SCENE 14: -
(jumapili
nyingine kama ilivyo kawaida ya kila jumampili kwamba Raymond haendi kazini
anakuwa nyumbani kwa ajili ya mapumziko, hivyo amekaa bustanini kwake, hewa
inaonekana ni nzuri na mazingira ya nyumba ile iko sawa kabisa,na yote hiyo ni
shukrani kwa Angelina,binti wa kazi na kipenzi cha siri cha Raymond .,Angelina
yupo getini na Ramadhani na wanaonekana kubadilishana mawazo ikiwemo na
kufurahia pamoja,Raymond yupo bustanini lakini anaonekana kuwa amemkubuka sana,Angelina
kwahiyo anamtafuta)
Raymond :(
anaita) Angelina…
(Angelina yupo Kwa mlinzi na wala hana wazo kama anatafutwa na bosi
wake)
Raymond: Angel…
(Kimya)
Raymond:(anaamua
kunyanyuka)huyu Mrembo yuko wapi jamani?(anaelekea kwa mlinzi ili amuulize,anakuta Angelina hana habari na
anacheka mno kitendo kinachompa hasira na wivu,ukiangalia anamfahamu Ramadhani
kwa uhuni)dah…mbona wanafurahiana hivi au Ramadhani keshanitangulia?...Dah!!!haiwezekani
Angelina ni wangu,na atakuwa wangu…(anajishangaa)mbona
nimewaka na wivu hivi,nakuwa kama Angelina keshakuwa mpenzi wangu yaani nashangaza
hata nikimwambia Edmond kuwa nampenda Angelina ila bado sijamtamkia na ninaona
wivu kila nikimkuta kakaa na mwanaume mwingine najawa na wivu
atanishangaa…hivyo basi natakiwa nijitahidi sana kutoonyesha udhaifu wowote(anamuita Angelina)Angelina…
Angelina :(
ndo anashtuka sasa) abeee kaka…
Raymond: hivi umeshapika?
Angelina: kaka sasa hivi bado asubuhi Sana na pia
tumetoka kunywa chai muda si Mrefu…ila kama unataka kuniagiza sokoni ni sawa tu
kaka
Ramadhani: yeye ndo bosi
Angelina: eeeh… (Anacheka)
Ramadhani :(
anacheka pia)
Raymond :( anajikuta
anachukia bila sababu ya msingi) naona mnafurahiana Sana eeh
Ramadhani: lazima tufurahiane bosi… (Anamshika Angelina bega) huwezi jua bosi
labda kanaweza kakawa ka shemeji kako…kabinti spesho
Raymond :( anazidi
kupandwa hasira na wivu) unamaanisha tayari umeshammiliki? (Anamuangalia Angelina ambae muda wote
anaonekana kucheka kwani ana kuchukulia utani)
Ramadhani: sijammiliki ila nikitaka naweza…sekunde tu
Raymond :( anapatwa
na wivu anatamani hata kumrukia Ramadhani ambae muda wote huo anaongea anadhani
wanataniana kumbe mwenzie anaumia sana kutokana kuwa amempenda Angelina kwa
dhati na hataki kumpoteza) hongera…yako...
Ramadhani :( anacheka)
Asante boss…
Raymond :(
anataka kuondoka)
Angelina: kaka huyu anatania wala usimchukulie Sana,
ni utoto ndo unamsumbua
Raymond:(anashusha
pumzi mithili ya mtu aliyechoka sana) sawa…toka hapo uende sokoni na pia
wewe si wa kukaa getini Angelina wewe ni wa kukaa ndani…kuna kila kitu kuna tv
na pia nimekununulia simu nzuri, ukikosa wa kuongea nae uwe unaongea na mimi
kwenye simu
(Ramadhani na Angelina wanabaki wanamshangaa)
Raymond: natania Kama mlivyonitania…
(Wote wanacheka)
Ramadhani: si ndo nikaanza kuwaza yamekuwa hayo
jamani?
