SCENE 25: -
(Christina anafika nyumbani Kwa Raymond akiwa amefura kwa hasira)
Christina :( baada
ya kufunguliwa geti anashuka kutoka kwenye gari lake na kumfuata mlinzi getini)
Raymond yuko wapi?
Ramadhani: salamu kwanza bwana…
Christina: unataka kuila au? Au umesikia ndo
itakutoa kwenye umaskini? (Anabenjua
midomo) okay…habari yako?
Ramadhani: Raymond yupo bustanini huko amepumzika…kwani
vipi?
Christina: hayakuhusu (anaondoka na kuelekea bustanini alipo Raymond baada ya hatua chache
sana anafika alipo Raymond) Raymond
Raymond :( anageuka
maana alikuwa amegeukia upande mwingine) naam…
Christina :(
anakaa kiti pembeni ya Raymond) habari yako…
Rayymond: salama…shikamoo
Chrristina: marahaba…za hapa
Raymond: salama…tu...Tupo (anampigia Angelina simu) njoo na (kwa Christina) unatumia kinywaji gani?
Christina: maji Tu...
Raymond: njoo na maji kuna mgeni
Angelina: sawa
Christina: siku hizi Mimi ni mgeni?
Raymond: usichukulie hivyo…Christina…basi nisamehe Kwa
kukuita mgeni
Christina :(
anaguna huku anabenjua midomo) sawa bwana kwahiyo hausigeli kanishinda?
Raymond: umejuaje?
Christina: huu mji mdogo Sana unaweza ukasema
unajificha ila watu wanakuona
Raymond: siwezi kukataa Christina …Kama tayari
umeshajua…basi ni kweli kabisa nipo kwenye mahusiano na msichana wangu wa ndani,
sasa sitamuita msichana wangu wa kazi ni mpenzi wangu
Christina :( anapandwa
na hasira ila anajikaza zisionekane)
Raymond: Na ninampenda Sana kwakweli…nampenda na
ninataka awe mke wangu…
Angelina :( analeta
maji na kumpa Christina)
Christina :(
anayapokea ila kwa makusudi kabisa anaiachia glasi)
Angelina: samahani Sana…
Christina: adabu mbaya (Kwa ukali) unashika maji Kama sijui unashika nini wewe mwehu nini?
Angelina :(
anajisikia vibaya)
Raymond :(
Kwa Angelina) it is okay baby…nenda ndani kalete mengine haina shida
Angelina :( anaondoka
na baada ya muda kidogo analeta maji)
Christina :( anayapokea
Kwa hasira na kuyaweka mezani)
Raymond :( Kwa
Angelina) nenda kaendelee na kazi zako baby
Christina :( anatamani
mpaka kulia)
Angelina :( anaondoka
zake)
Christina: why Raymond...?
Raymond: why nini?
Christina: umeniacha na kuwa na msichana wa kazi?
Raymond; mapenzi Christina…mapenzi
Christina: hiyo sio vizuri jamani
Raymond: naomba unisamehe…ila tangu nimekukuta na Peter
moyo wangu ulikataa kabisa kukusamehe na nilijilazimisha kuwa na wewe tu kwa
sababu baba anataka niwe na wewe…lakini siku nimemuona Angelina nafsi yangu
ilikiri wazi kuwa nampenda sana na siwezi kumuacha milele nay eye ndo kipenzi
changu haijalishi yeye ni nani na anatoka katika familia gani nachojua tu
kwamba nampenda sana na nitafanya kila kitu awe mke wangu...She completes me
and she is the woman of my life
Christina :( anajikuta
anapiga magoti mbele ya Raymond)
Raymond: hapana Christina usifanye hivyo… (Anamnyanyua)no don’t do that please
Christina: umenivisha Pete ya uchumba juzijuzi
tu…kila mtu yupo tayari Kwa ajili ya harusi yetu
Raymond: wataambiwa wataelewa tu
Christina: nini kitatokea Kwa wazazi wangu hiyo
aibu tutaificha wapi?
