IAM IN LOVE WITH MY HOUSEGIRL 17

 


SCENE 17: -

(Majira ya saa NNE usiku siku hiyohiyo ambayo Raymond na Christina wamerudi kutoka Dubai, Angelina anaingaia chumbani kwake mara baada ya kumaliza kazi zake za kila siku)

Angelina: bora kaka Ray karudi maana mmh…hili jumba lilivyo kubwa yaani nilikuwa naogopa kulala peke yangu(anaangalia kitandani anaona gauni zuri sanai)hili gauni limefikaje hapa na nani kalileta?(analinyanyua,kikaratasi kidogo kinaanguka,anainama kukiokota)hiki kinasema…vaa gauni hilo na viatu viko chini ya uvungu na unifuate bustanini…(anaguna)nani huyu kaniandikia ujumbe(anainama kuangalia chini ya uvungu anakutana na viatu vizuri na vya thamani…anavaa gauni kisha anavaa viatu anapaka poda kidogo kisha anatoka kwenda bustanini,baada ya hatua chache anafika bustanini)wewe ni nani…asante kwa zawadi nzuri ya viatu na gauni..

Mtu :( anageuka taratibu na mwisho anajionyesha sura ni Raymond) ni mimi…Angelina...

Angelina :( anashangaa Sana) kaka Raymond?

Raymond: Angelina…

Angelina: Asante kwa gauni zuri kaka yangu yaani una roho ya pekee halafu ile hela uliyonipa nimewatumia nyumbani nimewaambia wafungue ka biashara wameshukuru sana

(Sehemu hiyo imepambwa Kwa Maua mazuri sana na kuna utulivu wa hali ya juu)

Raymond :( anatabasamu) usijali

Angelina: haya kaka…gauni zuri kweli halafu kumbe kuna sehemu nyingine ya bustani pazuri hivi…sikuwahi kujua

Raymond :( anamkaribia na kumshika mkono) nakupenda Angelina…nakupenda sana, nilitaka nisikuambie chochote ila nimeshindwa, nakuhitaji sana katika maisha yangu

Angelina :( anamshangaa Sana) kaka yangu…kivipi tena kaka

Raymond: kimapenzi… (Anamshika mkono) tangu nakuona kwa mara ya kwanza kabisa moyo wangu umekubali na kujiridhisha kwamba ni wewe ndo nataka uwe mke wangu (anamshika mikono yote miwili)

Angelina:(anamsukuma) hapana…siwezi wewe ni mume wa mtu, na pia hata hatuendani maana wewe ni tajiri sana siwezi hata siku moja nikafanya ujinga wa kuwa na wewe kimapenzi huku najua unaenda kuwa mume wa mtu…tafadhali naomba uendelee kuniheshimu kama mdogo wako…na pia umeona unaweza kuninunua kwa gauni na viatu kweli watu matajiri mna dharau sana

Raymond: sio hivyo…nilitaka upendeze tu kisha nikuambie yaliyo moyoni mwangu nakupenda Sana hata Catherine na Edmond hata mama yangu wanajua na wapo tayari kuwa na sisi katika safari yetu mpya tafadhali nipe nafasi mpenzi wangu na hakika nitakutunza

Angelina: wewe ni mume mtarajiwa wa mtu…kesho tu unaenda kumvalisha pete ya uchumba mchumba wako…mimi sitaki matatizo na mchumba wako, unamjua alivyo

Raymond: Mimi na yeye hatuna upendo yaani hatupendani…yeye ana mwanaume anayempenda na mimi nina wewe…naapa mbele za Mungu  kuwa nakupenda sana, embu naomba unielewe Angel…tafadhali

Angelina (anaanza kumuelewa) sasa vipi kuhusu baba yako atakubali Mimi kuwa na wewe

Raymond: haijarishi nitakulinda siku zote za maisha yangu… (Anamshika mikono yake) nakupenda (anambusu kwenye paji la uso)

Angelina: lakini Mimi sitaki kubeba mimba sasa hivi…

Raymond :( anacheka) nani amekuambia kuwa ukishikwa na mwanaume tu au akikubusu unabeba mimba…usijali nitakulinda na sitakuchezea…nitakuoa…umesikia ee (anacheka) yaani wewe

