SCENE 11: -
(Raymond
anarudi nyumbani kwake mara baada ya kumaliza kazi zake za siku, anapofika kama
kawaida anafunguliwa geti na Ramadhani ambae ni mlinzi wake na mara baada ya
kufunguliwa geti anaingiza gari na kuliegesha eneo la maegesho halafu haraka
hata bila kumsalimia Ramadhani anaingia ndani)
Raymond :( huku
anakaa kwenye sofa dogo lililopo hapo sebulen) Angelina…
Angelina :( anatokea
chumbani kwake) abee kaka
Raymond :( anamuangalia
kwa muda kisha anaachia tabasamu zuri)
Angelina :( anatabasamu
pia) kaka mbona unacheka?
Raymond: sicheki natabasamu
Angelina: kwanini?
Raymond: nimefurahi kukuona mdogo wangu au
siruhusiwi kufurahi nikikuona?
Angelina: wala!!(Anacheka) hata Mimi nimefurahi kukuona kaka, za kazi?
Raymond: nzuri tu…za hapa?
Angelina: nzuri tu
Raymond: umeshapika?
Angelina: ndio kaka, nimemaliza kupika ndo nikaenda
kuoga
Raymond: sawa mdogo wangu... (Anavuta begi lake la kazini na kutoa simu aina ya Samsung Note 10 na
kumkabidhi)
Angelina: kaka...hii simu?
Raymond: zawadi…nimekuletea zawadi, umefurahi
Angelina: nimefurahi lakini si itakuwa bei sana
kaka yangu?
Raymond: kawaida tu dada
Angelina: huo ni Zaidi ya mshahara wangu kaka
kwakweli asante ila sitaweza kabisa kuipokea simu ya bei hivi
Raymond: tafadhali naomba uipokee Angelina napenda
kuongea na wewe mara kwa mara mdogo wangu
Angelina: kaka
Raymond: ipokee tu
Angelina: Mimi nina malengo mengi sana na mshahara
wangu kaka, familia yangu inanitegemea kwa asilimia 80 kaka yangu
Raymond: sitakukata mshahara wako hata shilingi
Angelina: kweli kaka?
Raymond: niamini mimi mdogo wangu (anampa) ipokee tu mama
Angelina :( anaipokea
kwa heshima) Asante kaka
Raymond: usijali mdogo wangu
Angelina :( anaifungua)
Mimi kitambulisho changu nilikisahau nyumbani labda kesho unipe simu niongee na
Catherine anipe cha kwake ili niweze kusajili laini
Raymond: nimeshakusajilia mdogo wangu...Kutumia
kitambulisho changu na namba ya kwanza nimeweka ya kwangu nyingine labda ya
shemeji itaingia hapo baada ya kwangu
Angelina :( anacheka
Sana) ya shemeji?
Raymond: ndio shemeji yangu kwako…kwani wewe huna
mpenzi?
Angelina: hapana sina na wala sina mpango wa kuwa
nae kwa sasa…nina mambo mengi sana
Raymond: unapika vizuri, una heshima na Zaidi una
sura nzuri na umbo zuri utakosa kweli mwanaume au ulikuwa nae ukaachana nae?
Angelina: hapana kaka sijawahi kuwa na mpenzi
Raymond :( anatabasamu)
njoo ukae hapa…
Angelina: hapana kaka sitaweza acha tu nisimame
Raymond: kwanini hautaweza?
Angelina: mke wako anaweza akaja ghafla akanikuta
nimekaa kwenye sofa la gharama tena na wewe
Raymond: ok... (Anasimama
nay eye) tuongee tumesimama
Angelina: kaka kwanini unafanya hivyo?
Raymond: nasimama Kama wewe…
Angelina :( anacheka
kidogo)
Raymond :( anatabasamu)
Angelina :( huku
anatafuta sofa la kukaa) haya nimekaa
Raymond :( anamfuata
alipokaa)
Angelina: kaka si ukakae ulipokuwa umekaa jamani
Raymond: yaani wewe humuogopi Christina Bali
uananiogopa Mimi sijui unahisi nitakubaka yaani hauna uhuru kabisa
Angelina: sio hivyo kaka
Raymond: Bali ni nini?
