SCENE 26: -
BAADA YA MWEZI MMOJA: -
(Angelina amekaa bustanini peke yake anakunywa
kinywaji chake cha baridi huku anaongea na kipenzi chake kwenye simu. Wakati
anaendelea kuongea Christina anafika mahali pale na kusimama kama sanamu kabla
hajamuita)
Christina
:( anamuita kwa utaratibu kama vile mtu
ambae ana urafiki nae au anataka urafiki nae) Angelina…
Angelina
:( anamalizia kuongea na simu) kata
nitakupigia baadae kidogo
Raymond:
kuna shida gani?
Angelina:
hamna shida kuna mtu tu anagonga geti
Raymond:
si umwambie Ramadhani ndo afungue geti? Umekuwa mfungua geti?
Angelina:
kaenda kuoga…Bwana kata simu mara moja
Raymond:
sitaki mpaka uniambie kuwa unanipenda…
Angelina:
haya nakupenda (anatabasamu)
Raymond:
nakupenda pia (anatabasamu kisha anakata
simu)
Angelina:
abeee…dada Christina karibu…
Christina
:( anatembea hatua chache na hatimaye
anamfikia Angelina)
Angelina
:( muda wote huo anamuangalia Kwa wasiwasi)
Christina
:( anapomfikia anakaa pembeni ya Angelina)
vipi za siku nyingi?
Angelina
:( bado ana wasiwasi) nzuri shikamoo
dada Christina…
Christina:
marahaba… (Anamuangalia Sana usoni kisha
anatabasamu) kumbe pesa nzuri sana
Angelina:
kwanini?
Christina:
umekuwa Mrembo Sana…Raymond anajitahidi Sana kukutunza…yaani hatujaonana mwezi
tu lakini umebadilika Sana
Angelina
:( anacheka lakini bado ana wasiwasi)
dada bwana...Mbona huji siku hizi?
Christina
:( anajichekesha) we kwani hujui kuwa
sina cha kunileta siku hizi au hujaambiwa na bwana wako?
Angelina:
aliniambia tu kuwa mmeachana…
Christina
:( anacheka kidogo) yes…tumeachana
baada ya kukaa katika mahusiano Kwa muda Mrefu Sana na tulikuwa tumebakiza
miezi kadhaa tufunge ndoa ila sijui akaonaje anaona ni bora tu tuachane
Angelina:
dah…Mungu ni mwema atakusaidia na wewe utapata mtu mwingine…
Christina:
hata Mimi naamini kuwa ipo siku na mimi nitapata mwanaume atakayenipenda na
kunithamini
Angelina:
kweli kabisa… (Anaguna kidogo) yaani
nimekaa hap ahata sijakuuliza unatumia nini?
Christina:
maji tu…
Angelina
:( ananyanyuka na kwenda ndani kuleta
maji)
Christina
:( anajisemea moyoni) Kwa akili yako
kabisa unaona Mimi nipo hapa kukupa hongera ya kuniibia Raymond au kuunda
urafiki na wewe? Umechemsha my dear
Angelina
:( anarudi akiwa ameshika glasi ya maji)
karibu maji
Christina
:( anapokea) Asante (anamuangaliia kisha anatabasamu)
Angelina
:( anarudi kukaa alipokuwa amekaa)
Christina
:( anakunywa maji kidogo kisha anarudisha
glasi kwenye meza ndogo iliyopo mbele Yao) unampenda Sana Raymond?
Angelina:
nampenda kweli ni mwanaume anayenipa Amani sana moyoni mwangu…
Christina:
na yeye je?
Angelina:
ananipenda…mi ndo naona hivyo na ananionyesha pia
Christina:
Na huwa mnaambiana kila kitu?
Angelina:
ndio…ananiambia
Christina:
oh…kumbe unajua kuwa ana mwanamke mwingine anamhudumia kwasababu amezaa nae?
Angelina
:( anashtuka Sana) ana mtoto na ana mwanamke?
Raymond huyuhuyu?
