IAM IN LOVE WITH MY HOUSEGIRL 23

 


SCENE 23:

(Asubuhi nyingine tulivu na njema, upepo Fulani mwanana unavuma kwa mbali, Christina anafika ofisini kwa Raymond anapofika anaenda moja kwa moja mpaka alipo nesi ambae walizungumza nae kuhusu masuala ya ujauzito)

Christina: za asubuhi shoga yangu

Imelda :( nesi) salama mambo vipi shoga?

Christina: poa…

(Wakati huo Raymond anatokea ofisini kwake na anaonekana hayuko bize sana na anatembeatembea kuwasalimia wafanyakazi wake)

Raymond :( Kwa sekretari wake) yaani Glory...Kwa kuchelewa wewe hujambo

Glory :( anacheka) jamani Raymond

Raymond :( anatabasamu huku anaangalia upande alipo Christina) yule si Christina?

Glory: ndo yeye

Raymond :( anamuita) Tina…

Christina :( anageuka anaona anayemuita ni Raymond anatoa macho kama mjusi kabanwa na mlango) Raymond...Nilipita kumsalimia Imelda…nakuja tangulia

Raymond: twende ofisini maana nataka kutoka…kuna sehemu naenda (anaingia ofisini kwake)

Christina :( anamfuata)

Raymond: karibu uketi…

Christina :( anaonekana hana Amani kabisa)

Raymond: vipi? Mbona unaonekana huna raha?

Christina: hapana mbona nipo kawaida?

Raymond: ulisema una mimba eeh…

Christina :( anakuwa na kigugumizi) …. ndi…o

Raymond: sawa lets comfirm it!!Kama una mimba nitatunza mtoto na wala sitakimbia majukumu yangu ila nikigundua kuwa unanidanganya…nitakasirika sana…

Christina: okay haina shida…

Raymond: okay… (Ananyanyuka na kuchukua kipimo cha mimba na kurudi kukaa, anampa kichupa) kalete mkojo

Christina :( anaonyesha kutetemeka)

Raymond: vipi? Mbona unatetemeka?

Christina: hapana Raymond…kawaida tu (anachukua kichupa kisha anatoka nje)

Raymond: mbona hata humu ofisini kwangu kuna choo…ingia humo

Christina :( anaingia chooni) Mungu wangu (anachukua mkojo) nitafanya nini Mimi Leo?

Raymond :( akiwa bado amekaa kwenye kiti chake) najua unanidanganya Christina…

Christina :( anarudi na mkojo kwenye kichupa kidogo na kumpa Raymond) halafu nilisahau kukuambia

Raymond: ulisahau nini?

Christina: mimba ilitoka…nahisi Mimi bila kujua

Raymond :( anacheka kidogo) we nenda tu nje nitakuita baada ya muda…

Christina :( anatoka akiwa anatetemeka)

Raymond: hata sijisumbui kupima huu mkojo ni kwamba tu hana mimba… (Anachukua simu ya mezani na kumpigia sekretari wake) Glory naomba umwambie Christina arudi ndani namuita…

Glory: sawa boss (anamuita Christina) dokta anakuita

Christina :( anaingia akiwa mnyonge Sana)

Raymond: mbona u mnyonge Sana? Tatizo nini?

Christina: hamna tatizo

Raymond: kwanini usifurahi kuwa unaenda kuwa mama

Christina :( anaonyesha kutoelewa kitu) una maana gani?

Raymond: sina maana yoyote ni kwamba umekuja kwangu…nikupime mimba inamaana unatakiwa ufurahi kuwa hatimaye unaenda kuwa mama lakini wewe tangu umeniletea mkojo niupime huna raha tatizo nini?

Christina: hakuna tatizo Raymond

Raymond :( anasimama na kumshika bega lakini ghafla anambinya kwa nguvu na kwa hasira) kwanini umenidanganya kuwa una mimba yangu?

Christina: Raymond… (Analengwa na machozi)

Raymond :( anapaza sauti) kwanini lakini Christina

Christina :( anaanza kulia) sikuwa na njia nyingine ya kukufanya ubaki kwangu Raymond…sikutaka kukupoteza Raymond nakupenda

Raymond: pumbavu…kabisa…sasa umenipoteza umekaa na mimi miaka yote hiyo ila inaonyesha kuwa hujui ninachokichukia…nachukia uongo (anamsukuma)

Christina :( anaangukia kwenye sofa)

Raymond: nilitaka ubaki kuwa rafiki yangu lakini hata huo urafiki nauvunja siutaki tena…. i hate you

Christina: naomba unisamehe sana mpenzi wangu na tusahau yaliyopita Raymond…usiniache (ananyanyuka na kumfuata aliposimama maana muda wote huo wanaongea Raymond alikuwa amesemama) naomba unisamehe Raymond tuendelee kuwa wapenzi sitajali hata nikiwa spea tairi (anapiga magoti) nisamehe Raymond jamani…naomba unisamehe

Raymond: nyanyuka na usirudie kunipigia magoti na ninakuomba uondoke na ukapumzike…sikusamehe Christina umenikosea sana

