SCENE 15: -
JUMANNE SIKU YA SAFARI YA DUBAI: -
(alfajiri na mapema Raymond na Christina wanatoa mabegi nje ili kuelekea
uwanja wa ndege kwa ajili ya kuanza safari yao ya kwenda Dubai, lakini kabla ya
kuondoka, Raymond anaona ni vyema kumuamsha Angelina na kumuaga. hivyo anaenda
mpaka mlangoni kwa Angelina na kugonga mlango)
Raymond: Angel…
Christina: mi nashindwa kuelewa kwanini unamuamsha
huyo tunachelewa bwana…
Raymond: Ni lazima nimuone Angelina, sitaondoka
bila kumuona
Christina :(
anashangaa) unamaana gani kusema kuwa huwezi kuondoka bila kumuona
Raymond :( anajishtukia
kuwa ameropoka) Ni msichana wangu wa kazi ni muhimu nimuone ili nimpe
maelekezo maana hatutakuwepo mpaka ijumaa
Christina: halafu mbona unamuacha peke yake kwanini
asiende kukaa hata kwa yule mke wa Edmond mpaka tutakaporudi? Mi siwaamini hawa
wasichana tutakuta kila kitu kimebebwa humu ndani
Raymond :( anatikisa
kichwa huku anaendelea kugonga mlango)
Angelina :(
anafungua mlango)
Christina: eti ndo kajifanya kuamka sasa hivi
unatuchelewesha bwana (anaangalia
pembeni)
Raymond: just whats wrong with you Christina,
kwanini unakuwa na roho ya hasira kiasi hiki?
Christina: stop judging Na ufanye haraka mi
nakusubiri kwenye gari (anampokonya
funguo na kuondoka zake)
Angelina: shikamoo kaka…
Raymond: marahaba mdogo wangu (anaachia tabasamu) yaani wewe mzuri hata ukiwa umetoka usingizini…
Angelina :( anacheka
kidogo) kaka bwana umeanza utani wako…
Raymond :(
moyoni) nakupenda Sana Angelina, I swear natamani nisiende hii safari
nibaki na wewe hapa tukae tu tufurahi na kadhalika…
Angelina: kaka umeniamsha…
Raymond: ndio mdogo wangu…Mimi nasafiri naenda Dubai
nitarudi ijumaa nadhani usiku kitu Kama hicho naomba uniangalizie nyumba yangu
nadhani Edmond na Catherine watakuwa wanakuja mara kwa mara kwahiyo usiogope
sawa mama
Angelina: sawa kaka nakutakia safari njema
Raymond: naomba nikukumbatie, Kama kaka yako
tafadhali Ili safari yangu iwe salama
Angelina: wifi akiingia ghafla italeta picha
mbaya…we nenda tu kaka mi nakutakia safari njema kaka
Raymond: sawa, mi naenda…ila ilikuwa tu kiheshima
maana tumekuwa pamoja Mimi na wewe na tunaheshimiana nipe tu nafasi
nikukumbatie ili nipate mema huko napoenda
Angelina :( anamkumbatia)
Raymond :( anamkumbatia
pia) Asante Angelina yaani hujui kumbatio lako limenipaje furaha na faraja
si umeona wifi yako alianza kunitibua…
Angelina: nenda sasa kaka, wifi anakusubiri…
Raymond :(
huku anaondoka) sawa tutaonana ijumaa nikuletee zawadi gani kutoka huko?
Angelina: yoyote…
Raymond: poa… (Anatoka
nje) Angelina my love, my housegirl, I really love you my darling
Christina: Raymond…tunaenda au hatuendi?
Raymond: hatuendi… (Anataka kurudi ndani)
Christina: ngoja nimpigie baba yako simu…sijui
yaani sijui umekuwaje wewe mwanaume?
Raymond :(
anapanda gari kimya bila kuongea chochote)
Christina: kiboko yako ni baba yako tu…
Raymond :(
kimya)
Christina :( anaanza
kuendesha gari na kuliondoa mahala pale) sasa nani atalirudisha gari
nyumbani?
Raymond :(
anamuangalia bila kusema kitu)
Christina: mbona husemi kitu unaniangalia tu jamani,
mbona umekuwa hivyo hukuwa hivyo…
Raymond :( anajisemea
moyoni) hivi ingekuwaje Kama Angelina au mwanamke kama Angelina angekuwa
ndo mtarajiwa wangu I swear hiyo raha ambayo ingekuwa moyoni mwangu ingekuwa
sio ya kifani…
Christina: una dharau siku hizi sijui kwanini...Yaani
unanikera…
Raymond: jamani huko airport hatufiki…please sitaki
kugombana na wewe sina hiyo nguvu tafadhali (anawasha redio iliyopo kwenye gari)
Christina: okay sitakusemesha maana naona unakereka
Sana mpaka naogopa kweli
Raymond: afadhali…
(wanaendelea na safari huku kila mmoja wao anaonekana kuwaza mawazo yake
mwenyewe, baada ya dakika kadhaa wanafika uwanja wa ndege, wanaposhuka kutoka
kwenye gari Raymond anabeba begi lake na bila kujali anaingia ndani na kumuacha
Christina peke yake anahangaika na kuegesha gari. anapokuwa ndani Raymond
anaona ni bora tu, ampigie kipenzi chake simu inaita mwisho inapokelewa) nambie bado umelala
Angelina: nimeshaamka mbona tangu uliponiamsha kaka
Raymond: niite tu Raymond nitafurahi sana ukiniita Raymond...
Angelina: sawa Raymond…
Raymond: Safi kabisa mdogo wangu…
Angelina: Na wewe niite Angelina…
Raymond: sawa malaika…
Angelina :( anacheka
kidogo) mmeshafika?
Raymond: ndio tumefika uwanja wa ndege nitakupigia
tena nikifika Dubai…
Angelina: sawa Raymond…
Raymond: baadae… (Anakata simu)
Christina: kwahiyo ukaona kunisaidia kupaki gari
nitafaidi Sana…
Raymond :( kimya
huku anaendelea kutembea kuelekea ndani)
Christina :( anatikisa
kichwa) sasa si Kama hukutaka kwenda Dubai si ungesema tangu siku nakuletea
habari?
Raymond: unataka nirudi nyumbani maana nakuona
unaongea tu…. huchoki kuongea jamani we mwanamke? Tangu Jana usiku unaongea
tu…nimechoka kusikia malalamiko yako bwana
Christina :( anaamua
kukaa kimya)
Raymond: Na ndio sikutaka kwenda Dubai wala
wapi…nataka kukaa hapa nchini nikiendelea na kazi na maisha yangu…wewe na baba
mmekomaa kweli kwenda huko Dubai
Christina: umekuwaje wewe
Raymond :( moyoni)
Mimi mwenyewe najishangaa yaani nasikia tu hasira tu ya kwenda huko Dubai
Christina: sikuelewi…Raymond kwani kuna shida gani?
Raymond :(
kimya)
Christin: unajua tumekaa muda Mrefu Sana hatuna
maelewano hii safari itatuleta pamoja au wewe unaonaje?
Raymond :(
kimya)
Christina :(
anamsogelea na kumbusu shavuni)
Raymond :(
anageukia pembeni)
Christina :( anamuona
hayuko sawa) baby are you okay?
Raymond :(
kimya)
Christina: talk to me jamani
Raymond :(
kimya)
Christina: baby… (Anajaribu kumgeuzia upande wake) basi kama hutaki
0 Comments