SCENE 18: -
ENGAGEMENT DAY: -
(ni siku ya Jumamosi,jioni tulivu sana….upepo wa baharini unavuma kwa
mbali,umati wa watu wapatao mia moja na hamsini wamekusanyika katika jumba la kifahari la Raymond Mtoto wa pekee
wa mfanyabiashara maarufu jijini hapo,watu wanaonekana kufurahia hali ya hewa
lakini pia mandhari safi nay a kuvutia ya nyumba hiyo ya kifahari,wahudumu
mbalimbali wanawahudumia wageni waalikwa…akiwemo na bibi harusi
mtarajiwa(Christina),wakati watu wapo nje wakiendelea kuburudika huku
wakisubiri sherehe ianze,Raymond yupo ndani tena chumbani kwa Angelina na
anaonekana hana raha hata kidogo)
Angelina: Raymond…ungetoka humu ndani uende
ukumbini…maana tayari watu wapo nje na wanasubiri sherehe ianze…
Raymond: kwanini usifanye juu chini hii sherehe
isiwepo Angelina…nakupenda wewe nataka kukuoa wewe
Angelina: naomba nikahudumie watu…tafadhali niache
nikafanye kazi yangu, tulizungumza hili mchana unakumbuka? Acha niende (anatoka)
Edmond :(
anaingia ndani) Raymond…uko wapi?
Raymond :( anafungua
mlango wa Angelina) nipo humu…
Edmond: (anashangaa)
wewe una kichaa? Wewe ndugu unafanya nini humo?
Raymond: nimekaa tu...yaani sin ahata chembe ya furaha...hii
engagement isiwepo tu Mond…I swear natamani kutoroka mwenzio
Edmond: acha ujinga embu twende mzee Bembele
anakutafuta
Raymond: sitaki kutoka humu ndani…na hakutakuwa na
sherehe ya pete
Edmond: acha kufikiria kitoto Raymond…watu wamejaa
kishenzi halafu Mimi sikujua Kama hii sherehe itakuwa kubwa...kudadeki
Raymond: sitaki sherehe…Mimi nataka kumuoa Angelina…natoka
nje sasa hivi naenda kutangaza kuwa namuoa Angelina Na si Christina
Edmond: Hiii nyie huyu chizi...embu acha uchizi
Mond
Mrs.Bembele :( anaingia
ndani) Raymond…baba
Angelina :( anatokea
jikoni) shikamoo mama…
Mrs.Bembele :( anamshika
mashavu na kutabasamu) marahaba mwanangu hujambo
Angelina: sijambo mama
Raymond :(
anakuja walipo)
Mrs.Bembele: najua hii ni ngumu sana kwa nyie
wawili ila Raymond toka nje ukamvalishe pete huyo Christina
Raymond: mama…
(Anamuangalia kwa huruma)
Mrs.Bembele: sina cha kukusaidia Zaidi ya kukuambia
wageni ni wengi na usipomvalisha pete Christina, baba yako ataaibika…
Raymond: unamaanisha mama hata ikifika ndoa nimuoe
tu Christina ili baba asiaibike? Mama Unajua kuwa nampenda Sana…
Mr. Bembele :( anatokea
nje) Raymond…
(Wote
wanashtuka)
Mr. Bembele: bado unavaa tu muda wote? Halafu mbona
mpo chumbani kwa mfanyakazi? (Kwa Angelina)
nenda nje ukawahudumie watu…Leo watu wengi Sana huwezi jua unaweza kupata
mchumba
Angelina :( hajibu
chochote na anatoka nje)
Mr. Bembele :( Kwa
Raymond) twende baba…ni muda wako sasa kuonyesha watu kuwa unatarajia
kumuoa mpenzi wako wa siku nyingi sana Christina...comeon lets go
Mrs.Bembele: twende mwanangu
Mr. Bembele: Mimi natangulia (anatoka)
Raymond: mama I can’t do this…siwezi mama kufanya
hivi…iam in love with Angelina…namtaka yeye
Mrs.Bembele: do it my son…tutajua mbeleni…ila kwa
sasa just do it…
Raymond: No mama
Mrs.Bembele: please
Raymond: mama
Mrs.Bembele: twende baba...no way out
(Raymond, Edmond na Mrs.Bembele, wanaelekea moja kwa moja mpaka
bustanini walipo watu. watu wanapomuona Raymond wengine wanapiga makofi wengine
vigelegele yaani ni shangwe na nderemo zinalipuka mahali hapo)
Mmoja wa watu: wow…Bwana harusi wetu mtarajiwa…umependeza
na suti yako…
Mr. Bembele: that is my son… (Anatabasamu)
Raymond :(
anamuangalia Sana Angelina aliyekuwa amesimama pembeni yake)
Catherine :(
anamnong’oneza Edmond) mbona shemeji kanuna hivi
Edmond: anampenda mwanamke mwingine
Catherine: nani?
