SCENE 21: -
(Mr. Bembele
na mke wake pamoja na wazazi wa Christina na Christina mwenyewe wanafika
nyumbani kwa Raymond wakionekana kuna jambo muhimu sana wanataka kuzungumza nae,
wanapofika wanapokelewa vizuri sana na Angelina ambae alikuwa anafanya usafi wa
ndani)
Angelina :( anawasalimia
Kwa heshima Sana) shikamooni...Karibuni
Mama Christina :( anabenjua midomo)
Shangazi :( anabenjua
midomo pia)
Christina :( anabenjua
midomo)
Baba Christina :( anaachia tabasamu) marahaba mama
Mrs.Bembele: marahaba mama hujambo
Mr. Bembele: ndo umeamka sasa hivi utasema wewe ndo
malkia wa nyumba hii
Raymond :( anatokea
chumbani) dad…
Mr. Bembele: huyu mtoto…anajiona malkia wa humu
ndani…anaamka saa nne
Raymond :( anaona
ampuuzie) karibuni ndani (Kwa Angelina)
nenda kaendelee na kazi nyingine achana na hii kazi kwanza utakuja kuendelea
baadae
Angelina: sawa (anaondoka)
Mr. Bembele: sema sawa boss
Angelina: sawa boss (anaondoka kuelekea jikoni)
Raymond :(
yupo kimya huku anaonekana kukasirishwa Sana)
Mrs.Bembele :( anamshika
bega mwanae)
Raymond: karibuni Sana
(Kwa pamoja wanaingia ndani maana muda wote walikuwa wanaongelea nje)
Baba Christina: habari za hapa mwanangu…
Raymond: salama kabisa baba… (Kwa wote) shikamooni
(Wote
wanaitikia ikiwemo na christina)
Mr. Bembele: za hapa mwanangu…?
Raymond :(
sio Kwa furaha) salama kabisa za huko?
Mr. Bembele: ila mbona unaonekana kutokuwa na raha
na mimi mwanangu?
Raymond: wasiwasi wako tu mi mbona nipo sawa
Mr. Bembele: sasa sisi hatutachukua muda mwingi
hapa tunajua umechoka na unahitaji kupumzika…
Raymond: sawa nawasikiliza tu…
Mr. Bembele: mwanangu mbona Jana ulimuacha mchumba
wako na kuingia na msichana wa kazi ukumbini unajua hiyo haikuwa picha nzuri
hata kidogo…unadhani mchumba wako alijisikiaje?
Raymond :(
anacheka kidogo) dad…hicho ndo kitu ulichokuja kuniambia? Mi nilichelewa
kujiandaa ndo maana nikamwambia Christina atangulie ukumbini na kuhusu kuja na Angelina
sikuona haja ya kumuacha…nyumbani
Mr. Bembele: nakuamuru mimi kama baba yako uweke
ukaribu Zaidi na mchumba wako na sio msichana wa kazi na pia nimepata habari
kutoka hata kwa Ramadhani kuwa upo karibu na msichana wako wa kazi
Raymond: Hilo nalo ni tatizo…baba kwamba kuwa
karibu na mtu anayekupikia nalo ni tatizo?
Mrs.Bembele :(
Kwa Raymond) baba tulia acha kujibizana na baba yako
Raymond :( kimya)
Mr. Bembele: huyu mtoto anajifanya anajua Sana, una
kiburi Sana je hivi ndo unanifanyia baada ya kukupa kila kitu?
Raymond: kwahiyo umenipa kila kitu ili unitawale?
Nisiwe na uhuru…okay navirudisha vyote…na huyo Christina simuoi
(Wote waliokuwepo hapo wanabaki mdomo wazi)
Mama Christina: baba usiseme hivyo
Raymond: Mimi Nina uhuru wa kuishi navyotaka…na
sitaki kumuoa Christina wala sitaki hii nyumba, kazi, gari wala chochote kile
Mr. Bembele :(
anajishusha) mwanangu umepaniki
Raymond: sijapaniki hata kidogo naongea nikiwa na
akili timamu ni kwamba sitaki kumuoa Christina na bora mmekuja wote ili
niwaambie vizuri kabisa kuwa sina nia ya kumuoa Christina…
Christina: kwanini ulikubali kunivisha Pete ya
uchumba?
