SCENE 28: -
(Siku ya tatu mara baada ya sakata la Angelina
kukimbia nyumbani Kwa boss wake wa zamani na sasa mpenzi wake, mchana wakati wa
mapumziko ya chakula cha mchana Raymond anaona aende kumtembelea Christina,
anapanda gari lake na ndani ya dakika ishirini anafika Nyumbani kwa kina Christina)
Raymond:
hodi… (Anagonga mlango)
Shangazi
:( anafungua mlango) karibu Sana baba
yangu
Raymond:
Asante, shangazi shikamoo
Shangazi:
marahaba baba hujambo
Raymond:
sijambo…Christina yupo…?
Shangazi:
yupo, nadhani atakuwa chumbani kwake
Raymond
:( anaingia ndani anakaa sebuleni)
naomba uniitie nahitaji kuongea nae
Shangazi:
jamani baba…si mkeo mtarajiwa huyo ingia tu utamkuta
Raymond:
hapana naomba nizungumze nae hapahapa
Shangazi:
ah baba kwani kuna tatizo?
Raymond:
hakuna tatizo…kila kitu kipo sawa
Shangazi
:( anaingia chumbani kwa Christina na
kumuita) shoga yangu Raymond amekuja anakuita kanuna huyo umemfanya nini?
Christina:
ana stress zake tu hana lolote…anikome Mimi
Shangazi:
(anacheka kidogo) anakuita
Christina
:( anatoka na kumwendea Raymond alipokaa)
Raymond…
Raymond:
shikamoo,
Christina:
marahaba karibu…
Raymond:
Asante…
(Kimya kidogo)
Christina
:( anavunja ukimya kwa kumuita msichana
wao wa kazi) dada…embu mletee mgeni juisi (kwa Raymond) si utakunywa juisi?
Raymond:
ofcourse nitakunywa Asante
Msichana
:( analeta juisi na kumpa Raymond)
shikamoo...Shemeji
Raymond
:( anapokea) Asante, marahaba…
Msichana
:( anaondoka zake)
Christina
:( Kwa Raymond) niambie
Raymond:
Christina, mara ya mwisho Mimi na wewe tunaachana naamini kabisa tuliachana
kiroho safi na tukakubaliana tutakuwa marafiki si ndio?
Christina:
ofcourse ulisema tuwe marafiki…na tumekuwa marafiki kwa kipindi hicho chote,
any problem?
Raymond
:( kimya kidogo huku anamuangalia usoni)
yes…kuna tatizo
Christina:
tatizo gani?
Raymond:
unataka kuniambia hujui? i mean comeon Tina yaani wewe unafanya kitu halafu
unasahau?
Christina:
ndo uniambie sijui
Raymond:
nilijua kuwa umekubali kuwa rafiki yangu utatunza furaha na Amani yangu (anakunywa juisi kidogo)
Christina:
unaongea kimafumbo Raymond sikuelewi kabisa…
Raymond:
naongelea kitendo ulichofanya juzi Christina
Christina:
nilifanya nini Raymond? naomba usinilaumu kila mara unapopata majanga Raymond
Raymond:
niliona kwenye CCTV juzi ulivyokuja na ulipochukua pesa zangu
Christina
:( anainama Kwa aibu)
Raymond:
hicho hakikuniuma kitu ulichoniudhi ni kumwambia uongo mwanamke wangu eti nina
mtoto na kuna mwanamke ninayemhudumia…namhudumia nani mimi? Yaani…ukahakikisha
mpenzi wangu ameondoka nyumbani kwangu yaani dah (anasikitika kidogo) isingekuwa Catherine na Edmond sijui ningempata
wapi mke wangu
Christina:
eti mkeo, umesahau au unataka kujifanya umesahau kuwa umenichumbia na mahari
umenitolea na hapa kila mtu anajua wewe ni mume wangu mtarajiwa, nina haki ya
kufanya kila kitu nilichofanya
Raymond:
huna haki yeyote Christina Mimi ni mwanadamu na mwananchi mwenye uhuru wa
kufanya chochote nachotaka, nimempenda Angelina na ni yeye ndo nitamuoa
Christina
:( anaguna) kwahiyo wazazi wako
wanajua?
Raymond:
hawajui ila watajua siku si nyingi haitakuwa kazi kuwaambia
Christin:
nyie wanaume kwanini mpo hivyo? Umenipa matumaini miaka yote huu halafu mwisho
wa siku unaniacha solemba
Raymond:
acha lawama ili mimi ndo nionekane nina makosa ili makosa yako
niyasahau…umefanya kosa kuniingilia na huku tulikubaliana kuachana
Christina:
uliniambia kuwa unaniacha ila mimi sikuwa tayari kwahiyo hatukukubaliana wala
nini ni wewe ndo uliamua
Raymond:
it’s about my heart and what I want…nimempenda Angelina it just happened,
sikupanga eti msichana aje na mimi nimpende na kumfanya awe mpenzi wangu…mimi
na wewe tuliachana kabla hata uchumba wetu haujatangazwa
Christina
:( anacheka) kwanini hukukataa
mapema?
Raymond:
Kwa wakati huo sikuwa na nguvu maana I was not in love…now iam madly in love
with my housegirl na hakuna atakae weza kunitoa kwenye dimbwi hilo sio wewe
wala baba yangu…sikuoi and that is final
Christina:
Raymond hiyo sio haki
Raymond:
huruhusiwi hata kidogo kuniingilia katika mahusiano yangu na mpenzi
wangu…nakuonya na naomba unielewe
Christina:
Raymond
Raymond
:( ananyanyuka na kuondoka zake)
Christina:
Raymond bado hatujamaliza kuongea
Raymond
:( anaondoka zake)
Christina
:( anakasirika Sana)
Shangazi
:( anakuja) nini shoga yangu
Christina:
anadhani ataniacha kizembezembe? Amechemsha mshenzi huyu yaani anipotezee muda
halafu aje aniache eti iam in love with my housegirl…Raymond…unataka
kuninyang’anya tonge mdomoni…sitakuruhusu, akitaka kuniacha labda aniue lakini
hivihivi…asahau
Shangazi:
kumbe kijana mjinga huyu ee
Christina:
amekuja kunionya nisirudie kumgombanisha na mpenzi wake
Shangazi
:( anaguna) amependa
Christina:
ni kwamba sitaruhusu kabisa yeye na huyo mwanamke wawe na mapenzi ya Amani
yaani nitawasumbua mpaka wachanganyikiwe, mimi ndo mke mtarajiwa wa Raymond...Hakuna
kinyago yoyote atakayeruhusiwa kuwa na mahusiano na Raymond…
Shangazi:
ila shoga yangu una dhambi unampenda mwanamume mwingine lakini unamtaka Raymond
unajua hata sikuelewi
Christina:
nampenda Peter Sana ila namtaka Raymond maana yeye ni atm wangu na
nitahakikisha kuwa ATM inabaki kwangu na hakuna mtu mwingine anaimiliki
Shangazi:
halafu unajua Raymond analijua Hilo
Christina:
atakoma mwenyewe…mi nachoangalia ni pesa
Shangazi:
chagua moja…Peter au Raymond
Christina:
wote maana Nina shida nao wote (anacheka
kwa kejeli)
Shangazi:
mtoto mbaya wewe
Christina:
lazima nijue namfanyaje raymond kabla haijawa too late
Shangazi:
pambana mimi nipo ndani (anaingia
chumbani)
0 Comments