SCENE 12: -
(mchana mwingine ulio mtulivu kabisa jua kwa mbali
linawaka na kila mtu anaonekana akiwa na mambo yake. Nyumbani kwa kina Christina,
Christina amekaa na mama zake na kama ilivyo kawaida yao hawana kazi ya kufanya)
Christina: na sisi kwa uvivu tunatia fora (anaguna kidogo) yaani sisi wavivu jamani
(anacheka) sasa hivi kila mtu
anafanya kazi sisi tumekaa jamani (anacheka)
Shangazi: si ndo maana tunataka mabwana matajiri
ili tuishi kama ma malkia
(Wote
wanacheka kimbea)
Christina: na tunataka matajiri kweli...
(Mlango
unagongwa)
Christina: nani tena?
Mama :( anamuita
msichana wa kazi) dada embu kafungue mlango
Christina: yaani wanawake nyie ni wavivu mpaka
kufungua mlango mnaagiza (anacheka)
Shangazi: wewe si upo kwanini usiende kufungua mama
yako kamuita dada?
Mama: si ndo hapo?
Christina: basi yaishe, msije mkanitoa macho bure
loh!!!
Msichana :( anafungua)
(Wazazi wa Raymond wanaingia)
Mama: oh…jamani karibuni
(Wazazi wa Raymond
wanawakaribia)
Shangazi: karibuni sana
Mr na Mrs.Bembele: asanteni (wanakaa)
Mama: Christina kawaletee wageni vinywaji
Christina :( Kwa
heshima) shikamoo baba, shikamoo mama…
Mr na Mrs.Bembele :( wanaitikia)
Christina: mnatumia vinywaji gani
Mr. Bembele: maji tu
Mrs.Bembele: hata Mimi nipe maji tu
Christina :( anajifanya
mstaarabu) sawa (anaenda jikoni na
baada ya muda anarudi na glasi mbili za maji na kuwatengea) karibuni (anaenda kukaa pembeni ya mama na shangazi
yake)
Mr. Bembele :( anakunywa
maji kidogo kisha anarudisha glasi mezani) habari za hapa?
Mama: nzuri tu mkwe za huko kwenu?
Mr. Bembele: salama tu
(Kimya
kinapita Kama vile kila mtu anawaza ya kwake moyoni)
Mr. Bembele: ah… (anavunja ukimya) mimi na mke wangu tumekuja kuwapa taarifa kuwa
wiki ijayo jumatano Raymond na Christina wataenda Dubai kwa ajili ya shopping
ya engagement…na pia kupata mapumziko kidogo…kwahiyo leo ni ijumaa na wiki
ijayo jumatano watakuwa wanaenda tuseme jumanne watakuwa wanaenda dubai kwa
ajili ya shopping hiyo
(Mama,
shangazi pamoja na Christina wanaonekana kufurahi sana)
Mama: Dubai?
Mr. Bembele: ndio Dubai…kwa waarabu (anacheka kidogo)
Shangazi: shopping ya kuvalishana tu Pete ya
uchumba…
Mr. Bembele: ndio...
Mrs.Bembele :( anaonekana
kutofurahishwa hata kidogo na Christina)
Mr. Bembele: sasa Christina utaenda kumwambia Raymond…maana
hata hatujamwambia tumefanya Kama surprise
Christina: sawa daddy haina shida
Mrs.Bembele: mara ya mwisho kumona Raymond ilikuwa
lini?
Christina: wiki iliyopita mama
Mrs.Bembele: na hapo unjiita mke mtarajiwa wa Raymond?