Angelina: sawa

Raymond :( anatabasamu) kwahiyo unamaanisha kuwa…

Angelina: nimekukubali…utakuwa mpenzi wangu

Raymond: na baadae mumeo… (Anacheka)

Angelina :( anacheka pia) ndio…

Raymond :( anambeba) asante Angelina hujui nimeisubiri hii siku muda gani tangu umekuja nimekufungulia mlango siku ile unaletwa na Edmond…nilipokuona tu nafsi yangu ilikubali kuwa wewe ndo wangu wa maisha

Angelina :( anacheka) umefurahi Sana?

Raymond :( huku anakaa) nimefurahi (anamsogelea)

Angelina: Ramadhan atatuona…

Raymond: sijali…hata akija Christina sasa hivi na kutushuhudia kuwa sitajali (anampigia mama yake simu)

(simu ya mama yake inaita)

Mrs.Bemebele :( anashtuliwa na mlio wa simu anafikicha macho) nani tena usiku huu? (Anaangalia simu anakuta ni Raymond) na wewe usiku wote huu una yapi?

Raymond: amenikubali… (Anatabasamu)

Mrs.Bembele: kweli??(Anatabasamu) hongera mwanangu…

Raymond :( anampa Angelina) ongea na mama

Mrs.Bembele :( anatoka kitandani na kwenda jikoni)

Angelina: shikamoo mama...

Mrs.Bembele: marahaba mwanangu…Asante Kwa kumpa furaha huyo kijana

Angelina :( anacheka)

Mrs.Bembele: laleni kesho ni siku ngumu hasa kwako ila elewa kuwa mwenzio anakupenda sana...imetokea tu inambidi atimize hilo ili yasiwe makubwa kwa baba yake si unaelewa?

Angelina: naelewa mama

Raymond :( anatabasamu)

Mrs.Bembele: nakata simu, nasikia baba yenu ananifuata (anakata simu kisha anafungua friji na kutoa maji na kuanza kunywa)

Mr. Bembele: mna nini cha siri na Raymond?

Mrs.Bembele: umejuaje kuwa naongea na Ray?

Mr. Bembele: nimehisi tu...au unaongea na mwanaume mwingine mama Ray?

Mrs.Bembele: hapana baby...

Mr. Bembele: enhe mlikuwa mnaongea nini na Raymond?

Mrs.Bembele: kanipigia simu kaniambia kuwa hawezi kulala maana anawaza Sana sijui kesho itakuwaje

Mr. Bembele: wala asijali sana kila kitu kitakuwa sawa tu

Mrs.Bembele: nimemwambia pia… (Anachukua jagi la maji kisha anaondoka)

Mr. Bembele :( anajisemea moyoni) kuna jambo lingine tofauti hapo…unavyomchukia Christina… (Anaguna kisha anamfuta mkewe chumbani kwao)

(Upande wa Raymond na Angelina)

Raymond: mama amekufurahia Sana…unaona sasa hatutakuwa na shida

Angelina: mama ni mcheshi

Raymond: na ni mpenda watu wa rika zote na tabaka mbalimbali

Angelina :( anapiga miayo)

Raymond: usingizi…

Angelina: Sana…

Raymond: twende…nikusindikize chumbani kwako ukalale… (anatabasamu kidogo)

Angelina: (anaguna)

Raymond: kuwa na amani wala sitafanya chochote kinyume na matakwa yako…

(Wanaenda moja kwa moja mpaka chumbani kwa Angelina)

Angelina: Raymond…

Raymond: usiogope, siwezi kufanya chochote usichokitaka…kuwa na Amani nadhani nimeshakuambia

Angelina: Asante…

(Angelina anapanda kitandani wakati huo Raymond kasimama pembeni ya kitanda, anamfunika kisha anamuwekea neti vizuri)

Angelina: nenda kalale maana kesho ni siku kubwa kwako

Raymond: natamani isifike… (Anazima taa kisha anatoka na kwenda chumbani kwake) nakupenda Angel

Post a Comment

0 Comments