SCENE 24: -
(Ni asubuhi
nyingine njema kama ilivyofanywa Na bwana, watu wanaonekana kuanza kazi zao za
siku Kama ilivyo kawaida, Angelina yupo jikoni anaandaa chai huku anaimba wimbo
mmoja wa kumsifu Mungu)
Raymond :( anakuja nyuma yake na kumkumbatia)
wow una sauti nzuri sana bibie… (Anacheka
kidogo) umeamkaje lakini?
Angelina: salama… (Anamsukuma) wewe wazazi wako wakija ghafla je…?
Raymond: I do not care…yaani hata sijali kwakweli
Angelina: yaani wewe…litakukuta jambo si unawajua
wazazi wako tena hasa baba yako
Raymond: hata sijali mwenzio Asante kwa upendo…wako
(anataka kumbusu)
Angelina :( anachengesha)
Raymond ulisema utasubiri…
Raymond :( anacheka)
haidhuru kitu ila uko sawa bwana… (Anacheka)
haina shida mke wangu…
Angelina: kaa hapo nikuletee chai…
Raymond: hapana we huoni nimeshajiandaa nataka
tutoke nikupeleke shopping ukanunue nguo, viatu na simu mpya nataka uwe mke
wangu na nitafanya kila kitu uwe wa hadhi yangu…usiichukulie vibaya hiyo…haya
cha kufanya nenda kavae tutoke mke wangu
Angelina :( anacheka
Sana) sawa nipe dakika kadhaa nikaoge na kubadili nguo…
Raymond :( anaguna)
sasa hapo nitalazimika kukaa na kunywa chai maana nyie kuoga na kuvaa ni
mnachukua miaka hata mia… (Anachukua chai
na kujitengea mezani na kuanza kunywa)
Angelina :( huku
anaingia chumbani kwake) nipe dakika 20 tu
Raymond: sidhani Kama hizo dakika 20 utakuwa tayari
(Angelina anaingia chumbani na kuanza kuoga na baada ya muda kidogo
anamaliza kuoga, anavaa harakaharaka kisha anatoka na kumkuta Raymond bado
anakunywa chai)
Angelina :( anatabasamu)
mi si nilikuambia? Nachukua dakika chache sana kumaliza maandalizi
Raymond :( anamalizia kunywa chai) haya twende au
tusubiri unywe na wewe?
Angelina: hapana…twende tu (anatoa vyombo alivyotumia Raymond) haya tayari twende tu…
Raymond :(
anachukua funguo wa gari, kisha yeye pamoja na mpenzi wake wanatoka nje na
kupanda gari) baby uko poa? (Anamfunga
mkanda kisha analiwasha gari)
Ramadahani: naona mnaenda matembezi
Raymond :( anatabasamu)
baadae kidogo
Ramadhani :( anafungua
geti na kuruhusu gari liondoke)
(Raymond na mpenzi wake wanaondoka kuelekea duka la nguo moja maarufu,
njiani wanaongea mambo mengi na angelina anaonekana kuifurahia safari hiyo.
Baada ya mwendo wa karibia nusu saa hatimaye anafika dukani)
Raymond :(
huku anashuka kwenye gari) haya tumeshafika baby...
Angelina :(
nae anashuka kutoka kwenye gari)
(Wanaingia
ndani ya duka na kuanza kuchagua nguo)
Angelina: nisaidie kuchagua nguo maana Mimi hata
sijui kuchagua
Raymond: usijali mpenzi wangu, Mimi mjanja ndugu
yangu (anacheka kidogo) hapa umefika
Mdada wa mapokezi :( anatabasamu)
Raymond :( Kwa
dada) vipi dada mbona unanicheka?
