SCENE 27: -
(majira ya saa kumi na mbili jioni Raymond anarudi
nyumbani akiwa anaonekana kuwa amechoka sana na kazi na mizunguko ya siku ile,
mara baada ya kuegesha gari lake anaingia ndani ili aungane na kipenzi chake.
anaanza kuitia nje ili apate kupokelewa kama ilivyo kawaida yao)
Raymond:
baby….
(Kimya)
Raymond:
malaika… (Anaingia ndani)
(Kimya)
Raymond
:( anashangaa) my love…
(Kimya)
Raymond
:( anacheka kidogo) najua
unajificha…na sijui kwanini unajificha…anyway nimekuzoea basi acha utani my
love mi mwenzio nilikuwa na kazi nyingi sana njoo unipoze mwili na moyo wangu (anacheka kidogo)
(Kimya)
Raymond
:( huku anakaa) Angelina…
(Kimya)
Raymond:(ananyanyuka na kwenda chumbani kwa Angelina)
baby…(hamkuti)ameenda wapi? (anaenda na chumbani kwake) Angelina…. (anakuta droo anayowekea pesa imefunguliwa)
nani kafungua droo yangu (anaangalia kitandani)
mbona box langu lipo kitandani (anafungua
ndani anagundua kuwa pesa zimepungua) kuna mtu amechukuwa pesa zangu…Mungu
wangu isije ikawa mke wangu ametekwa na majambazi wamechukua pesa… (anatoka nje haraka) Ramadhani…
Ramadhani:
naam boss…
Raymond:
Angelina yuko wapi?
Ramadhani:
katoroka…kabeba mizigo yake akaondoka
Raymond:
haiwezekani…Angelina hawezi kunifanyia Mimi hivyo
Ramdhani:
boss unamuamini Sana…unasahau kuwa na yeye ni mwanadamu
Raymond:
sijasahau na wala sio kwamba sijui kuwa Angelina ni mwanadamu na anaweza
akafanya dhambi ila sidhani tu kama anaweza kutoroka na kuniibia pesa zangu
Ramadhani:
makubwa…kaiba pesa?
Raymond
:( hajibu kitu na badala yake anachukua
simu yake na kumpigia Angelina) pokea simu malaika…wangu
Ramadhani:
hawezi kupokea simu maana anajua amefanya dhambi…mtoto mbaya huyu…kwanini
lakini unawaza Sana si umuache aende?
Raymond:
Ni kwamba hujui kuwa Angelina ni mwanamke nimpendae kwa dhati au unataka
kunisumbua akili yangu?
Ramadhani:
duh…pole Sana boss jamani…nakuonea huruma Mimi mpaka natamani kulia
Raymond
:( anampigia simu Edmond simu inaita Kwa
muda na mwisho inapokelewa) brother
Edmond:
wewe umemfanya nini Angelina? Nilitaka nikupigie… yaani wewe umemfanya nini
huyu mtoto?
Raymond:
sijafanya chochote kibaya…. kwani vipi?
Edmond:
Mimi ni kama kaka yako lakini hata siku moja hukuwahi kuniambia kuwa una
mwanamke umezaa nae na unamhudumia
Raymond
:( anashangaa Sana) what are you
talking about?
Edmond:
Angelina yupo Kwa Catherine Analia na aachi kulia anataka kurudi kwao…anasema
umemdanganya na hataki kukuona tena milele
Raymond:
embu nakuja… (Anakata simu na haraka
anapanda gari na kuondoka) my God…
(Anaendesha Kwa muda na baada ya kama dakika kumi
na tano anafika nyumbani kwa Catherine, bila kupoteza muda anaingia ndani)
Catherine:
karibu shemeji yangu…
Raymond:
habari shemeji…
Catherine:
Safi
Edmond
:( anakuja akitokea chumbani) hey…Mond
Raymond:
yes Mond...Nambie…Angelina yuko wapi?
