica:(anabenjua midomo kisha anafyonza)

Olivia:(anarudi akiwa amebeba glasi mbili za maji moja anampa rafiki yake huku nyingine akiitumia yeye) enhe (anakunywa kidogo) nambie…shemeji anasemaje?

Monica:(anakunywa kidogo) ah…Edwin?

Olivia: sasa je au una bwana mwingine shoga yangu?

Monica: ah…wapi nina yeye tu...hana usemi anakusalimia…sana

Olivia:(anacheka kidogo) kweli eeh…hata mimi namsalimia pia (anacheka tena)

(kimya kidogo)

Monica:na wewe shem anasemaje?

Olivia: utamuweza? yupo tu...

Monica: mnaendelea vizuri tu…

Olivia: sana…

Monica: vizuri sana… (anajisemea moyoni) muda wa kuendelea vizuri umeisha mama…namtaka Patrick ili anifanyie haya aliyokufanyia Olivia...

Olivia: vipi? mbona kimya ghafla?

Monica: sina cha kuongea tena ndugu yangu

Olivia:(anacheka)

Monica: kwahiyo mnaaminiana sana na hakuna mnachofichana

Olivia: hamna kitu tunachofichana...ananiambia kila kitu yaani ananipenda kweli na hanifichi jambo...si unajua tunaandana kuwa wanandoa

Monica: hata wewe ile inshu ya yule mzee kukuchumbia kisha kukuacha kwenye mataa nayo umemwambia

Olivia: hilo nilimwambia hata kabla hatujaanza mahusiano kipindi hicho ndo tunachati kama marafiki

Monica: kumbe…basi kumbe mnaaminiana sana

Olivia:(anacheka) na kupendana pia…nampenda Patrick na kumheshimu sana na Zaidi namuamini sana nay eye ananiamini sana…

Monica: basi vizuri…kumbe hata aliwahi kukuambia kuwa aliwahi kuuza na kutumia madawa ya kulevya? akakamatwa huko South Africa?

Olivia:(anashtuka sana) alikuwa anauza madawa ya kulevya …na kutumia pia? mbona hakuniambia hili?

Monica…dah!!!sasa utasemaje kuwa mnaaminiana na kuambiana mambo yenu yote mbona mwenzio anaonekana hakuamini na kukuficha?

Olivia: siamini kabisa kwa kitu unachoniambia…Patrick anajifanya kunipenda kumbe ananificha mambo yake

Monica: ila naona kuwa sio kosa kubwa sana

Olivia: inategemea na jinsi tulivyowekeana, tumewekeana kuwa tunaambiana kila kitu… (anachukua simu yake na kupiga) ngoja nimpigie… (ananyanyuka na kwenda zake chumbani kwake) Patrick...

Patrick: mwanamke…nambie mpenzi wangu

Olivia:(anaonyesha jazba) jamani Patrick kwanini hukuniambia kuwa uliwahi kujihusisha na madawa ya kulevya

Monica:(anamchungulia kwa mbali) kimewaka(anatabasamu)ngoja nimwambie Edwin (anapiga simu kwa Edwin, simu inaita hatimaye inapokelewa) kimewaka huku…

Edwin: usiniambie…

Monica: sana…Olivia kakasirika mi namjua huyu hapendi uongo sana

Edwin: safi…sana… (anakata simu)

(kwa Olivia)

Olivia: Patrick unajua kuwa nachukia uongo

Patrick: tulia nakuja tuzungumze

Olivia: hapana Patrick we ni mtu hatari nitajuaje kuwa hauzi tena hayo madawa? Sitaki kukuona tena sitaki kukuona tena, Patrick…it is over…

Patrick: usinifanyie hivyo Olivia…wewe mwenyewe unajua navyokupenda…ni kosa ndio lakini sio kosa kubwa la kufanya penzi letu likaharibika…mpenzi wangu...

Olivia: niache Patrick… (Anakata simu)

Patrick :( anampigia) pokea simu tafadhali…

Olivia: yaani amenifanya mimi mtoto mdogo ananificha mambo yake pengine anaendelea kuyauza...Siwezi kuwa na mwanaume muuza madawa ya kulevya... (Anarudi sebuleni)

Monica: vipi shoga yangu?

Olivia: nimeachana na Patrick…yaani simtaki maana kama amenificha inamaana kuwa bado anayauza na sitaki kuolewa na mwanaume muuza madawa ya kulevya

Monica :( anacheka chinichini, akiangaliwa na Olivia anajifanya kuhuzunika)

Olivia: yaani wanaume

Monica: yaani waache tu…wapo kama wamezaliwa na baba mmoja, ila mimi nimeambiwa kila kitu na Edwin na kwamba walikuwa wanauza madawa ya kulevya ila kwa sasa wote wameacha na aliongea hivyo akijua labda tayari ameshakuambia

Olivia: hajaniambia na labda ni kwasababu anaendelea kuuza madawa hayo, mi nitatoa taarifa polisi asilete utani na mimi

Monica: muache usimsemee mwenzio jamani

(Baada ya dakika chache mlango unagongwa, haraka Olivia anaenda kufungua anakuta ni Patrick, anaufunga mlango)

Monica :( anajisemea moyoni) ah…huyu nae amekuja kufanya nini?

