SCENE 9: -
(Jioni ya siku hiyohiyo, Raymond anafika nyumbani kwake)
Raymond :( anapiga
honi)
Ramadhani :( haraka
anafungua geti)
Raymond :( anaingiza
gari lake anafika maegesho, analiegesha kisha anashuka kuelekea chumba cha
mlinzi) Ramadhani…za jioni ndugu yangu
Ramadhani: salama za kazi?
Raymond: njema tu…yuko wapi Angelina...Simuoni hapa
Ramadhani: yupo chumba cha sinema…anaangalia sinema
Raymond: sawa…ngoja nimuone
Ramadhani: ngoja nikuitie (anataka kwenda)
Raymond: hapana usijali...Nitaenda kumuona… (Anaelekea chumba cha sinema baada ya hatua
kadhaa anafika) Angelina…
Angelina :( ananyanyuka
kwa kuwa alikuwa amejilaza) abee…kaka
Raymond :( anakaa
pembeni yake) hujambo?
Angelina: sijambo kaka, shikamoo…
Raymond: marahaba… (Anamuangalia usoni na nafsi yake inakiri ni kweli kabisa amemkubali mtoto
wa kihangaza) unaonekana una heshima
Angelina :( anacheka
kidogo)
Raymond: sawa…naomba uniambie kidogo kuhusu wewe…umri
wako, kabila lako, elimu yako…niambie pia kuhusu familia yako
Angelina: sawa, Mimi kwa majina naitwa Angelina Daniel…ni
mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watano, umri wangu…nina miaka ishirini
na mbili
Raymond :( wakati
huo Angelina anaongea yeye anatabasamu tu huku anamuangalia sana usoni)
Angelina: kabila langu mimi ni mhangaza, na elimu
yangu ni darasa la saba maana nilishindwa kuendelea na elimu yangu ili
kuwaachia wadogo zangu wasome…maana mama yangu alikuwa hana uwezo wa
kutusomesha wote
Raymond: baba yuko wapi?
Angelina: alishafariki siku nyingi Sana
Raymond: maskini
Angelina: ndo hivyo kaka
Raymond: mama ana shughuli gani?
Angelina: hana shughuli yoyote
Raymond: sasa huwa mnaishije?
Angelina: nahangaika Sana…nahangaika kwa ajili ya
wadogo na mama yangu, mama yangu amepooza...Kwahiyo mama yangu hafanyi
kazi…kwahiyo ili maisha yaendelee huwa nafanya kazi mbalimbali ili tupate kula
na kadhalika
Raymond: unaonekena ni mwanamke shupavu sana
Angelina: ukubwa jalala kaka…mabaya yote yanakupata
ili wengine waishi
Raymond: aisee nimekufurahia Sana, sasa Catherine
ni dada yako kivipi?
Angelina: mtoto wa baba yangu mkubwa
Raymond: wenyewe huwa hawawasaidii?
Angelina: si ndo dada Catherine akaniambia nije
huku tena akaniambia kuwa wewe, wewe si ndo Raymond?
Raymond: ndio
Angelina: aliniambia kuwa utakuwa na uhitaji wa
mfanyakazi,kwahiyo nikaja na kweli Mungu ni mwaminifu nikapata kazi tulikuwa
hatua uhakika ila dada akaniambia kuwa nitapata kwako tu na ikawa kweli
Raymond: dah…wewe unasali?
Angelina: ndio nasali T.A.G
Raymond: wow…Kama mimi na Edmond
Angelina: eti eeh…
Raymond: tutakuwa tunaenda kusali jumapili, Mimi…wewe,
Edmond na Catherine…
Angelina: sawa kaka…napenda sana kuongea na Mungu
wangu…maana ameshanitendea makuu mengi maishani mwangu…mimi na familia yangu
tunaishi kwa neema yake
Raymond: dah…nimekufurahia Sana
Angelina: Asante kaka…
Raymond: sawa…ungependa nikulipe shilingi ngapi?
Angelina: yoyote tuu kaka…siwezi kukupangia
Raymond: wewe unataka shilingi ngapi?
Angelina :( anacheka)
Raymond: Mimi nitakulipa laki na hamsini
Angelina: kazi za ndani???
Raymond: utaanzia hiyo…au nimekupunja
Angelina: hapana kaka iko sawa kabisa sema tu
nimeshangaa maana sijawahi kushika pesa nyingi hivyo
Raymond: usijali...Nichukulie Kama kaka yako…ukiwa
na shida utakuwa unaniambia tu tunasaidiana dada
Angelina: sawa kaka
Raymond: haya kaniletee chakula ulichopika
Angelina: sawa kaka
Raymond: umepika nini?
Angelina: wali, nyama na maharage (huku anaondoka)
Raymod: niletee…na ndizi mbivu…napenda sana
Angelina :( anaondoka)
Raymond: eeh huyu ndo mwanamke sasa ni mzuri, mchapakazi,
na jasiri pia nampenda sana…anafaa kuwa mke wangu…iam in love with my
housegirl…nampenda msichana wangu wa kazi…(anatabasamu)
love at first sight...
Angelina :( anarudi
amebeba chakula kwenye trei na kumtengea Raymond) karibu kaka (anamnawisha)
Raymond :( ananawa)
Asante… (Anapakua wali huo kisha
anapakuwa na mboga…halafu anaonja) mmmh!!!Chakula kizuri Sana
Angelina: nimefanya kazi Kwa waarabu kama msichana
wa kazi, walikuwa wananifundisha sana kupika kwahiyo kwenye mapishi niko vizuri
sana
Raymond :( huku
anaendelea kula) vizuri Sana…mi Nina mchumba hajui kupika hata chai
Angelina: labda bado mdogo
Raymond: ana miaka 36…
Angelina :(
anacheka)
Raymond: utamuona…ila sitamuoa…nitakuoa wewe (anacheka)
Angelina :(
anacheka) Mimi???
Raymond: nakutania ila kwani hutaki kuchumbiwa na
mimi?
Angelina: wewe si mchumba wa mtu???
Raymond :( anacheka)
haya bwana sina usemi nakuacha tu...nakutania lakini usije ukaona nakusumbua
Angelina :(
anacheka)
(Raymond anaendelea kula na anaonekana anakifurahia sana chakula kile,
anakula huku Angelina amekaa pembeni yake na wanazungumza na kucheka utasema
walijuana siku nyingi huku ndo wamejuana, wanacheka, wanafurahi maisha kwa
ujumla)
Raymond:
chakula kitamu sana asante (anatabasamu)
0 Comments