Edmond: Angelina
Catherine: mdogo wangu?
Edmond: ndio
Catherine: makubwa (anashangaa)
Edmond: nyamaza…
(Pete ya
uchumba inaletwa na mmoja wa wafanya kazi wa ofisi ya Raymond)
Christina :( anafurahi
Sana)
(Watu wanashangilia Sana)
Angelina :( ameinama
na anajisemea moyoni) bora hata nisingemkubalia…nisingekuwa naumia hivi…bora
nisingeruhusu moyo wangu umpende Raymond
Raymond :( Kwa
uyonge anapiga goti moja) Christina
Watu: woyooooooooooooo…
Raymond :( anamshika
Christina mkono) will you marry me?
Watu :( wanapiga
kelele)
Christina :(
anatabasamu)
(Mama na shangazi wa Christina wanaonekana kuwa na furaha kuliko watu
wote hapo)
Christina: Yes…Raymond…I will marry you…
(Watu
wanashangilia Sana)
Raymond :( ananyanyuka
huku anamuangalia Angelina chinichini)
Christina :( anamkumbatia)
Raymond :(
anamkumbatia pia)
Christina: I love you Raymond…
Raymond: I love you too
(Shangwe na
nderemo vinatawala mahali pale, watu wanawavamia Raymond na Christina huku
wengi wao wakitaka kuiona pete ya gharama aliyovalishwa Christina, wakati watu
wanamzingira Christina, Raymond anatumia mwanya huo kuongea na Angelina)
Raymond :( anamvuta
pembeni Angelina) Angel…
Angelina: nambie Raymond…hongera Kwa kuchumbia
Raymond :( anamuangalia
usoni) nakupenda…Sana…nakupenda Angelina
Angelina: wageni wanahitaji vinywaji …naomba
nikafanye kazi yangu
Raymond: Tafadhali…naomba ukae na mimi kidogo
Angelina: baba yako ni mkali sana sitaweza kubishana
nae (anataka kuondoka)
Raymond: Tafadhali Angelina usichukulie hiki kitu
kirahisi hivyo
Angelina :( anamuonea
huruma) tutaongea Raymond...kwa sasa naomba nikahudumie watu
Raymond :( anamkumbatia
na kumvalisha pete Fulani) hii sio pete ya uchumba usishtuke...ni pete tu
nataka uivae kama ishara ya upendo wangu kwako…
Angelina: Asante…
Edmond :( anaonekana
kama alikuwa anamtafuta saa nyingi) ah…Raymond…unaitwa unajua…na kwanini
mnakaa pamoja? Watu watawashtukia
Raymond: kwani ni dhambi?
Edmond: okay sina mood ya kuongea sana, unaitwa na
baba yako
Raymond :(
Kwa Angelina) nenda ukapumzike ndani, acha usifanye kazi yoyote wewe ni mke
wangu…ingia ndani
Angelina :(
anaingia ndani)
Raymond :( Kwa
Edmond) twende
(Wanaelekea ukumbini)
Mr. Bembele :(
anamuona Raymond) ulikuwa wapi baba?
Raymond: chooni…
Mr. Bembele: okay…watu walikuwa wanakuulizia
Christina :( anakuja
alipo Raymond) naomba tucheze...Please
Raymond: nimechoka
Edmond :( anamshika
bega Raymond na kumshawishi)
Raymond :( anavuta
pumzi) okay… (Anamshika kiuno na
kuanza kucheza nae)
Christina: uko sawa?
Raymond: yes
…. Niko sawa…kwani vipi?
Christina: umepooza kweli
Raymond: usijali ni uchovu tu
Christina: you are now my fiancé
Raymond: (hajibu
chochote anaendelea kucheza kama mtu aliyelazimishwa sana)
(Watu wengine nao wanaungana nao kucheza, sherehe
inafana kwelikweli watu wanakula, na kila kitu ni burudani tupu kasoro kwa
raymond)
0 Comments