Olivia: naomba uondoke nyumbani kwangu…Patrick nadhani nimeshakuambia kuwa sitaki mahusiano na wewe na kila kitu ulichonipa nitakurudishia...

Patrick: jaribu kunisikiliza...Olivia…ni kweli

Olivia: too late Patrick...Siwezi kukusikiliza tena…iam sorry we endelea tu na maisha yako uliyoyachagua…

Patrick: don’t panic my love embu kaa utulie…tafakari

Olivia: haina haja ya kutafakari chochote Patrick…it is over basi…ngoja nifunge kila ulichonipa kesho nitakuletea nyumbani kwako…

Patrick: haina haja kurudisha nilivyokupa

Monica :( anacheka chini chini)

Olivia: nilikupenda Sana Patrick…lakini badala yake ukawa unafanya mambo bila ya mimi kujua…it is over Patrick…nimeachana na wewe…Monica

Monica: abeeee….

Olivia: mwambie Patrick aondoke…

Patrick :( anaondoka kimya kimya)

Olivia :( anajikuta anapata uchungu) hivi unajua kuwa Patrick alikuwa mbioni kuja kunichumbia ili anioe?

Monica: dah…sasa si umsamehe mwenzio kakosa kenyewe kadogo hivyo jamani?

Olivia: Siwezi…na hilo kosa sio dogo…nimemuacha kuanzia sasa hivi

Monica: utamwambiaje mama yako?

Olivia: nitajua mwenyewe…iam sorry naomba Kama hutojali naomba nibaki peke yangu…

Monica: bila shaka rafiki yangu (anabeba mkoba aliokuja nao na kuondoka zake) kwaheri

Olivia: poa…tutaonana (anaingia zake chumbani kwake)

Monica :( anatoka nje kisha anampigia simu Edwin inaita kisha inapokelewa) hello…Edwin…wameachana kabisaaaa

Edwin: Safi sana…cha kuombea usiku wasiongee maana wanaweza kuyajenga

Monica: ndo hivyo…

Edwin: kesho asubuhi…nenda kwa Patrick na mimi kwa Olivia…tutajifanya tunawapooza kujenga urafiki na hatimaye mapenzi…

Monica: ndo hivyo…hongera mume mtarajiwa wa Olivia

Edwin :( anacheka kidogo) Na wewe hongera mke mtarajiwa wa Patrick…

(wanacheka kisha wanakata simu Kwa pamoja)

Monica: pole Sana Olivia… (Anacheka kisha anaendoka zake)

(Upande wa Olivia bado anaonekana ana hasira juu ya habari ya Patrick)

Olivia: yaani Patrick jamani mbona anaonekana mstaarabu halafu aliniambia kuwa yeye ni mlokole au nalo ni kwasababu anajua mimi ni mlokole kaamua kuniingia hivyo? namchukia kama ndo mipango yake ndo hiyo(Analia )jamani shetani huyu…kwanini kila nikifika hatua nzuri na mwanaume ni lazima mambo yaharibike?Patrick mpenzi wangu jamani(Analia)nimeachana nae na sijui kama kuna uwezekano wa kurudiana na yeye naumia sana mahusiano yetu yameisha pamoja na ahadi nyingi…(Analia)je anaweza kuwa bado anayauza ndo maana haniambii?je nimshtaki…au ngoja nimuache tu maana nampenda na wala sitataka kumuona akiwa na matatizo yoyote…lakini kwanini nimempenda mwanaume ambae ni tishio kwa jamii?

Mama :( anamuangalia Kwa mbali na anahakikisha uwepo wake haugunduliwi na Olivia) huyu mtoto ana nini jamani mbona Analia? Sipendi kumuona Analia sijui nini…nitamuuliza...Ngoja atulie (anaendelea na shughuli zake)

Olivia :( anaendelea kulia Kwa uongo wa Patrick) najua mpaka leo atakuwa anayauza..Hajaniambia tu…sasa mwanaume wa hivi ni mtenda dhambi na sipo tayari kuwa nae, its over Patrick huna tena nafasi kwangu nakuchukia sana

(Upande wa Patrick amekaa kwenye gari yake na anaonekana ana mawazo sana)

Patrick: dah!!!Olivia amechukia sana kwa kitendo cha kutomwambia ukweli wote wa maisha yangu ningejua basi ningemwambia kila kitu...na ninamjua aliyewaambia yote hayo…ni Edwin yamkini alikuwa anaongea tu na mpenzi wake kama kuongea lakini kwa kuwa wanawake wamebobea kwenye umbea basi Monica kampelekea umbea kwa mpenzi wangu…usijali mama wewe punguza hasira nitarudi kuongea na wewe (anawasha gari kisha analiondoa)

(Upande wa Olivia)

Olivia: nakupenda Sana Patrick mpenzi wangu

Patrick: nakupenda Sana kipenzi changu…nakujitaji bado

Olivia: ila nakuchukia umenidanganya eti wewe mlokole kumbe muuza madawa nachukia uongo (Analia)

Patrick:(bado anaendelea kuendesha gari lako) nakupenda Olivia utaendelea kuwa wangu

Olivia:(akiwa bado amekaa chumbani kwake) madawa ya kulevya si yanaweza kuua mtu? kwahiyo Patrick alikuwa muuaji? (Analia)

(Patrick anaendelea kuendesha gari lake kuelekea nyumbani huku Olivia bado Analia)

Post a Comment

0 Comments