SCENE 10: -
(Raymond anaingia ofisini kwake akiwa Ni mtu
mwenye furaha Sana, anaketi kwenye kiti chake anachukua simu ya mezani na
kumpigia sekretari wake)
Raymond: Glory…naomba uniletee lile faili la Jana
tafadhali…
Glory: sawa boss... (Ananyanyuka anachukua faili Hilo na bila kupoteza muda anaingia ofisini
kwa Raymond akiwa ameshika faili) habari za asubuhi boss
Raymond: nishakwambia usiwe unaniita boss…niite tu
kaka
Glory :( anacheka
kidogo)
Raymond :( anaimba
wimbo Fulani wa dini)
Glory: mbona Leo unaonekana una raha sana?
Raymond: we acha dada...Kwani naonyesha mpaka usoni
kuwa Nina raha eeh
Glory: kabisa
Raymond: dada Mungu anajibu maombi Sana unajua eeh
Glory: kwanini?
Raymond: sijui nikwambie? Sijui itakuwa mapema
Sana? Anyways, ngoja nikwambie iam in love…
Glory: wow...Kweli na nani?
Raymond: hiyo sasa ni siri yangu kwanza ila we jua
kuwa iam in love
Glory: hongera Sana brother au na huyo mkeo
mtarajiwa?
Raymond: ah…wapi sio na huyo kivuruge (anacheka)
Glory: una maneno wewe (anacheka)
Raymond :(
anacheka)
Glory :( huku
anaondoka) ngoja mi niende nisije nikakutwa hapa na mkurugenzi mkubwa hapa
ikawa shida (anatoka)
Raymond: poa we kaendelee na kazi acha mimi niwaze
(anacheka sana) ahh!!!(anajisemea mwenyewe)nimemkumbuka yule Mrembo…(anatabasamu)mimi nina nini jamani yaani
mdada amekuja jana tu leo kanijaa akilini utasema sijui nini?yaani Christina
simtamani kabisa yule mwanamke..kanitoka kabisa…lazima nijenge mahusiano na Angelina
anaonekana ni mtu mzuri sana na mpenda watu,ngoja nipige nyumbani angalau tu
nisikie sauti yake ndo niendelee na kazi zangu(anacheka)jamani ukisikia love at first sight no hii jamani(anachukua simu yake na kupiga simu ya mezani
ya numbani kwake,inaita sana bila majibu hatimaye inakata)mbona hapokei?(anapiga tena)ngoja nimjaribu Ramadhani
pale getini(inaita kwa muda kidogo tu
halafu inapokelewa)nambie Rama kwema hapo?
Ramadhani: kwema za kazi
Raymond: nzuri kaka...Angelina yupo hapo?
Ramadhani: yupo bustanini anamwagilia Maua…vipi?
Raymond: ah!!Poa tu kuna maagizo nataka nimwambie
sasa sijui unaweza kuniitia mara moja mtu wangu
Ramadhani: usihangaike Ray…niambie tu nitamwambia
Raymond: muite tu…nimwambie if you do not mind my
friend
Ramadhani: sawa haina shida kabisa mtu wangu…kata
nimuite halafu nitakupigia hata kwenye simu yangu
Raymond: poa nibipu tu mara moja
Ramadhani: poa (anakata
simu kisha anaenda bustanini alipo Angelina) wewe dada…boss anataka kuongea
na wewe kwenye simu…
Angelina :( anaacha
alichokuwa anafanya kisha anamfata)
Ramadhan :(
anambipu Raymond)
Raymond (haraka anapiga inaita kisha inapokelewa)
nambie
Angelina: shikamoo kaka
Raymond: marahaba Angelina hujambo?
Angelina: sijambo kaka…za kazi?
Raymond: nzuri tu
Angelina: Ramadhani ameniambia kuwa kuna kitu
unataka kuniambia kaka
Raymond :(
anashikwa kigugumizi) …yes…ah…vipi umekula? Ah…mchana utakula nini? Au
utapika nini?
Angelina :( anacheka
kidogo) kaka bwana Jana si uliniambia Leo nipike wali samaki na mboga za
majani ndo nitapika hivyo kaka au unataka kubadilisha?