Raymond: nisamehe Christina naomba unisamehe Sana
Christina: Raymond marafiki zangu wameshashona sare
tayari kabisa Kwa ajili ya harusi…
Raymond: siwezi kuriski furaha yangu ili
uwafurahishe marafiki zako...please understand
Christina; naomba unioe utanipa talaka huko mbeleni
Raymond: dini hairuhusu hata kidogo…we nyanyuka tu Na
ukae upate maji yako…naomba tuwe marafiki…
Christina: Raymond
Raymond: wewe nyanyuka tu…
Christina :(
ananyanyuka na kukaa kwenye kiti) Raymond, amekupa nini huyu binti?
Raymond: hata mimi sijui (anatabasamu kidogo) ila alichonipa namuomba aongeze yaani kama ni
dozi naomba iwe hata mara saba maana najisikia vizuri sana kuwa in love nae…
Christina: iam not joking...Iam being serious
Raymond
Raymond: hata Mimi sitanii…nipo very serious au
unaona nacheka?
Christina: what happened to us? Tulikuwa tunapendana
Sana
Raymond: tusiyazungumzie hayo tena maana umeniuliza
Hilo swali atleast mara arobaini na nimechoka kukujibu ila kama unataka
nikujibu basi ni kwamba ulikuwa unanisaliti mara nyingi sana katika mahusiano
yetu sio mara moja na mara nyingine ulionyesha wazi kuwa unataka pesa zetu…sasa
wewe sio mwanamke nayemtaka
Christina: nakuahidi kuwa nitakuwa ni mwanamke
unaemtaka Raymond
Raymond:umechelewa sana…na sikupanga kwamba eti
hausigeli atakaekuja nitafanya awe mpenzi wangu…huyu dada ana undugu na mpenzi
wa Edmond…can you imagine nilivyokuwa naogopa kumwambia hata Edmond kuwa
nimempenda sana shemeji yake…hata Edmond alidhani nimempenda au nilipanga
kwamba akiniletea msichana nitamtongoza na kumfanya awe hawara jibu ni hapana
sikupanga na wala sikutaka kabisa awe mpenzi wangu ila moyo uliipinga akili…na
akili ikakiri kwamba moyo umeshinda na nipo tayari hata kusimama mbele ya baba
yangu na kumwambia kuwa nina mwanamke nampenda sana na huyo mwanamke ni
hausigeli wangu
Christina :(
anadondosha machozi)
Raymond: hata akinifukuza kwenye hii nyumba ni sawa
nitaenda popote na Angelina as long as nipo na Angelina basi hakuna
nitakachoogopa…
Christina: unadhani baba yako atakubali?
Raymond: I don’t care…nampenda Angelina na hata
mama yangu anajua Hilo tangu mara ya kwanza naanza kuhisi kumpenda sana Angelina
nilimwambia mama na mama akanipa ushauri na support yake
Christina :( ananyanyuka
na kuondoka zake huku Analia) sitaki kukusikiliza tena Raymond… (Anapanda gari lake kisha analiondoa kwa
hasira)
Raymond: sikutaka kumuumiza mtu yeyote…nataka kuwa
na Amani tu…jamani hata iweje siwezi kumuacha Angelina...Nampenda sana (anaingia ndani na kumkuta Angelina anaosha
vyombo anamkumbatia kwa nguvu) mke wangu
Angelina: nimemuona Christina Analia kila kitu kipo
sawa?
Raymond: ndio (anambusu
shavuni) usipike jioni twende tukale nje…
Angelina: we nidekeze tu... (Anacheka kisha anaendelea na kazi yake)
Raymond :(
anacheka kisha anaingia chumbani kwake)
Angelina
:( anatabasamu) Asante Sana Mungu
wangu mwema…naliinua jina lako mfalme…wewe unasatahili sifa zote (anatabasamu kisha anaanza kuimba pambio ili
kumtukuza Mungu wake) nina amani na huyu mwanaume…nampenda sana Raymond
0 Comments