SCENE 29: -
(jioni njema na Ya kuvutia kuna hali Fulani ya
utulivu unaendelea, jua kwa mbali linaanza kuzama, kila kitu kinaonekana katika
utulivu, watu wanatoka katika mahangaiko yao ya kila siku, Raymond na Angelina
wamekaa bustanini, wanafurahia faragha yao)
Raymond
:( anamshika Angelina mashavu) yaani
siamini Kama tupo wote Mimi na wewe mpenzi wangu maana dah…acha tu
Angelina
:( anacheka kidogo) usijali mpenzi
Mimi na wewe milele penzi letu litadumu milele
Raymond
:( anamuangalia kisha anatabasamu)
sijui ulikuwa wapi miaka yote kwanini hukutokea siku nyingi uuponye moyo wangu?
Maana nilikuwa nateseka mwanamke niliyekuwa nae nae hakuwa mtu mzuri hakuwa na
mapenzi na mimi
Angelina:
nimekuja sasa na ninaahidi sitakuacha labda wewe uniache
Raymond:
unasema kweli baby?
Angelina:
nakwambia kweli
Raymond
:( anamuangalia usoni) nakupenda Angelina
wangu wewe ni mwanamke wa ndoto zangu
Angelina:
Na wewe ni mwanaume wa maisha yangu nakupenda na ninakuheshimu sana Raymond….
Raymond:
nataka nikawaone wazazi wako…ulisema una mama tu huna baba
Angelina:
ndio
Raymond:
nataka nikamuone mama yako mpenzi wangu
Angelina:
nitafurahi Sana mpenzi wangu…
Raymond:
hivi umeshawahi kumwambia kuwa una mahusiano na mimi?
Angelina:
bado sijamwambia
Raymond:
kwanini?
Angelina:
Nitamwambia, ila tu naona Kama hatafurahi akisikia kuwa nimekuja mjini badala
ya kufanya kazi mimi nimeamua kuwa na mwanaume
Raymond:
lakini Mimi si mwanaume yeyote Angelina Mimi ni mwanaume ninayekupenda kwa
dhati na lengo langu ni kufunga ndoa na wewe
Angelina:
sijakataa na wala sibishi juu ya nia yako lakini acha kwanza tukae kidogo mama
tutamwambia tu
Raymond:
au una mtu wako nyumbani kwenu?
Angelina:
hapana sina mtu wala nini nipo Mimi na wadogo zangu na mama yetu sina mwanaume
Raymond:
sawa (kimya kidogo huku anamuangalia Kwa
uchu kidogo)
Angelina:
vipi? Mbona unaniangalia hivyo?
Raymond:
kila siku huwa naombea kurudi nyumbani mapema ili nikuone huwa upo moyoni
mwangu na akilini mwangu kila saa mpenzi wangu
Angelina
:( anacheka Kwa aibu kidogo)
Raymond
:( anamsogelea na kutaka kumbusu mdomoni)
Angelina
:( anaogopa)
Raymond:
usiogope Angelina…
Angelina:
hapana unataka kufanya nini Raymond?
Raymond:
nataka tu kukubusu na si vinginevyo
Angelina:
lakini haya mambo tuliongea na kukubaliana kuwa hatutakuwa tunayafanya mpaka
siku tutakapooana
Raymond:
hata busu? Mimi nilikubali kuwa hatutafanya tendo la ndoa mpaka tuoane lakini
sasa hata busu…sisi ni wapenzi Angelina sio kaka na dada
Angelina:
kila kitu kisubiri Raymond…nilijiahidi kuwa mwanaume atakaekuwa wa kwanza ndo
atakuwa mume wangu
Raymond:
Mimi nitakuwa mumeo Angelina
Angelina:
mpaka siku ifike ndo nitalala na wewe
Raymond:
acha hizo baby Mimi nimekuahidi nitakuoa nakupenda Angel
Angelina:
umeniahidi utanioa ndio ila sina uhakika juu ya maneno yako je kama
unanidanganya?
Raymond:
siwezi kukudanganya Angelina nimeshakuonyesha upendo na nia yangu kwako,
nimeshakutambulisha kwa mama yangu huamini nini Angelina
Angelina:
kunitambulisha kwa mama yako sio tija Raymond unaweza kunitambulisha na mwisho
ukaniacha solemba…mfano Christina wewe si mpaka watu walikuja kushuhudia
mnavalishana pete ya uchumba hapa? Lakini mbona Leo hii umemuacha?
