SCENE 30: -
(Asubuhi majira ya saa tano, Angelina yupo
njiani anaonekana kuwa ametoka sokoni kwani ana kikapu kilichojaa mbogamboga,
akiwa njiani anakuwa anaongea Na simu)
Angelina
:( anacheka) yaani hapa nilipo ndo
natoka sokoni Leo nimechelewa Sana kutoka sokoni
Raymond:
ulikuwa unafanya nini muda wote?
Angelina:
Leo nilikuwa Nina mahemezi mengi Sana
Raymond:
yaani wewe (ananyamaza kidogo)
Angelina:
sasa mbona huongei?
Raymond:
nakumbuka hasira zako Jana (anaguna)
nilihisi utanishushia kipondo
Angelina:
ah wapi siwezi kufanya hivyo sijalelewa hivyo
Raymond:
vizuri Sana my dear
Angelina:
Leo nitakupikia chakula ukipendacho…nimenunua nazi Kama ugomvi
Raymond
:( anacheka Sana) eti Kama
ugomvi…sasa unagombana na nani mimi nipo kazini labda ukagombane na Ramadhani
Angelina:
nagombana na wewe
Raymond:
Mimi utanionea maana sina hata hizo nguvu za kugombana Na mtu
Angelina
:( anacheka) Kwahiyo unaniletea
zawadi gani jioni
Raymond:
midoli
Angelina:
Akha!!Sasa Mimi midoli ya kazi gani jamani kwani Mimi mtoto?
Raymond:
ndio wewe mtoto…. nakuitaga baby unaitika wewe unajua maana ya baby?
Angelina:
nitajulia wapi sikusoma?
Raymond:
umeanza sasa kujishusha unanikera Angel
Angelina:
ndo ukweli huo
(Gari ndogo aina ya Mark II linakuja kuegesha
pembeni yake)
Angelina:
embu ngoja nifanye kazi za jamii
Raymond:
nini tena?
Angelina:
nahisi kuna watu wamepotea njia wanataka kuniuliza kitu
Raymond:
poa we fanya kazi za jamii ila ukimaliza tu naomba unipigie tena napenda
kushinda nasikia sauti yako
Angelina:
(anacheka kidogo) sawa
Raymond:
nakupenda Sana Angelina
Angelina:
nakupenda pia
Raymond:
bye
Angelina:
bye (anakata simu kisha analisogelea gari
lile)
(Kuna mtu anashusha kioo na Angelina anapoangalia
vizuri anaona ni Christina)
Angelina:
shikamoo dada Christina
Christina:
marahaba…mbona unatembea Kwa miguu bwana’ako hajakununulia gari?
Angelina
:( anacheka kidogo) bado
Christina:
panda nikupe lifti mpaka kwako, maana ishakuwa nyumba yako
Shangazi
:( nae yupo kwenye gari) hongera yake
Angelina
:( huku anapanda kwenye gari)
shikamoo mama
Shangazi:
marahaba
(Christina analiondoa gari kwa kasi kubwa mahali
pale)
Angelina
:( hana Amani)
Christina
:( anamuangalia kupitia kioo cha mbele)
vipi Angelina mbona unaonekana huna Amani? Shida nini?
Angelina:
hapana dada mbona Mimi Nina Amani tele
Shangazi:
vizuri
Christina
:( anaipita nyumba ya Raymond)
Angelina:
dada Mimi nimefika
Shangazi:
eti nimefika…kwako pale?
Angelina:
kwani nini tatizo?
Shangazi:
mwisho wa ubaya ubaya tu wewe umeiba mume wa mtu halafu unachukulia poa…tunakupeleka
tunapotaka sisi
Angelina:
(anajaribu kupiga kelele)
Shangazi
:( anamuonyesha kisu) nitakutoa
utumbo sasa hivi kimya…(anafyonza)
Christina
:( anacheka Sana) muoga kweli halafu
vya watu unakula tena bila uoga mshenzi mkubwa
Angelina:
nisameheni
Shangazi:
tumeshakusamehe lakini ni lazima tukuonyeshe kitu ili ukome usirudie tena mwehu
wewe
Angelina:
Kama ni Raymond mchukueni tu mimi roho yangu niachieni jamani mimi nategemewa
na familia yangu
Christina:
familia yako ilikutuma uje utafute riziki na sio kutafuta mabwana za watu
mshenzi wewe
Angelina:
tafadhali nisamehe Sana dada Christina
Shangazi:
lazima ufundishwe adabu…
(Gari linaenda kwa mwendo wa kasi sana)
Angelina
:( anapiga kelele) nawaomba Sana
msinidhuru Mimi jamani nitaachana na Raymond, ni kweli nimefanya kosa kwa
kuingilia mapenzi ya watu nisameheni
Christina:
kila afanyae kosa ni lazima aadhibiwe hivyo basi ulifanya kosa lazima uadhibiwe
Angelina:
nisamehe Nina mama na wadogo zangu ambao wananitegemea sitaki kufa
Shangazi
:( anamzaba kofi moja kubwa la kutosha)
kelele…ulitumwa ufanye umalaya?
Christina:
embu niambie umelala nae mara ngapi?
Angelina
:( huku Analia Sana) sijawahi kulala
nae haki ya Mungu tena sijawahi haki ya Mungu siwadanganyi
Shangazi:
muongo huyu…
(Wanafika katika jumba moja chakavu ila lina
madirisha na milango na bati)
Shangazi:
tumefika
(Christina anashuka kisha anamvutia Angelina
nje na kumsukumia ndani ya jumba hilo chakavu)
Angelina
:( Analia Sana na anakumbuka kuwa
ameshika simu anajaribu kumpigia Raymond)
Shangazi:
wewe jaribu uone (anamnyang’anya simu)
pambana na hali yako Malaya wewe
Angelina
:( Analia Sana)
Christina:(anacheka sana) kutesa kwa zamu, yaani
mimi Raymond ananiaacha mimi eti (anamuiga
Raymond) I am in love with my housegirl…. Loh!!!Yaani wewe takataka ni wa
kunipokonya mimi tonge mdomoni na sasa sitakuacha hivihivi ni lazima nikuue
Angelina:
hamna dada nisamehe…nimekosa (anapiga
magoti) usiniue…
Christina
:( anatoa kitu Kama mkanda kutoka kwenye
mkoba wake na kuanza kumchapa Angelina mara nyingi sana)
Angelina:
mama, nakufaaaa (Analia Kwa nguvu Sana)
Shangazi:
kufa Malaya wewe
(Wanamchapa Kwa zamu mpaka Angelina anapoteza
fahamu)
Christina:
shenzi Sana… (Kwa shangazi) tufunge
milango tuondoke tutarudi baadae
(Wanafunga milango na madirisha kisha wanaondoka
wakimuacha Angelina bado amezirai)
0 Comments