Raymond: hapana hiyo iko sawa mdogo wangu…nilitaka
tu kujua Kama uko makini na kwamba husahau kitu…
Angelina: nipo makini kaka yangu
Raymond: vizuri…tutazungumza baada kidogo mdogo
wangu
Angelina: sawa kaka…uwe na kazi njema huko ulipo
Raymond: Asante (anatabasamu)
Angelina: Asante kaka
Ramadhani: poa rudisha simu sasa
Angelina :(
anamrudishia Ramadhani simu yake kisha anaenda kuendelea na kazi zake)
Ramadhani: haya poa…. (Anamuangalia kwa matamanio)
mtoto mzuri huyu mweeeee (anaingia
kibandani kwake)
(Huku ofisini alipo Raymond)
Raymond:(anatabasamu)
yaani mimi nimekuwa kama mtoto…mapenzi bwana…(anaegemea meza kama vile kujilaza)nampenda Angelina na ninatamani
kila saa niwe naongea nae jamani(anaguna
kidogo) Edmond akijua si ataniua mimi…embu nijitahidi kuficha…ila hapana
cha kufanya nimwambie tu Angelina pamoja na Edmond au itakuwa haraka sana maana
napo haraka haraka haina Baraka na mwenda pole hajikwai…ila pia ngoja ngoja
huumiza matumbo na pia unaweza ukachelewa ukakuta mwana sio wako sasa nifanyeje
na nafsi yangu kweli inakiri kwamba nimempenda sana Angelina na niko tayari kwa
lolote,matusi ya baba,vitisho vya Christina ila siko tayari kugombana na rafiki
yangu aliyeniaminia akaniletea huyu malaika…nampenda Angelina…I swear nampenda
kuliko kawaida…she is the woman that I have always wanted(anatabasamu kidogo)she is beautiful and
kind,hardworking,responsible yaani anaweza kuilea familia hata kama hali ni
mbaya she is the opposite of Christina…(anakaa
vizuri kisha anaendelea na kazi zake)lazima nimwambie mapema kuwa nina
mchumba ndio ila nafsi yangu imempenda yeye…(anaguna)lakini atanielewa kweli jamani?ok ngoja nimwambie tu…potelea
mbali au ngoja nisubiri kidogo itakuwa haraka sana hiyo(anaendelea na kazi zake kama kawaida)oh My God kwanini siwezi
kufanya kazi zangu,namuwaza sana Angelina…huyu binti amenipa nini mimi jamani
mbona nakuwa chizi sasa,embu niache ujinga wagonjwa wananihitaji kwa kila
hali…natakiwa kuweka akili na nafsi yangu kwenye hii kazi(anafanya kazi)oh no
nataka kumuona kabisa hata ikiwa kwa mbali nataka kumuona…(anatafakari jambo)No Raymond embu kaa utulie bwana,huyo ni shemeji
wa rafiki yako…ukileta stori za mapenzi hapa itakula kwako na isitoshe wewe ni
mume mtarajiwa wa mtu(anajilazimisha
kuendelea na kazi)no…ngoja niende nyumbani mara moja nimuone hata kwa
mbali(ananyanyua anabeba koti lake la
suti)ila mimi mjinga yaani naacha kazi naenda kwa mwanamke…(anajishangaa)kwani huyu mtoto amenipa
nini mimi jamani kiasi cha kuwa mjinga hivi(anakaa)ngoja
niendelee na kazi zangu nitamuona jioni(anavuta
kompyuta yake na kuendelea na kazi)nampenda sana Angelina wangu,ipo siku
tutakuwa tu…ngoja niwe mpole na mvumilivu(anaendelea
na kazi zake)
Sekretari
:( anakuja akiwa amebeba faili lingine)
boss umemaliza kufanyia kazi Hilo faili lipo lingine
Raymond:
kwanza umerudia kuniita boss huku nimeshakukataza lakini pili hilo faili hata
sijaligusa…
Sekretari:
kwanza samahani kwa kujisahau na kukuita boss…lakini pili kwanini hujashika
faili?
Raymond:
naona basi…ile sura ya kipenzi inakuja mara nyingi nyingi kwenye faili
(Wanacheka Sana)
Sekretari
:( anacheka Sana) aaah ila wewe
hapana…sasa si umpigie simu
Raymond:
hana simu
Sekretari:
mnunulie wifi simu usilete ujinga
Raymond:
eti ee…hiyo ni kweli dada ngoja nimnunulie simu niwe nampigia kila saa ila sasa
akipokea sijui nitakuwa nafanyaje
Sekretari:
kwanini?
Raymond:
huwa napigwa butwaa nikisikia sauti yake
(Wanacheka tena)
Raymond:
kiukweli sijawahi kumpenda mwanamke hivi
(Wanabaki wanacheka)
0 Comments