SCENE 20:
(majira ya saa moja jioni, Raymond anaingia
ukumbini akiwa na Angelina na wamependeza sana, ukumbi umependeza watu
wamefurika kuna onekana kuna vyakula na vinywaji vya kutosha, kuna muziki na burudani
ya kutosha na kila kitu kinaonekana kinaenda vizuri, wakati Raymond na Angelina
wanaingia, baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya Raymond wanawaona na wanajikuta
wanavutiwa na muonekano wa wawili hao)
Rachel: jamani ona bosi Raymond alivyopendeza jamani mpaka raha mpaka
nimependa
Pendo:
tena huyo dada ndo kamfanya apendeze Zaidi…dada mzuri huyo
Rachel:
Ni nani?
Pendo:
msichana wake wa kazi shoga yangu
Rachel:
wow…mbona mzuri kuliko yule shoga kidawa yaani ni Mrembo hatari…duh Raymond si
amchukue
Pendo:
si ajabu keshajichukulia…
Christina
:( ambae yuko hapo muda wote miongoni mwa
watu) yaani Raymond ana dharau Sana huyu mwanaume yaani ameniambia
nitangulie kumbe anakuja na dada wa kazi jamani?
(Wakati huo Raymond hata hajali)
Mrs.Bembele :( anamfuata Raymond
na Angelina) sikujua kuwa mnaendana hivyo yani mmependezeana...Mungu
awatunze
Raymond: Asante mama, tumependeza eeh
Mrs.Raymond: sana
Angelina :( anacheka Kwa aibu)
Mr. Bembele :( nae anakuja)
Raymond ndo nini hiki?
Raymond: sijaelewa dad…nini?
Mr. Bembele: mchumba wako amekuja peke yake halafu wewe upo hapa na
hausigeli
Raymond :( anacheka kidogo ingawa
sio kwa furaha) yaani dad…hicho ndo kitu cha kunigombezea mimi? Angelina
ninaishi nae na nilitaka nije nae kwahiyo ningemuacha nyumbani kisa ni
hausigeli
Mrs.Bembele :( anampooza Raymond)
basi baba…msigombane…ona watu wanawaangalia Sana…mtazungumza
Mr. Bembele: naomba uende kwa Christina na uwe nae hii sherehe ni yako
na christina sio na huyu housegirl
Angelina :( anaangalia chini)
Mrs.Bembele: Raymond nenda tu mwanangu …nenda baba
Mr. Bembele: sasa hivi…
Raymond :( anaondoka huku anamuangalia
Sana Angelina)
Mrs.Bembele :( anamshika mkono Angelina)
twende mwanangu
Mr. Bembele: aende wapi abaki hapa…na kwanza yeye si kijakazi? christina
amejisikia vibaya sana, kila mtu alikuwa anawasifia walipoingia (kwa Angelina) wewe si unajua kuwa Raymond
ni mchumba wa mtu?
Angelina: ndio baba…
Mr. Bembele: usiniite baba…Mimi sio baba yako, siwezi kuwa baba yako
wewe maskini
Mrs.Bembele: kwani yeye kasema wewe ni baba yake si kakuita tu kiheshima
Mr. Bembele: Gloria kwanini unapenda Sana kumtetea huyu kijakazi
aliyekuja kuharibu sherehe Za watu?
Mrs.Bembele: hajaharibu sherehe za watu, basi fanya unavyotaka
Mr. Bembele: haraka (Kwa Angelina)
nenda kagawe vinywaji na hilo gauni zuri sijui nani kakununulia au umepewa na
mkwe wangu
Mrs.Bembele: jamani baba Raymond ni maneno gani hayo makali unayoongea
kwa binti wa watu?
Mr. Bembele: huna mamlaka ya kunihoji…
Mrs.Bembele: Nina mamlaka baba Ray…usishau mimi ni mkeo
Mr. Bembele :( Kwa Angelina)
unaona wewe binti unayoyasababisha ugomvi kwenye familia yangu,mke wangu na
mwanangu wote wanakutetea wewe umetoka na uchawi gani Ngara?
Angelina :( kimya)
Mrs.Bembele :( Kwa Angelina)
nenda mwanangu ukafanye kazi zako
(Angelina anaondoka na kwenda
kugawa vinywaji)
Pendo:(anamuona Angelina anagawa vinywaji)
jamani Mrembo anagawa vinywaji(anamfuata)wewe
kuna watu wamewekwa kwa ajili ya hii kazi wewe tena umeingia na boss kazi yako
ni kufurahia maisha, halafu wewe na bosi mmedamshi kweli yaani hivi mmejiona?
