SCENE 13: -
(Jioni
nyingine Safi kabisa, Christina anafika nyumbani Kwa Raymond
Mlinzi: karibu shemeji
Christina: Asante (anaegesha gari kisha anaelekea ndani kwa Raymond) yupo huyu… (anaelekea ulipo mlango wa kuingilia chumbani
kwa Raymond)
Mlinzi: yupo…
Christina :( anagonga
mlango) hodi…
Angelina :( anafungua)
Christina :( anamuangalia
kwa dharau) wewe ni nani?
Angelina: naitwa Angelina ni msichana wa kazi wa
kaka Raymond…karibu nikusaidie dada…unamtafuta kaka Ray? na nimwambie
anatafutwa na nani?
Christina :( anamfyonza
kisha anaingia) shenzi Sana…wewe hujui Mimi ni nani?
Angelina: dada…sidhani Kama ni ungwana kunitukana
ambapo nimekuuliza kitu kidogo tu…
Raymond :( anakuja
akiwa ametokea jikoni ambapo anaonekana alikuwa anapika)
Christina: wewe dada kwanini umemuachia mume wangu apike?
Raymond: nimetaka mwenyewe kupika na sioni kosa
hapo
Christina: Ray…huyu kinyago ni nani?
Raymond: we koma kabisa kumuita huyu dada kinyago
ana jina huyu (kimya kidogo) anaitwa Angelina…
Angelina: Ni msichana wake wa kazi
Christina: sijakuuliza…
Angelina :( anakaa
kimya)
Christina: mimi naitwa Christina…ni mke mtarajiwa
wa Raymond...Ulitaka kujua, je. Una swali lingine…
Angelina: hapana…sina swali (anaenda jikoni)
Raymond :( Kwa
ukali) we mwanamke unataka nini?
Christina: kwani vipi Raymond?
Raymond: sidhani hata Kama nakutaka tena Christina
Christina: pole Raymond…nimekuja kukupa taarifa kuwa
wiki ijayo kwenye jumatano hivi tutakuwa tunaenda Dubai Kwa ajili ya shopping ya
engagement party…yetu
Raymond: ah...Wapi...Mbona sina taarifa juu ya
Hilo?
Christina: ndo nimekupa sasa hivi…baba Na mama yako
walikuja kuniambia wakaniambia nije mwenyewe kukuambia kuwa tuna safari honey
ya kwenda Dubai
Raymond: siendi na wala sitaki
Christina :( anacheka)
Raymond: kwanini una roho ya hivyo we mwanamke?
Christina: ipoje…
Raymond :(
anampigia mama yake, simu inaita kisha inapokelewa) mama…shikamoo?
Mrs.Bembele: marahaba baba…vipi?
Raymond: mbona hamkuniambia kuwa natakiwa nisafiri
kwenda nje? Hamjui kuwa nina ratiba zangu?
Mrs.Bembele: samahani mwanangu…ni baba yako ndo
aliamua hayo yote
Raymond: bwana muwe mnaniuliza kuhusu hivi vitu…sio
mnajipangia...Tu nishakuwa mtu mzima na sio mtoto mdogo bwana…
Mrs.Bembele: usikae unagombana na baba yako…we
msikilize tu si unajua alivyo? We kuwa mpole mwanangu…nakupenda sana mwanangu…najua
huyo mwanamke humtaki tena ila sasa baba yako keshaamua…kuwa tu kama wahindi
kwamba umepangiwa kuoa mtu Fulani kuwa mpole na umuoe tu…
Raymond :( anakata
simu kwa hasira)
Christina :( anacheka)
Raymond: yaani Christina…nakuchukia Sana
Christina: wewe vipi…kwani Mimi ndo niliamua hili
si umchukie baba yako?
Raymond: I hate you so much; you are ruining my
life…
Christina :(
anacheka)
Raymond :(
anaenda zake chumbani)
Christina :(
anamfuata) Raymond
Raymond: naomba uniache
Christina :( anajikuta
anajishusha) nisamehe mpenzi kama kuna sehemu nimekuudhi!!Nilikuwa
nakutania tu jamani, nisamehe Sana mpenzi wangu Maana nimekuona umechukia sana
Raymond: (anashusha
hasira) sijachukia na wala sina sababu ya kuchukia sema tu hawa wazazi
wangu wamenifanyia kitu ambacho sijakipenda na ndo maana umeona nipo hivi ila
usijali sijachukia kuwa na Amani,na kwa kuwa wameshaamua hiyo safari basi sina
jinsi Zaidi y kutii walichokipanga
Christina: oh…my love (anamkumbatia) nakupenda na sitaki tuwe tunagombana kizembe baby
Raymond :( anaonyesha
kutotaka kumkumbatia pia) ok …it is okay
Christina :( anaanza
kujidekeza) leo nalala huku kwako na sio leo tu…mpaka siku tunasafiri
Raymond: hiyo itakuwa ni kukaa pamoja na bado hatujaruhusiwa kuishi pamoja
Christina: sitaki kukukera baby…so sawa nitalala Leo
then kesho nitaondoka
Raymond: sawa…
(Mlango
unagongwa)
Christina :( anafungua
mlango anakuta ni Angelina) nini?