Raymond: hata msinijali sana ndugu zangu…ok Angelina,
nenda sokoni uje nikusaidie kupika (anatabasamu)
Angelina
:( anatabasamu) sawa kaka (haraka anaingia ndani kuchukua kikapu cha
sokoni na kuondoka zake)
Raymond
:( Kwa Ramadhani) na wewe punguza bwana
yaani mtoto wa watu kaja juzi tu leo unamtaka, kila saa unamuita huku
Ramadhani
:( huku anacheka) ushamtamani Mtoto
wa watu nini?
Raymond:
hamna wewe…ni msichana wangu wa kazi atabaki kuwa mdogo wangu na isitoshe nina
mchumba hata wewe unajua
Ramadhani:
yule mnaegombana nae kila mkikutana? (Anacheka
Sana) mwanamke kiwingu yule…Duh
Raymond:
ndo hivyo, sasa unadhani nitafanyaje Kama ndo alitolewa kwenye ubavu
wangu…nitapingana na mipango ya Mungu?
Ramadhani:
duh…Kama Mungu alikupangia yeye ndo awe Hawa wako rafiki yangu kazi unayo…
Raymond
:( anacheka kidogo) sasa unadhani
nitafanyaje?
Ramadhani:
tafuta chombo kipya…wewe kaka una hela zako
Raymond:
Kama Angelina hivi
Ramadhani:
si umesema ni mdogo wako huyo?
Raymond:
mfano tu
Ramadhani:
eeh…katoto kadogo dogo kana heshima zake
Raymond:
sawa nitafanya mpango…
Ramadhani:
hapo sawa, ila sasa sio Angelina maana nishampangia
Raymond
:( anajikuta tena anakasirika) …achana
na Angelina bwana tuongee mada nyingine bwana
Ramadhani:
poa hamna noma au umempenda Angelina tunazugiana tu hapa?
Raymond:
hamna…halafu Jumatano au jumanne nasafiri naenda Dubai narudi, ijumaa, jumamosi
namvalisha Pete ya uchumba Christina...
Ramadhani:
yaani unamvalisha Pete huku unaona kabisa hamna maelewano?
Raymond:
nitafanyaje ndo baba kapanga kwahiyo sio umbake Angelina huku nyuma nitakutoa
masikio
Ramadhani:
wewe Angelina ameshakuteka wewe (anacheka)
Raymond
:( huku anatabasamu) hamna ni dogo tu
Fulani…hamna jipya
Ramadhani:
haya bwana yetu macho, tutakuja kusikia tu si tupo (anacheka)
Raymond:
hamna (huku anaingia ndani)
Ramadhani:
angalia huyo unaetaka kumvalisha Pete asije akatutoa wote masikio
Raymond
:( anacheka) mtajijua wenyewe…
Ramadhani
:( anaingia kibandani kwake)
Raymond:(anajisemea moyoni)I
love Angelina so much mpaka siwezi tena kuficha hizi hisia…nampenda,tangu
nimemuona nimeshindwa kufuta picha yake kichwani mwangu…nampenda…and I wish to
make her my wife(anajitupa kwenye sofa
kama mzigo)Raymond weds Angelina…hiyo siku will be the happiest day of my
life…(anajichekea mwenyewe)lakini
mimi mjinga ee…Angelina si mdogo wangu huyu jamani mbona nataka kutia aibu
mimi…lakini hamna kwani tumezaliwa tumbo moja…sio mdogo wangu ni mwanamke wa
ndoto zangu…I will marry her…yes I will marry her(anajishangaa tena)hivi mimi nina akili kweli jamani?(anajicheka sana)oh Angelina…iam going to
make you my wife…oh my God…I cant wait to be your husband..Na ulivyo shapu
unaweza ukawa unakuja kunifungulia geti wewe yaani dah…eeh Mungu nisikie na
umfanye Angelina awe wangu jamani (anacheka
peke yake)
Angelina: kaka tunapika nini?
Raymond: chochote maza hausi…wewe ndo mmiliki wa himaya yangu
Angelina :( anashangaa Sana) nini?
Raymond: nini kwani?
Angelina: umesema maza hausi?
Raymond: nakutania (anacheka)
pika chochote (anacheka sana)
Angelina: kaka bwana... (anacheka
sana)
0 Comments