SCENE 16: -
(Jioni nyingine ya siku ya ijumaa, Edmond na wazazi wa Raymond wamekaa
uwanja wa ndege wakiwasubiri Raymond na Christina wawasili)
Edmond :( anaguna)
mmmh…wamechelewa
Mr. Bembele :( anamuangalia
kwa dharau) wewe unajua nini wewe? Hata ndege umeshawahi kupanda kweli
wewe?
Edmond :(
kimya)
Mrs.Bembele: jamani mume wangu maneno gani hayo?
Kwanini unamdharau Mtoto wa watu?
Mr. Bembele: Na wewe mke wangu…kwani hapo
nimesemaje?
Edmond :(
kimya)
Mrs.Bembele: basi tufanye yameisha baba
(Raymond Na
Christina wanawafika walipokuwa)
Raymond: hello…mambo zenu
Edmond: oh… (Anamkumbatia)
Mr. Bembele: kwahiyo Mimi baba yako na uzee wangu
nimejikongoja weee mpaka nimekuja kukupokea hujaniona umemuona tu huyo Mond
mwenzio si ndio?
Raymond: dad…please…
Mrs.Bembele: sidhani hapo kuna tatizo baba Raymond…tafadhali
msianze ugomvi hapa mbele za watu ni aibu jamani
Christina :( anatabasamu)
shikamoo baba…
Mr. Bembele: marahaba mwanangu za Dubai? Did you
enjoy?
Christina: Sana dad...Asante… (Anaachia tabasamu)
Mr. Bembele: usijali…nitafanya chochote
kukufurahisha mkwe wangu…
Raymond :( anatikisa
kichwa ishara ya kutokubaliana na neno mkwe)
Edmond :( Kwa
Raymond) enhe…Mond nambie
Raymond: ah…fresh…tu mapya?
Mr. Bembele: bado tu umemuona huyo rafiki yako?
Mrs.Bembele: shida nini baba Raymond…Mimi mbona
hajanisalimia?
Raymond: let’s get out of here!!!Itakuwa msala sasa
hivi…
(Wanatoka nje na kuelekea kwenye gari kubwa waliokuja nalo kina Mr.
Bembele na mkewe)
Edmond :(
anataka kupanda kwenye gari)
Mr. Bembele: (kwa
Edmond) wewe Mtoto huruhusiwi kupanda hili gari…nakuchukia Sana maana wewe
ndo chanzo cha mimi na mwanangu kugombana kila mara…
Edmond :( Kwa
upole anashuka na kujiweka pembeni)
Raymond :( Kwa
kuwa na yeye alikuwa amekwisha panda gari anashuka) huu ni unyama
uliokithiri…sitaruhusu usimfanyie haya rafiki yangu eti kisa nini…kwamba
anatoka katika familia ya kimaskini?
Mr. Bembele: umaskini ni laana wewe Mtoto elewa…
Raymond: hata Kama hata wao ni watu…na huwezi
kunipangia nimpende nani naweza hata nikaoa mwanamke maskini
Mr. Bembele :( anacheka
Kwa kejeli) unamuoa Christina na si mwanamke maskini…utake usitake utamuoa
Christina
Christina :(
anachekelea moyoni)
Raymond: sio lazima…kumuoa Christina
Mrs.Bembele :( anagundua
Christina anaufurahia ugomvi huu) tafadhali acheni kugombana for heavens
sake mnawafurahisha na maadui ambao hawana mapenzi mema na hii familia
Mr. Bembele: Kama nani?
Mrs.Bembele :( Kwa
ujasiri) Kama Christina
Christina: Mama Mimi tena?
Mrs.Bembele: unaweza kuniambia unachekea nini?
Christina: sijacheka mama… (anajifanya mpole) unanichukia ndio nakubali ila kitendo cha kuona
kila nachofanya ni kosa…kwakweli sikubali…
Mr. Bembele :(
Kwa mkewe) mama Raymond muombe msamaha mkwe wako mara moja na nimesema…mimi
mume wako…
Christina :(
anajisemea moyoni) tuone sasa utafanyaje wewe bibi kizee mshenzi usie na
akili…
Mrs.Bembele :( anamgeukia
Christina) nisa…
Raymond :(
anamkatisha mama yake) No…never, kwani umemkosea nini?