Angelina: chakula tayari
Christina: mbona mapema Sana?
Raymond :( anatokea
kwa nyuma yake) ndo tamaduni ya nyumba yangu…kwahiyo ni vyema wote
tukaifata… (Anaelekea nje) Angel…njoo
Angelina :( anamfuata)
abee kaka
Raymond: umeshatenga chakula?
Angelina: ndio kaka…karibuni mezani
(Raymond na
Christina wanaelekea mezani)
Angelina :(
Simu yake inaita, anatoka pembeni na kuipokea)
Christina :( anaishangaa
ile simu) yaani kijakazi ana simu nzuri Kama ya boss wake
Raymond: kwani kuna ubaya gani jamani?
Christina: hakuna ubaya halafu mbona Kama vile unamtetea
Sana huyu dada umeshalala nae?
Raymond :( anajikuta
anakasirika Sana) unadhani Mimi ni msaliti kama wewe? (Anakasirika Sana)
Christina: okay tusianze ugomvi, tule
Christina: badilika wewe mwanamke…
Christina :( anapakua
chakula kisha anaanza kula)
Raymond :(
kimya)
Christina: halafu mbona hukuniambia kuwa umempata
msichana wa kazi?
Raymond: sikuona haja ya kukuambia…
Christina :( anaguna)
hayo majibu yako siku hizi
Raymond: yamefanya nini? Au unataka nikujibuje wewe
mwanamke?
Christina: Ray, unataka kuachana na mimi? Unajua
sikuelewi kabisa
Raymond: honestly yes…ila kwa kuwa ndo ishapangwa
kuwa ni lazima nikuoe sina jinsi bali kuwa mpole tu unadhani nitafanyaje mimi?
Christina :(
anaguna halafu anakaa kimya)
Raymond: Ina maana kati yetu upendo umeisha
kabisa…kwani hilo hulioni?
Christina: lakini wazazi wamepanga mimi na wewe
tuoane no matter what wenyewe hawataki kusikia kuwa sijui upendo umeisha kati
yetu…tufunge tu ndo Ray…najua upendo utarudi kati yetu
Raymond :(
kimya huku anaendelea kula chakula chake)
Christina: basi afadhali unijibu chochote Raymond…
Raymond: He!!!Wewe dada vipi?
Christina: naomba unijibu tu jamani!!
Raymond: sina cha kukujibu…endelea kula
(Angelina
anarudi mara baada ya kumaliza kuongea na simu kuongea na simu)
Raymond :( huku
anatabasamu) naona shemeji alikuweka sana maana si kwa kuongea huko
Angelina: hapana kaka ni mama yangu…anakusalimia
sana…
Raymond :( anaachia
tabasamu) Asante, anaendeleaje?
Angelina :( anatabasamu)
anaendelea vizuri tu
Christina :( anabenjua
midomo) kwahiyo wengine ni kugombana tu lakini kijakazi anachekewa basi
sawa
(Raymond na Angelina wanakaa kimya)
Christina :( ananyanyuka)
nimeshiba…asanteni kwa chakula... (Anaingia
ndani kwa hasira)
Angelina: wifi mkali kweli
Raymond: achana nae… (Anavuta kiti) kaa ule chakula
Angelina: we unataka nitolewe masikio kwa jinsi
wifi alivyo mkali siwezi hata kuthubutu kukaa na wewe, mi naenda kula jikoni (anaenda jikoni)
Raymond :(
anabeba sahani yake na kumfuata jikoni)
Angelina: kaka vipi?
Raymond: mi nataka nikae na wewe kama hautajali
(wanakaa
kula, wanaonekana kufurahia maana wanaongea mambo mbalimbali, wanacheka na kila
kitu kinaonekana kipo vizuri kati yao…wanaendelea kula na kucheka sana na mtu
kama ungewakuta ungejua ni mtu na mpenzi wake au mtu na mtu wake wa karibu sana
maana wanaonekana kuridhiana na kupendana pia)
Raymond:
wewe mpole sana hadi raha (anatabasamu)
0 Comments