Raymond:
usijifananishe na Christina mapenzi yetu yalishaisha…
Angelina:
ulimaliza mapenzi na mwanamke uliyempenda miaka mingi sana sembuse mimi
uliyenijua juzi tu…, mimi kiukweli subiri kwanza ukinioa tutafanya tendo la
ndoa mara nyingi unazotaka kwa sasa hapana
Raymond:
hapana Mimi nataka busu tu
Angelina
:( ananyanyuka Kwa jazba) au ndo
maana unaniongelesha maneno mazuri kumbe lengo lako utembee na mimi kisha
uniache kama Christina?
Raymond:(ananyanyuka na kujaribu kumshika) calm
down baby…sio nataka kukuacha na wala sina hiyo nia mimi ni mwanaume nina
mahitaji yangu ya kimwili lakini kama hauko tayari sijakulazimisha Angel
unaweza tu ukaacha sio lazima na pia mimi mbona nilikubaliana na wewe
Angelina:
hapana Raymond naogopa maumivu ya moyo Nina moyo mdogo sana siwezi kuvumilia
siku ukiniacha tena baada ya kuniachezea usichana wangu na kuniacha
Raymond:
si basi Kama umekataa?
(Huku getini Ramadhani anasikia majibizano Yao)
Ramadhani
:( anacheka) enhe!!!!leo ndo leo
wameanza kugombana wenyewe humu ndani(anacheka)sijui
watakuwa wanabishana nini sijui Yanga na Simba au namba za nida zinatoka lini
maana duh, inshu ya nida iko moto mpaka watu wanakaa kwa kupaniki (anacheka sana) embu ngoja nikawacheki (anaenda bustanini walipo Angelina na Raymond)
leo pamenuka halafu (anaangalia vizuri)
mwanamke nae mbabe
Raymond:
Angelina ya nini marumbano mpenzi Kama haiwezekani hakuna anayekulazimisha Kwa
lolote kufanya usilolitaka
Angelina:
ndo maana unaniambia unanipenda kumbe unawaza mambo yako ya ajabu
Raymond:(anashangaa) ningekuwa wa hivyo Angelina
kwa muda tuliokaa kama wapenzi ningetaka ningekubaka tu humo ndani na hakuna
ambae angejua na usingenifanya lolote...nakupenda na ninakusikiliza unachotaka
basi hakuna mjadala wa kuumiza kichwa
Angelina
:( anazidi kuwa mbishi maana akili yake
imeshaamini Raymond hampendi anataka kumchezea tu) hunipendi Raymond si
useme tu wazi kuwa naomba tusaidiane maisha mimi kwa kuwa sasa hivi sina mpenzi
naomba nitimize haja za mwili wangu kwako basi (Analia) lakini sio kukaa unanidanganya
Raymond:
sipendi kuona machozi yako Angelina na isitoshe tumekaa hapa nje tukiwa na
lengo la kupumzisha akili zetu na miili yetu baada ya kazi nyingi za siku hii
lakini wewe unataka kunichanganya tu sijui lengo lako ni nini
Ramadhani:
ngoja nikawaulize naona watu wanalia tu (anaenda)
jamani za jioni
Raymond:
salama vipi?
Angelina
:( anafuta machozi) salama shikamoo
Ramadhani:
marahaba, kuna tatizo?
Raymond:
Ni kutoelewana tu kidogo baina yangu na mwenzangu…. hakuna tatizo
Ramadhani:
basi poa, maana nimesikia sauti mpaka getini kule nikaona labda mambo yamekuwa
mambo
Raymond:
hapana
(Ramadhani anaondoka, huku Raymond anajaribu
kumbembeleza mwenzie anayeonekana kukataa kabisa kumsikiliza)
Raymond:
basi nisamehe, sitazungumzia tena mapenzi na tendo hilo tena nisamehe mpenzi
wangu
Angelina
:( anamuangalia kisha anakumbatia)
sipendi kugombana na wewe Ray
Raymond
:( anamkumbatia pia) nakupenda Angelina
Angelina:
nakupenda Raymond
Raymond: wewe kumbe mkali ee (Anacheka)
Angelina: (anacheka)
0 Comments