Mr. Bembele: Raymond…usiingilie maamuzi
yangu…niheshimu...Mimi ni baba yako na nimekupa kila kitu
Raymond :( anamuangalia
usoni) kwahiyo dad…ulinipa kila kitu ili uniamuru chochote tu…na sio kwa
upendo?
Mr. Bembele: sijamaanisha hivyo baba (anapoa)
Raymond: Kama ulinipa Ili unifanye chochote
dad…nakurudishia kila kitu na itakuwa ni vizuri maana hata kumuoa Christina
sitamuoa tena…
Mr. Bembele: mwanangu umenielewa vibaya
baba…nimekupa Kwa upendo kabisa
Raymond: mama, Edmond…tuondoke zetu, sisi hapa ni
maskini na hatuna hadhi ya kusimama na Mr. Bembele
Mr. Bembele: no son, sio hivyo baba yangu jamani
basi nisamehe Mimi mwanangu
Raymond :(
anaita taksi) navirudisha vyote (Kwa
mama yake na Edmond) twendeni… (Anapanda
kwenye gari)
(Mrs.Bembele na Edmond wanapanda kwenye gari na kuondoka zao)
Mr. Bembele: shit!!!nimefanya nini mimi jamani? Nimegombana
na mwanangu tena!!! Hii imeshakuwa ni tatizo
Christina: mwanao ana kiburi tu…muache akitulia
atarudi tu kuomba msamaha
Mr. Bembele: Raymond ni mwanangu wa pekee na
ninamfahamu vizuri sana akiamua kitu kaamua… (Anampigia simu Raymond inaita Sana mwisho inakata) hapokei (anasikitika)
(Upande alipo Raymond, Edmond na Mrs.Bembele)
Mrs.Bembele: usiwe na hasira baba msamehe baba
yako…
Raymond: siwezi…atanisumbua sana eti kisa alinipa
nyumba, gari, na kazi ndo anipe na mwanamke na rafiki pia?
Edmond: take it easy...
Raymond :(
anatulia kidogo) by the way…kuna jambo nataka kuwaambia…
Mrs.Bembele: au ndo sababu ya kutuleta humu?
Raymond: no dad…kaniboa…anyway nataka tu kutumia
hii nafasi ya kuwaambia yangu ya moyoni…
Edmond: tuambie…tunataka kusikia? Christina ana
mimba?
Raymond: no… (Kimya
kidogo) sijui mtalipokeaje ila ni lazima niwaambie…
Mrs.Bembele: enhe… (Anaonekana ana shauku Sana)
Raymond: IAM IN LOVE WITH MY HOUSEGIRL
Edmond Na Mrs.Bembele :( wanakuwa Kama wamegandishwa maana wanashangaa sana)
Raymond…. yes, nampenda…Sana Angelina…I feel she is
right for me…
Edmond: yaani Raymond
Raymond: naelewa unachotaka kusema kuwa ni shemeji
yako na kwamba nimemchezea…au nilikuwa na nia hiyo…jamani ilikuja tu tangu siku
ya kwanza namuona…it was love at first sight…yaani nilipomuona tu…I swear
nikampenda na haikuwa nia yangu kwamba Edmond akiniletea mwanamke mimi
nitamfanya awe wangu…imetokea tu
Edmond: wala hiyo haina shida…nataka kukuambia
kesho unamvalisha Pete Christina…
Raymond: I swear akili yangu haifanyi kazi
nachotaka tu ni kukimbia nyumbani na kumzawadia Angel…hizi zawadi na kumwambia
kila kitu…kuwa nampenda nataka awe mke wangu
Mrs.Bembele: sasa baba…usiache kesho kumvalisha Pete
huyo mwanamke…fanya hayo kwa kumtunzia baba yako heshima yake…sawa baba ee
tumeshaalika watu baba naomba uelewe hilo sawa ee
Raymond: sawa mama…naelewa
0 Comments