Hujui hata anakula nini nani anamfulia nguo, hujui hata nani anamnyooshea nguo
za kazini nani anamtandikia kitanda eti unajiita mke mtarajiwa (anabenjua midomo kwa dharau)
(Mama na shangazi wanaangaliana chinichini)
Christina: mama, kila nikienda simkuti
Mrs.Bembele: kwani huwa anaondoka na vyombo vya kupikia?
au huwa anatembea na nguo zake
Mr. Bembele: Mama Ray…hawa ni watoto na hairuhusiwi
kukaa pamoja kabla ya ndoa
Mrs.Bembele: hakuna hiyo mbona akitaka hela huwa
anamtafuta popote mpaka anampata? Baba Ray we huoni huyu dada anachopenda kwa Raymond
ni pesa? Yaani mwanangu anahangaika mpaka kaleta msichana wa kazi yaani hana
raha hata kidogo, eti ana mke mtarajiwa loh (anaangalia
pembeni)
Mr. Bembele: hayo ni ya watoto tuwaachie wenyewe
Mrs.Bembele: Mimi ni mama yake Raymond na ninamjua
mwanangu ni wewe ndo unakomaa na hii ndoa itokee, Raymond hataki hata kidogo
Mr. Bembele: Raymond na Christina wanapendana sana
na hilo liko wazi
Mrs.Bembele: nani kakwambia? Yaani Raymond na
Christina wapo tu bora liende baba Raymond…sio Raymond sio Christina hakuna
anayempenda mwenzake huko…hivi wewe tatizo lako huwa hukai na mwanao ukamuuliza
kwa kifupi tu hata mimi simfurahii huyu Christina
Mr. Bembele:(kwa
akina Christina) jamani nisameheni leo sijui kaamkaje unajua sio siku zote
zinakuwa ni jumapili naona kaamka na jipya leo nawaomba radhi kwa hilo jamani
Mama: hata usijali mkwe kuwa na Amani...Baba
Mr. Bembele: sawa… (Kwa Christina) inabidi ukampe ripoti mwenyewe…kamwambie kuwa mna
safari ya kwenda majuu siku ya jumanne Ili ijumaa muwe hapa na sherehe itakuwa
jumamosi
Mrs.Bembele :(
anaguna) tunamtumbukiza mtoto wetu kwenye shimo refu ambalo mwisho wa siku
sijui atakuja kutoka vipi maskini mwanangu
Mr. Bembele: Mama Raymond naomba uwe na adabu
kidogo hii itakupa sifa nzuri kwa wakwe wako hawa watarajiwa
Mrs.Bembele: sitaki kuonekana nina sifa nzuri kwao
maana hata siwataki kabisa mimi…yaani simtaki mimi huyu Christina (ananyanyuka na kuondoka zake)
Mr. Bembele :(
ananyanyuka pia) jamani jitayarisheni na sherehe ya kutoa mahari na pete ya
uchumba atake asitake atake lazima hii ndoa itafanyika mimi ndo baba wa familia
ile kwahiyo msihofu (anatoka)
Mama na shangazi: sawa…hamna shida
(Mr. Bembele anaondoka kuelekea nje na kuungana na mkewe ambao kwa
pamoja wanapanda gari na kuondoka zao, huku ndani Christina na mama zake
wanaendelea na maongezi)
Mama :( anaguna)
yaani mama Raymond hakupendi wewe Christina hata kidogo yaani umemfika kifuaani
mpaka ameamua kuongea mbele ya mume wake…ulimfanyaje?
Christina :(
huku anabenjua midomo) wewe unahisi Mimi Hilo linanipa mawazo? Aende zake
huko (anafyonza) huyu mama anazeeka
vibaya na sura yake mbaya…mi sijawahi kumfanya chochote, Raymond atanioa mimi
na sio mtu mwingine
Shangazi: naomba nicheke (anacheka) maana nimejibana kwa muda Mrefu kucheka (anacheka tena) pamoja na hayo yote
umeona baba mtu anakutetea na kama ni hivyo hatuna shaka lazima hii ndoa
ifanyike bado miezi miwili tu tule wali na wiki ijayo jumamosi pete kidoleni
Mama: ni hatari, hongera mwanangu
Christina: Asante mama
(Wanacheka kimbea)
Mama: Mama Raymond atapata tabu Sana yaani mpaka
namuonea huruma maskini…anahangaika sana eeh
Shangazi Na Christina: sana yaani
Christina: kama kichawi hiki kibibi kizee
(Wanacheka Kwa dharau na kebehi na kumteta
sana mama yake mzazi Raymond)
0 Comments