Angelina :( anacheka kidogo)
Pendo: acha kuhudumia shoga yangu tukae wote
Mr. Bembele :( anajitokeza kwa
nyuma yao) unamwambia aache kuhudumia wewe kama nani?
Pendo: He!!!Makubwa!!!
(Upande alipo Raymond na Christina)
Christina: yaani wewe mwanaume una dharau Sana…yaani umeniacha nije peke
yangu halafu wewe ukaja na msichana wa kazi…
Raymond :( anampuuzia)
(Edmond na mpenzi wake wanaingia ukumbini hapo na Raymond
anawaona bila kupoteza muda anawandea)
Raymond: karibuni jamani mmependeza
Edmond: hatukuzidi…
Catherine: habari za jioni shemeji
Raymond: salama shemeji yangu karibu Sana hapa kwetu
Catherine: Asante (anaangalia
angalia huku na huku kama mtu anayetafuta kitu) simuoni Angelina hajaja?
Raymond: yupo na mama yangu… (Anaangalia
angalia huku na huku anamuona Angelina amebeba trei la vinywaji anapita kwa
watu na kugawa vinywaji) what???!!!My woman? Anagawa vinywaji? (Anamfuata)Angelina kwanini unafanya
hivi?
Angelina: niache Raymond tafadhali hii ni kazi yangu na sitaki ugomvi…we
endelea na sherehe imepangwa kwa ajili yako na mchumba wako
Raymond: lakini…
(Anakatishwa na tangazo Fulani linalotangazwa na
baba yake)
Mr. Bembele: jamani habari za jioni mabibi na mabwana…ninatumaini
mnafurahia usiku huu mtulivu
Watu: Sana
Raymond :(macho yote kwa Angelina
ambae anaendelea kugawa vinywaji)
Mr. Bembele: nimeomba utulivu ila naona wapo wadada wengine sijui wamelelewa
vipi na wazazi wao bado wanafanya mambo yao kama wewe binti unaegawa vinywaji
huwezi kujiongeza kuwa kuna mtu yuko hapo mbele anahitaji utulivu?
Christina :( anacheka Sana)
Shangazi yake Christina: acha kucheka shoga yangu
Christina :( anaacha) yaani
amepewa la usoni
Shangazi: we acha tu (anacheka
pia)
Raymond :( anachukia Sana)
Mrs.Bembele :( nae anaonekana
kuchukia)
Mr. Bembele: tabia za kimaskini hizo (anajichekesha kidogo) tuendelee tafadhali na endeleeni kufurahia maisha
yenu binafsi… (Anashuka na kuendelea na shughuli nyingine) cheers to my son and
his fiancée
Watu: cheers (wanagonga glasi)
Raymond :( anamfuata Angelina)
Angel…nakupenda sana na naomba hilo uliweke kichwani kuwa nipo kwa ajili yako
mpenzi wangu nakupenda mno…tafadhali kama hutajali naweza kukupeleka nyumbani
tukawe na sherehe yetu wawili tu mimi na wewe baby…
Angelina: acha niendelee na kazi zangu… (Anaondoka alipo Raymond)
Raymond :( bado anamfuata Angelina)
najua umejisikia vibaya sana kwa alichosema baba mbele za watu naomba unisamehe
mimi Angelina
Angelina: nimeshakusamehe naomba uende kwa mchumba wako
Edmond na Catherine :( wanawaangalia
Angelina na Raymond)
Edmond: yaani hili penzi lina vita Sana, sijui Kama litafika mbali
Catherine: wenyewe tu wanatakiwa wawe na msimamo wasipokuwa nao lazima
wataachana tena hivi karibuni
Edmond: yaani mzee Bembele hampendi kabisa Angelina
Catherine: yaani… (Anatikisa
kichwa ishara ya kusikitika)
Edmond: embu tuendelee na mambo yetu
(Watu
wanaendelea kufurahia sherehe ile, wengine wanakunywa, kuna wanaocheza,
wanaokula, wanaocheka, huku Angelina akionekana kufanya kazi yake kiufasaha,
huku Raymond akionekana hana raha na sherehe hiyo)
Raymond: Angel…please baby
Angelina: please ndo nini sijasoma Mimi
Raymond: naomba unisikilize
Angelina: nenda kwenye sherehe
Raymond: twende nyumbani
Angelina: kamwambie mchumba wako (anaondoka zake)
(Raymond anabaki akiwa mnyonge Sana)
0 Comments