Raymond: ilikuwa ni presha kutoka kwa baba…sina
mpango wa kukuoa Christina
Mrs.Bembele :(
anamshika bega) mwanangu
Mr. Bembele: Mama Ray…tafadhali mshawishi mwanao
kuwa itakuwa aibu Sana tumeshaalika watu wengi sana
Raymond: watakuja kushuhudia yangu na mwanamke
mwingine…baba kosea vyote ila usikosee kuoa au kuolewa utajuta maisha yako yote,
sipo tayari kukosea sitaki kujuta mimi baba
(Wote
wanabaki wanamshangaa)
Baba Christina: mwanangu…Raymond…mi naona kabisa
umechukia Sana, baba yako anavyokusukuma mambo mengi msamehe nay eye ni mzazi
anataka kuona mwanae una furaha najua unaongea kwa hasira msamehe baba yako na
tusamehe sote
Raymond :( kimya
huku ameangalia chini)
Shangazi: tusamehe baba…tumekosa Sisi…yaishe
mwanangu
Mr. Bembele: nisamehe mwanangu sitakusukuma
tena…ila tu naomba usiuvunje huu uchumba tafadhali
Raymond :(
anashusha pumzi kama mtu aliyechoka) sawa haina shida...
Mr. Bembele: Asante mwanangu…
(Kila mtu anaonekana amepata Amani Fulani)
Mrs.Bembele :( anamuangalia
Angelina ambae yupo jikoni ambapo mtu kama umekaa sebuleni unamuona aliopo
jikoni na aliyopo jikoni anamuona mtu aliyopo sebuleni kwa kifupi kuna uwazi)
Angelina :(
anamuangalia Mrs.Bembele kisha anatabasamu)
Mrs.Bembele :( anamuangalia
pia kisha anatabasamu)
Mr. Bembele: Mama Ray…twende... (Anaangalia anapoangalia) unaangalia
nini?
Mrs.Bembele: hakuna jipya
Mr. Bembele: na wewe unamfurahia huyo dada?
Mrs.Bembele: twendeni
(Wote
waliokuja wananyanyuka na kuondoka wakiwa wanasindikizwa na Raymond)
Raymond :( akiwa
amewafikisha kwenye magari waliokuja nayo) haya jamani fikeni salama mi
ngoja nirudi kulala
(Wanaagana kisha wanapanda kwenye magari na kuondoka)
Raymond :(
anarudi ndani anamkuta Angelina anaendelea na usafi anamkumbatia) malkia
wangu
Angelina :( anahangaika
kujitoa kwake) Raymond…je Kama hawajafika mbali na wakatukuta tupo hivi?
Raymond: hawawezi kurudi hata kwa bahati mbaya… (Anamvuta na kumpakata) natamani
nitangaze ndoa yetu hata jumapili hii
Angelina: baba yako atatunyonga…
Raymond: nikikuoa kisiri ataniua?
Angelina :( anacheka
Kwa aibu)
Raymond: nakupenda sana mpenzi wangu na ninataka
nikuoe Angel…
Angelina: nakupenda pia (ananyanyuka)
Raymond: ukizaa watoto watakuwa wazuri
Angelina :(
anacheka huku anaenda jikoni) Asante…nitakuzalia usijali
Raymond:
ngoja nikalale…nisije nikajikuta nafanya dhambi hapa (anaingia ndani kwake na kupanda kitandani kisha analala huku jikoni Angelina
anaendelea na kazi zake kama kawaida) kesho nitaenda kuongea na Christina
jambo Fulani ni muhimu nimuone kesho (anapanda
kitandani na kujilaza)
0 Comments