SCENE 22: -
(majira ya saa kumi na mbili jioni, mara
baada ya kazi Raymond anaamua akamuone Christina ili azungumze nae mawili matatu,
anapanda gari lake kisha analiondoa kuelekea katika jumba la kifahari la kina
Christina baada ya mwendo wa kama nusu saa anafika nyumbani hapo, anawakuta
Christina na mama zake wamekaa barazani wakizungumza umbea kama kawaida yao,
anawasalimia kwa heshima kubwa)
Raymond
:( anatabasamu kidogo) shikamoo mama,
shikamoo shangazi…
Mama
na shangazi :( wanaitikia) marahaba
baba…karibu
Raymond:
Asante (Kwa Christina) habari za
hapa?
Christina:
nzuri karibu (ananyanyuka na kuelekea
ndani) karibu ndani
Raymond
:( anamfuata ndani) Asante… (Anaingia ndani)
Christina
:( anakaa kwenye sofa)
Raymond
:( nae anakaa kwenye sofa)
Christina
:( anajaribu kumkalia)
Raymond:
hapana…sipo tayari Kwa sasa
Christina:
una maana gani?
Raymond:
naomba utulivu…
Christina:
okay…ungependelea kinywaji gani…my love?
Raymond:
no thank you…nipo sawa…
Christina:
at last…tupo pamoja baada ya muda Mrefu… (Anacheka
kidogo lakini tabasamu linapotea mara baada ya kugundua kuwa Raymond hayuko nae
yaani ana mawazo mengine) vipi Raymond uko sawa baby?
Raymond
:( kimya huku anaonekana hajui aanzie
wapi)
Christina:
talk to me baby…whats wrong.
Raymond
:( kimya)
Christina:
kuna sehemu nimekuudhi?
Raymond:
hapana hakuna sehemu uliyoniudhi ila kuna jambo nataka kukuambia na sijui
nianzie wapi
Christina:
kuwa huru baby…nakusikiliza…
Raymond:
iam ni love with someone else… (Kimya
kidogo) sijui ilianzaje but kuna mwanamke nampenda Sana na siwezi kuficha
tena kwa watu nataka niwe nae…yeye ndo ananipa Amani ya moyo…nampenda sana
Christina
:( anakasirika Sana huku machozi
yanamlenga) you cannot be serious Raymond…
Raymond:
Kwa bahati mbaya nipo very serious…nipo very serious Christina
Christina
:( Analia) tumekaa pamoja miaka mingi
sasa tunakaribia kuwa mke na mume unaniambia kuwa una mwanamke mwingine na
unampenda sana…
Raymond:
iam so sorry sikupanga yote haya mama, yaani hata Mimi naumia kila
nikatafakari…naona nimekufanyia unyama ila imetokea na kila siku nampenda zaidi
ya jana…
Christina:
hatuwezi kuachana Raymond…
Raymond
:( Kwa mshangao) kwanini?
Christina:
our wedding is around the corner watu watanifikiriaje Mimi na familia
yangu…basi nioe utanipa talaka mbele ya safari…
Raymond:
iam so sorry siwezi kufanya hivyo hata nikitaka…haiwezekani namuoa huyo dada
ambae nafsi yangu imeniridhia…iam so sorry Christina
Christina:
(bila kutarajia) iam pregnant…
Raymond
:( kwa mshangao) what?!!!
Christina:
yes…Nina ujauzito wako Raymond
Raymond:
mbona hukuniambia mapema Leo ndo unaniambia?
Christina
:( anafuta machozi) nilitaka iwe
surprise…ila leo umenijia na hili nimeona tu nikuambie tu
Raymond:
Ina muda gani?
Christin:
miezi miwili...
Raymond:
lakini mbona hiyo miezi miwili hatukutana kimwili tumekutana juzi tu…inamaana Kama
mimba labda ina mwezi hivi na sio miwili au umechanganya...
Christina
:( anajiumauma) kitu Kama hicho sina
uhakika…
Raymond:
okay nionyeshe matokeo au kipimo cha mimba si umepima?
Christina:
sijui niliyaweka wapi…
Raymond:
una uhakika una ujauzito?
Christina:
ndio unaona nakudanganya au?
Raymond:
iam a doctor kesho njoo hospitali kwangu nitakupima
Christina:
inamaana huniamini au?
Raymond:
hapana sio hivyo nachotaka ni kujua hiyo mimba ina muda gani…maana wewe
mwenyewe hujiamini na wala huna uhakika
Christina:
okay mi nitakuja kesho kupima ila je ikiwepo itakuwaje?
Raymond:
sitaukimbia wajibu wangu Kama baba wa huyo mtoto
Christina:
kwahiyo tutaoana?
Raymond:
hapana hatutaoana…tutakuwa tu wazazi wenza…na mwanamke wangu nitamwambia juu ya
hilo
Christina:
huyo mwanamke ni nani?
Raymond:
sitapenda kumuweka wazi kwanza mpaka pale baba atakapomkubali…
Christina:
you are such an animal and I hate you so much…
Raymond:
iam sorry I love her too much...Yaani mpaka nimeamua kukuambia Ni kwamba I cannot
control my feelings anymore
Christina
:( anasikitika huku Analia) ninakupenda Sana Raymond…
Raymond:
iam so sorry...
Christina: haina shida lakini
Raymond:
okay (huku ananyanyuka) kesho
usisahau kuja ofisini kwangu tuangalie hiyo mimba ni ya muda gani…
Christina:
sawa…
(Kwa pamoja wanatoka nje walipo mama na
shangazi yake Christina, Raymond anawaaga kisha anapanda gari lake na kuondoka)
Christina
:( anaguna)
Mama:
mwenzetu vipi?
Christina:
acha tu…
Shangazi:
tatizo nini?
Christina:
Raymond ameachana na mimi
Mama:
kisa nini?
Christina:
eti anampenda mwanamke mwingine...
Shangazi:
halafu alivyo ana dharau mshenzi huyu…anakuambia kabisa yaani mtoto hana haya
huyu (anafyonza)
Christina:
kizaazaa kinakuja nimemdanganya kuwa Nina mimba…huku sina na wala sijui naitoa
wapi sasa hivi...
Mama:
we endelea tu kumdanganya mpaka pale tutakapopata ufumbuzi mwingine…
Christina:
amesema kesho niende akanipime
Shangazi:
usiende
Mama:
asipoenda atakuja hivi unamjua Raymond unamsikia?
Shangazi:
sasa tufanyeje
Christina:
kwa sasa sijui cha kufanya natamani ardhi ipasuke niingie ili hiyo kesho nipate
kisingizio kuwa ardhi ilipasuka nikaingia...
(Shangazi na mama wanacheka sana)
0 Comments