Christina:
ndio...mi nikajua kakwambia Mimi nimekuambia tu kirafiki maana kwanza sina
uadui na wewe mama nataka urafiki na wewe na nimeongea na wewe kama vile kimbea
tu kama marafiki wanavyoongea
Angelina:(anashikwa
na hasira sana) yaani Raymond ananidanganya mimi…ananiambia hajawahi hata
siku moja kumpa mimba mwanamke na kama nitabeba mimba mimi ndo nitakuwa wa
kwanza
Christina:
ndo hivyo shoga yangu wanaume ni waongo sana wana maneno mazuri ili wapate
wanachotaka na wakipata ndo utaona ubaya wao…shoga yangu wanaume ni mbwa hawa
jamani
Angelina:
hanikuti hapa…ananidanganya Mimi Kama mtoto…
Christina:
bora tuujiondokee tu shoga yangu maana mwanaume Kama huyo anakudanganya hivyo
siku nyingine anaweza kukudanganya mambo makubwa hata yahusuyo afya yake
Angelina:
kweli dada…. hawa wanaume ni wabaya ndo maana mimi sikutaka kabisa kuwa na
mwanaume yeyote, sitaki anikute hapa ameniudhi sana
Christina:
wewe usiondoke…bwana mwenzio ikijulikana kwamba Mimi ndo nimekuambia
atanichukia Sana
Angelina:
wewe usijali…sitakutaja ila mimi naondoka hapa sitaki kabisa mahusiano
nae…namchukia sana Raymond ameniudhi kumbe nay eye ni muongo ee (anaingia ndani)
Christina
:( anacheka Sana) simple tu wala
sijahitaji nguvu nyingi za ziada nimekuja nimejifanya rafiki nikasema uongo
basi huyoooo anaondoka zake…sasa next plan… (Anatabasamu) lazima niwagombanishe Zaidi na Zaidi
Angelina
:( anatoka amebeba begi lake)
Christina
:( anamuendea na kujaribu kumzuia)
ila mi naona kuwa ungemsubiri tu umuulize anaweza akakuambia ukweli au hata
akakanusha uvumi huu
Angelina:
sina huo muda wa kumsikiliza…amenidanganya mara moja anaweza kufanya hivyo Mara
nyingi atakavyo
Christina:
kweli lakini (kimya kidogo Kama anawaza
kitu) sasa hapa wewe unaenda wapi?
Angelina
:( anafuta machozi maana alikuwa Analia
muda wote tangu amepewa taarifa hizo) popote dada… (Anaondoka)
Christina:(anacheka kwa dharau huku anatikisa kichwa)maskini
pole yake sana…hana akili hata kidogo(haraka
anaingia chumbani kwa Raymond kwa kuwa mlango ule haufungwi inakuwa rahisi
kwake kuingia na kufanya chochote)hapa ni kuanza kuchezesha akili tu ili
wachukiane milele…(anafika chumbani anafungua
bei dogo ambalo Raymond anaweka pesa,anachukua kiasi kingi cha pesa na kuliacha
begi hapohapo kitandani)sasa akija Raymond hapa itakuwa virahisi kwake yeye
kujua aliyeiba pesa ni Angelina na akakimbia kuogopa msala (anacheka sana)nimeua ndege wawili kwa
jiwe moja…najipenda sana…najipenda mimi na akili zangu(anatoka na kuelekea kwa Ramadhani)
Ramadhani
:( Kwa furaha) ah shemela…nilikumisi
Christina
:( anamfikia) acha unafki
wewe…unanimisi au ndo ulifurahi Mimi kuachika na huyo Malaya ambae hana hata
akili vizuri kachukua nafasi yangu
Ramadhani:
shemeji sio kweli kwamba nilifurahi…
Christina:
anyway, sina muda wa kupoteza hapa…kuna jambo nataka unisaidie kama ikiwezekana
Ramadhani:
itawezekana tu we nambie
Christina:
huyo mshenzi nimemdanganya danganya kuhusu Raymond akaondoka mwenyewe…sasa
nataka Raymond akija umwambie kuwa Angelina amekimbia Na ameiba pesa nyingi Sana
Ramadhani:
sawa shemela usijali
Christina
:( anatoa pesa taslimu Kama laki tano)
shika na unifanyie hii kazi vizuri bila kubabaisha
Ramadhani
:( anapokea Kwa mikono miwili) Asante
Sana shemeji na ndo maana mimi nilikuwa
nakupenda wewe huyo maringo mengi na madeko
Christina:
mi naondoka bwana sitaki Raymond anikute hapa
Ramadhani:
haya tutaonana na asante kwa hela ya soda
Christina:
poa… (Anapanda gari lake kisha anaondoka)
Ramadhani: mi nakula tu pesa…nitafanyaje sasa…kumpenda nampenda Angelina
na naona wanaendana kweli na boss ila nifanyeje…sasa nataka hela (anacheka kidogo kisha anaingia ndani kwake)
0 Comments