SCENE 19: -
(asubuhi nyingine baada ya siku ya sherehe ya uchumba kati ya Christina
na Raymond. Raymond anapata chai huku anaonekana anaperuzi kitu mtandaoni)
Raymond :( anaguna)
yaani huyu mwanamke anapenda kujionyesha kweli…picha kila sehemu huko
instagram…yaani (anaweka simu pembeni na
kuendelea kunywa chai) huu ni ushamba, yaani kahakikisha kila mtu anaona
picha hizi ushamba nao ni mzigo (anafyonza)
Angelina :( anakuja
kutokea jikoni) shikamoo…
Raymond: kaka Ray… (Anacheka Kwa nguvu)
Angelina :( anacheka
pia) hata nilikuwa sitaki kukusalimia hivyo…
Raymond: ulitaka kunisalimiaje? Shikamoo mume wangu
au?
Angelina :( anacheka) kwani umeshakuwa mume wangu? Raymond
bwana una masihala sana
Raymond: natarajia…si natarajia kuwa mumeo?
Christina :(
anatoka chumbani akiwa amevaa nguo za kulalia)
Angelina :( anaangalia
chini)
Raymond :(
anamuangalia Angelina)
Christina: good morning my love… (Anambusu Raymond shavuni)
Raymond :( hajafurahia)
morning…umeamkaje?
Christina: nimelala vizuri Sana my love yaani Nina
raha kweli mwenzio
Raymond: Ni vyema Kama ni hivyo…
Christina :(
anatabasamu kisha anakaa pembeni ya Raymond)
Angelina :(
anaondoka)
Christina: binti niletee na mimi kikombe ninywe
chai
Angelina: sawa wifi yangu (anaelekea jikoni)
Christina :( anatabasamu)
Raymond :( ananyanyuka
na kuelekea jikoni) Angelina… (Anamfikia
na kumshika mkono) alilala chumbani kwangu ila sijalala nae, haki ya Mungu
tena…sijamgusa
Angelina: haina shida, hata Kama ulilala nae si
mpenzi wako? Ni mchumba wako
Raymond: nakupenda Sana wewe Angelina, sitachoka kukuambia
hilo baby…nataka mpaka uelewe ni kiasi gani nakupenda Angel
Angelina: ngoja niende nikatenge chai Kwa malkia wa
nyumba
Raymond: wewe ndo malkia wa nyumba hii my love
nakupenda na nitafanya juu chini nikuoe
Angelina: huku umeshatoa mahari, Kwa hiyo sina cha
kutegemea hapo
Raymond: niamini… (Anamshika mikono) Angelina
Angelina: niache Christina anaweza kuja ghafla hapa
ikawa msala
(Wanasikia
sauti ya Christina)
Christina: wewe dada hicho kikombe unanunua
Marekani?
Angelina: naleta dada... (Anarudi alipo Christina) hiki hapa dada…
Raymond :( hana
raha)
Christina: njoo baby tunywe chai…Asante kwa jana
usiku...Usiku ulikuwa mzuri
Raymond :(
anamuangalia Angelina chinichini)
Angelina :(
anamuangalia pia)
Raymond :(
anapandwa hasira) Christina kuna haja gani ya kuongea hayo mbele za watu...na
unaujua ukweli
Christina: si ninaongea tu my love kwani kuna uongo
hapo? Mimi na wewe ni mtu na mtu wake na ni lazima watu waelewe kuwa lazima
tuwe na muda mzuri pamoja… (Anamuagalia Angelina)
au ninasema uongo binti
Angelina: Ni kweli dada unachosema...hujakosea dada
Raymond :(
ananyanyuka kwa hasira na kwenda zake chumbani kwake)
Christina: yaani Raymond ana hasira huyu
Angelina :(
anacheka kidogo kisha anaelekea nje kuendelea na kazi nyingine)
Raymond :( yupo
chumbani kwake) damn this woman!!!!Yaani ana mpango wa kuniharibia penzi
langu na Angelina (simu yake inaita)
nani tena (anaiangalia kisha anapokea)
dad…
Mr. Bembele: mwanangu…hujambo
Raymond: sijambo shikamoo?
Mr. Bembele: marahaba…sasa nilitaka kukuambia kuwa
ofisi imekuandalia sherehe kidogo Kwa ajili ya kukupongeza Kwa kupata mchumba
lakini pia kumaliza chuo
Raymond: dad, sherehe tena? Naanza kuchoka na hizi
sherehe jamani...zimekuwa nyingi wewe huoni? Kunipongeza si tayari baba
umeshanipongeza au mimi ndo sielewi?
Mr. Bembele: relax sio mimi niliyeandaa ni
wafanyakazi wako
Raymond: lini na saa ngapi?
Mr. Bembele: kesho jioni
Raymond: sawa dad…hakuna shida nitakuwa hapo… (anakata simu)
0 Comments