Mdada: hapana sikucheki nakuangalia tu unavyompenda
mke wako…
Raymond: Ni malkia wangu ni lazima nimpende
Mdada: hiyo ni kweli yaani hadi raha mnaonekana
mnapendana sana (anatabasamu) basi
endeleeni kuchagua…
Raymond :(
anaendelea kumchagulia nguo Angelina wake)
Angelina :( anaonekana
kufurahia)
Raymond: mke wangu…chukua hii ukajaribu tuone
itakukaaje? (Anamuita mhudumu) njoo
uende ukamsaidie malkia wangu kuangalia hii nguo
Mhudumu: sawa haina shida (anamuongoza Angelina mpaka chumba cha kubadilishia nguo)
Raymond :( anaendelea
kuchagua nguo)
Mhudumu :( yupo
ndani na Angelina) imekukaa vizuri sana
Angelina: ila ni fupi sana...
Mhudumu: kamuonyeshe mumeo…atafurahi yaani imekupendeza
Sana
Angelina: hapana ni fupi sana
Mhudumu: si unaenda kumuonyesha mumeo?
Angelina :(
anajikuta anaona aibu)
Mhudumu: twende bwana
(Wanatoka)
Raymond :( anageuka
na anakutana na Angelina akiwa ndani ya gauni moja matata) wow… (Anamuangalia umbo lake lilivyo zuri)
umeumbika jamani
Mhudumu :( anacheka) yaani unavyomuangalia…Kama sio
mkeo...Limemkaaje?
Raymond: amependeza sana jamani nimebahatisha…
(Mdada WA
mapokezi na mhudumu wanacheka)
Raymond: hili tutalichukua…
(Wanaendelea kuangalia nguo nyingine na viatu na wakati huo mmoja wa
marafiki wa Christina anaingia katika duka lile, anaangaza angaza lakini ghafla
anamuona Raymond akiwa na Angelina)
Rafiki wa Christina: jamani huyo si shemeji? (anamuangalia vizuri) ni yeye…anaonekana
yupo kwenye mahaba mazito na huyu binti…mwenzangu ngoja nimuulize shoga yangu
huyu…(anaguna)na huu umbea utatuua jamani
(anachukua simu na kumpigia Christina,
simu inaita na mwisho inapokelewa) shoga mambo vipi?
Christina: poa…kwema?
Rafiki: kwema…shoga yangu nachoona sijui ni kweli
au macho yangu?
Christina: kwanini unasema hivyo?
Rafiki: kwani wewe na shem…mmeachana?
Christina: hapana…kwani vipi?
Rafiki: namuona hapa yupo na demu mwingine
nakwambia ni full maloveee
Christina: ananisaliti huyo mwanaume mshenzi (anajisemea moyoni) ni nafasi nzuri na ni
muda wangu muafaka kumjua huyo Malaya aliyenipokonya danga langu (kwa rafiki yake) embu naomba uwapige
picha unitumie whatsapp tafadhali naomba unisaidie
Rafiki: usijali love, nafanya hivyo sasa hivi (anawapiga picha na kumtumia Christina)
shoga angalia whatsapp yako
Christina: poa (anakata
simu na kuangalia anapigwa na butwaa na haamini anachokiona) what? housegirl?
yaani housegirl ndo kanipiku mimi?
Rafiki :( anampigia tena) umemjua huyu dada…
Christina: hapana simjui
Rafiki: njoo shoga yangu…uliamshe
Christina: haina haja (anakata simu) Raymond… (Anajikuta
anapiga kelele) mshenzi wewe…nakuchukia (anajikuta anatokwa machozi) yaani hausigeli ndo kanipiku Mimi…
nilivyo mzuri hivi (Analia Sana)
(Upande wa kina Raymond wanamaliza kuchagua nguo na viatu, analipa kisha
wanatoka na kuondoka zao)
Raymond: twende tukanunue simu nataka simu zetu zifanane...Nataka
tuwe na iphone 12
Angelina: ndo ipoje? Hii inanitosha bwana
Raymond: twende bwana (wanapanda gari na kwenda zao)
Rafiki
yake Christina: yaani wanaume yaani kasahau kabisa kuwa ana mchumba jamani nyie
hawa wanaume (anatema mate kisha
anaendelea kuangalia nguo)
0 Comments