Christina: nipe adhabu nyingine ila usiniache Raymond…

Raymond:toka ofisini kwangu wewe ni shetani kama tu umeweza kunidanganya kitu kidogo…je nikikuoa si utanidanganya mambo mengi na makubwa?siwezi kuwa mpenzi wako hiyo pete uliyo nayo mkononi ni ya thamani sana na unaweza kuiweka kama zawadi yangu kwako kuanzia leo sitaki kukuona hata kidogo usinijue usinipigie wala usinitafute kwa njia yoyote ile mimi na wewe ni basi kabisa…sitaki tena umenidanganya vya kutosha kuwa umeachana na Peter huku bado upo  nae…leo tena umenidanganya mimba sijui kesho utanidanganya nini I can’t take that risk…so it is over…haya nje mara moja…

Christina: nisamehe nakuomba

Raymond :( anachukua simu ya mezani na kupiga kwa walinzi) naomba mje mmtoe nje kuna mtu analeta fujo

Christina: imefikia huko Raymond…

(Walinzi wanakuja na kumshika Christina na kumtoa nje)

Raymond:(anakaa chini huku amejiinamia kwa mbali anasikia sauti nyororo ya kike inamuita ananyanyua uso na kukutana na kipenzi chake yaani Angelina) Angel…malaika wangu (ananyanyuka na kumkumbatia) asante kwa kuja mama nakuhitaji sana wakati huu

Angelina: nimemuona Christina anaburuzwa kuna nini? Na mbona wewe unaonekana una mawazo Sana

Raymond: nikumbatie mpenzi…nachohitaji ni faraja yako…nina hasira sana

Angelina :( anamkumbatia) punguza hasira

Glory :( anaingia bila hodi anawakuta wamekumbatiana) oh…samahani (anafunga mlango haraka na kurudi ofisini kwake)

Raymond: Christina muongo Sana…Jana nilienda kumwambia ukweli juu ya penzi letu, akaniambia hawezi kuniacha maana ana ujauzito wangu…kumbe Ni uongo…

Angelina: wewe umejuaje kuwa Ni uongo?

Raymond: tabia yake tu tangu amefika nikawa siielewi  

Angelina :( anamsikiliza kwa makini)

Raymond: nilimuuliza na bila uoga akajibu kuwa ilibidi afanye hivyo ili asinipoteze…nimemuacha simtaki tena katika maisha yangu mwanamke ni muongo sana huyu…

Angelina: basi…punguza hasira…

Raymond :( anashusha pumzi kisha anabadilisha mada) nambie sasa umekuja kufanya nini? (Anampakata)

Angelina: kukusalimia tu…nimeona nyumbani sina mtu wa kuongea nae

Raymond: Safi Sana…usiongee na Ramadhani yaani nina wivu kama wa ngedere

Angelina :( anacheka Sana) inabidi upunguze usiwe na wivu mpenzi wangu...Wivu hubomoa

Raymond :( anacheka pia) serious Nina wivu sitaki ukae peke yako na Ramadhani ni mhuni sana sitaki kabisa akuzoee wala umzoee sawa ee

Angelina: sawa nakusikiliza wewe mpenzi...Nakuahidi sitakaa nae karibu nakusikiliza wewe (anatabasamu kisha anamkumbatia Kwa mahaba mazito mpenzi wake huyo)

Raymond: nikumbatie tena…nafurahi kukuona Angelina wangu mpenzi

Angelina :( anamkumbatia) utazoea bwana

Raymond: kumbe wewe sio mshamba Kama nilivyokuwa naona (anacheka)

Angelina: kwahiyo Mimi mshamba

Raymond: nakutania jamani sio ukweli bwana

Angelina: sitaki bwana

Raymond: nakupenda Sana…na ninakuhitaji sana

Angelina :( anatabasamu) hata Mimi nakuhitaji Sana Raymond…

(wanaendelea kucheka na kuongea huku kila mmoja wao anaonekana kufurahia uwepo wa mwenzie na wanaonekana wamezama kabisa katika penzi zito na wala hawajali kama kuna mtu atakuja na kuwakuta katika hali ile, ni shangwe kati yao na mara kwa mara wanaangaliana, wanatabasamu, wanafurahi yaani kwa ujumla ni Amani tu kati yao)

Glory :( anawachungulia) jamani wanaonekana wanapendana hao …hapo sasa boss amepata mwanamke sio yule kigagula mwanamke ni mcharuko huyo kha!!

Angelina: acha Mimi niende nimekusalimie

Raymond: tukae wote bwana kwanza leo sina kazi nyingi sana

Angelina: unaonekana huna kazi maana umekaa tu

Raymond :( anacheka) kwahiyo nimekaa tu Kama zombie

Angelina: zombie ndo nini?

Raymond: Leo tukaangalie muvi ya zombie utawajua tu... (anacheka kwa nguvu)

Angelina: wanaonekana kuogopesha Sana

Raymond: kumbe unawajua

Angelina: nimehisi tu

Raymond :( anacheka)

Angelina :( anacheka pia)

Post a Comment

0 Comments