Catherine:
yupo chumbani
Raymond
:( anawaacha hapo na kukimbia chumbani,
anamkuta Angelina amekaa kinyonge sana huku macho yake yanaonekana kuvimba sana)
baby…
Angelina:
usinishike tafadhali …siamini Kama unaweza kuwa ulikuwa unanidanganya muda wote
huu…
Raymond:
hapana Angelina sijawahi kukudanganya kwa chochote nilipokuambia kuwa nakupenda
nilimaanisha kuwa nakupenda Angelina…niliposema kuwa nataka kukuoa nilimaanisha
kweli nataka kukuoa amini tu mpenzi wangu
Angelina:
Na huyo kipenzi chako unayemhudumia…. mwenye mtoto wako…
Raymond
:( anashusha pumzi) sina mwanamke
wala mtoto nje Angelina…sina mwanamke ninayemhudumia ningekuwa nae basi
ningekuambia mpenzi wangu tafadhali niamini…naomba Angelina usiniache ukiniacha
haki ya Mungu tena nitajiua nakupenda Sana mpenzi wangu tafadhali naomba turudi
nyumbani kwetu na tuendelee na maisha yetu kama kawaida
Angelina
:( ananyanyuka) hapana…Mimi sikutaki
tena…Raymond Mimi na wewe mapenzi basi…najuta hata nini kilinifanya nikukubali
umeniumiza sana
Raymond
:( anakuwa mnyonge sana) Angelina…
Angelina:
nataka niondoke na kwenda nyumbani Raymond…sitaki tena nipe mshahara wangu
niende kwa mama na wadogo zangu nilitumwa kuja kufanya kazi na sio kuendekeza
mapenzi… (anaanza kulia) hii ni laana
mama yangu alinituma nije nifanye kazi mimi nimekuja kuendekeza mapenzi…(Analia)nimejuta
Raymond
:( machozi yanamtoka) sio hivyo Angelina
wangu…na sijui ni nani amekuambia uongo huo…na nia yake ni kututenganisha
tusimpe nafasi…Angelina tafadhali naomba unisikilize…
(Edmond na Catherine wanakuja chumbani hapo)
Catherine:
Angella kaa utulie mdogo wangu nakuomba ukae chini kwanza tuongee huku umetulia
Angelina
:( anatii na kukaa chini)
Edmond:
shemeji…hiyo habari uliyoambiwa ni ya uongo…Raymond hana mtoto wala mke nje na
kama angekuwa nae mimi ningejua mimi nay eye hatufichani…
Angelina
:( anaanza kutulia)
Edmond:
huyo aliyekuambia ni muongo sana na ni muuaji anataka kuua penzi lenu na Raymond
anaona kabisa nyie mnapendana sana na anafanya kila kitu ili awagombanishe
msimpe nafasi hiyo…Raymond anakupenda na atabaki anakupenda hivyo
milele…muamini na acha kusikiliza maneno ya watu nje…umesikia shemeji yangu wa
pande zote mbili?
Angelina
:( anaonekana ameanza kuelewa)
Raymond
:( anashusha pumzi na anaachia tabasamu
tulivu)
Angelina:
sawa nimeelewa…lakini Raymond anatakiwa kuniambia ukweli Kama kweli ana mtoto
nje au lah
Raymond:
sina Mimi mtoto…na ninajua kuwa ni Christina ndo amekuambia kuwa nina mtoto nje
Angelina:
ndio...ILA umejuaje kuwa ni yeye?
Raymond:
najua tu maana hata yeye alikuwa anahisi kuwa Nina mwanamke nje na mpaka
akamwambia baba yangu na walimsumbua sana (kwa
Edmond) si unakumbuka
Edmond:
nakumbuka duh kumbe kwasababu ya ile (anacheka
kidogo) …ilikuwa gumzo…
Raymond
:( anamgeukia Angelina) nakupenda Sana
kipenzi changu na ninakuahidi sitakusaliti kwa vyovyote vile…
Angelina:
Asante…mpenzi wangu
Edmond:
ooooh… (Anapiga makofi)
Catherine
:( analeta begi la Angelina) rudi na
mpenzi wako nyumbani kwenu mkayajenge na mpange siku ya ndoa tumechoka
kusubiri…
(Wote wanacheka kisha Angelina na Raymond
wananyanyuka na kuondoka zao)
Catherine: mapenzi bwana Angelina amekuja hapa analalamika ona alivyoondoka
(anacheka)
Edmond :( anacheka pia)
kwakweli mapenzi Yana nguvu Sana (anacheka
Sana)
0 Comments