Angelina: haileti tu picha nzuri ulivonisogelea
hivyo kaka yangu
Raymond: Mimi mbona nimekusogelea kawaida tu
Angelina: haya kaka tuendelee kuongea
Raymond :( anataka
kumshika mkono)
Angelina :( anaogopa)
Raymond :( anajisemea
moyoni) huyu shetani ashindwe…huyu ni mke mtarajiwa wangu sitakiwi
kumuonyesha udhaifu wangu…
Angelina: kaka nashukuru kwa simu ngoja nikaiweke
chumbani kisha nitarudi
Raymond: sawa
Angelina :(
anaondoka haraka)
Raymond: nachotakiwa ni kuwa muangalifu sasa
nikimuonyesha udhaifu mapema naweza kumkosa
(Huku chumbani alipo Angelina)
Angelina: kwanini kaka Raymond alitaka kunishika
mkono? Au alikuwa anataka kunibaka? (Anaguna)
kwanini amefanya hivyo, halafu anavyoniangalia jamani ee, Mungu wangu lazima
niwe makini yaani sitaki kukaa nae karibu…Mimi hapa ni mfanya kazi za ndani na
si vinginevyo
Raymond :( anaenda
mpaka mlangoni kwa Angelina na kisha anagonga) hodi
Angelina :( anaogopa)
Mungu wangu anagonga…sifungui hata kidogo acha agonge mpaka akome
Raymond: Angel…samahani sijui nini tu kilinijia
lakini haikuwa kwa nia mbaya mdogo wangu nisamehe
Angelina :(
anajisemea moyoni) yaani (anaguna)
wanaanzaga hivihivi we unadhani akishanibaka akanipa mimba atanikumbuka kweli
na tayari ana mke huyu (anaguna tena)
acha tu nimjibu mbovu ili anikome, au ndo maana amenipa simu…
Raymond: samahani njoo utenge chakula tule
Angelina :( anafungua
na kumrudishia simu) kaka asante kwa simu ila naona umetaka kuitumia simu
kunichezea
Raymond: hapana Angelina…mimi nimeokoka siwezi
kukufanyia hivyo hiyo simu nimekuletea maana unaweza kukuta saa nyingine nataka
kukupigia labda unakuwa uko mbali na nyumbani sio kwa ubaya Angelina tafadhali
naomba unisamehe, tafadhali, sitaki tugombane maana tunakaa sehemu moja kwanini
tukwaruzane kwa vitu vidogovidogo kama hivi? Mimi sipo hivyo mama
Angelina :( anashusha
pumzi kisha anaguna kidogo) sasa kwanini ulitaka kunishika mkono kwa
mazingira ya utata?
Raymond: ila sijakushika…ningekushika ndo
ungelalamika ila sijakushika mdogo wangu
Angelina: sawa kaka, najua hujanishika ila ulitaka
kunishika inamaana nisingewahi kukuzuia ungenishika…sawa lakini ila mi naomba
tuheshimiane kama kaka na dada…
Raymond: sawa mdogo wangu (anajisemea moyoni) sawa wife… (Anatabasamu)
Angelina: unatabasamu nini?
Raymond: wala…Mimi wala sitabasamu mbona?
Angelina: haya bwana…
Raymond: katenge chakula tuje tule
Angelina :(
anaenda jikoni kisha anaanza kutenga chakula mezani) karibu chakula kaka
Raymond :( anaenda
mezani)
Angelina :(
anamsogezea sahani)
Raymond :( anachukua
huku anamuangalia usoni) mbona umenuna Sana?
Angelina: hapana kaka sijanuna…nimeamua tu
kunyamaza kuwa na Amani kaka yangu
Raymond: usininunie mdogo wangu
Angelina (anatabasamu
kidogo)
Raymond :( anacheka)
ewaaaaa!!!Hapo sasa ndo sawa (anacheka
tena)
Angelina: sawa bwana
Raymond: kaa basi tule
Angelina: hapana kaka Mimi nakaa jikoni
Raymond: twende…tukakae wote
Angelina: kaka
Raymond: mi najua unaniogopa Mimi sitajaribu
kukushika tena chochote we kaa tu na mimi hapa tule
Angelina: haya ngoja nikubali yaishe…tutoke jikoni
twende tukakae huko
Raymond: Mimi nataka hapahapa…nimepapenda
Angelina :( anacheka
kidogo) yaani wewe una utani mkeo akikuta huku jikoni
Raymond: we nae huachi kumzungumzia mke wangu kila
saa mke mke…kuna stori nyingi tu ambazo tukikaa tukazungumza tutafurahia sana
kuliko kila saa mke ah!!!Unanichosha
Angelina :( anacheka)
basi nisamehe kaka sitamzungumzia mke wako tena, hata Kama ikiwa vipi
sitamzungumzia…ila sasa kwanini umekaa jikoni…wakikuta ndugu zako…nitalaumiwa
mimi kwanini nimekuruhusu wewe baba mwenye nyumba kulia chakula jikoni
Raymond: nikwambieje kuwa nilipokuwa peke yangu hi
indo ilikuwa sehemu yangu ya kulia chakula...
Angelina: haya bwana…ngoja nikubali (anakaa chini sakafuni)
Raymond :( nae
anakaa sakafuni)
(Wanakaa pamoja na kufurahia chakula cha jioni,
wanaendelea kula huku wanaonekana kusahau tukio la kutaka kushikana viuno,
wanacheka wanazungumza kwa ufupi wanaonekana kama mtu labda na mke wake au
mpenzi wake maana wanafurahiana kuliko kawaida)
0 Comments