SCENE 4: -
(Siku ya pili
tangu Raymond akabidhiwe ofisi na utawala wa hospitali ya wazazi wake, amekaa
ofisini kwake akiendelea na kazi zake za asubuhi. wakati huo huku nje Christina
anafika ofisini hapo na anapofika anataka kila mtu ajue kuwa amefika hapo,
maana anafanya vituko mbalimbali ikiwemo kuongea na simu kwa nguvu kama
mwendawazimu)
Christina :( anapita
kwa watu bila kuwasalimia)
Pendo :( ananong’ona)
yaani huyu dada ...Yaani hana salamu hivi ni nani?
Rachel: nasikia ndo mchumba wa boss wetu
Pendo: loh!!! Mbona anaonekana mtata
Rachel: acha tu ndugu yangu embu tufanye kazi
mengine hayatuhusu
Pendo: kwakweli shoga tufanye yetu (anacheka)
Christina :( anaenda
mpaka ofisini kwa Raymond na bila kupiga hodi anaingia)
Raymond: (anashangaa kumuona) Christina...Vipi?
Christina: poa…habari za kazi (anakaa karibu kabisa na Raymond)
Raymond: nzuri…tu (hamuangalii)
Christina: (analazimisha
Raymond amuangalie) Raymond…hiyo ndo tabia gani mkeo mtarajiwa anaingia na
wewe huna muda hata wa kumuangalia
Raymond: Christina please...
Christina: (anamfokea)
huna adabu Raymond
Raymond: sikiliza nikwambie kitu unaweza ukawa
umenizidi umri lakini Mimi ni mwanaume na natakiwa kuheshimiwa tafadhali naomba
heshima iwepo kwa kiasi kikubwa nisije nikajikuta nakukinai na kuacha kutimiza
baba anayoyataka kwanza kwa uliyonitendea ilinipasa nikuache kabisa badala
unitii wewe unaniletea ubabe
Christina: (anamuangalia
usoni) mbona siku hizi una hasira Sana…simu zangu hupokei, yaani kila kitu
kimebadilika Sana Raymond kwanini lakini?
Raymond: wewe umekuja Kwa heri au Shari niambie
kabisa ili na mimi nijiandae
Christina: najua nilikusaliti Raymond lakini huna
sababu ya kunichukia hivyo
Raymond :(
ananyanyuka) sio usaliti tu Christina…mambo mengi Sana yananifanya
nisitamani kuwa mumeo
Christina: nini Zaidi Raymond, au Kwa kuwa sijui
kupika mpaka Leo hii Nina miaka 36?
Raymond: labda na hiyo ni sababu moja wapo ya
kunifanya nisitake kukuoa lakini pia…
Christina :( anamkatisha)
basi yaishe mume wangu mzuri jamani (anajichekesha)
miaka sita tupo kwenye mahusiano leo ndo utake kuniacha baba tupo dakika za
mwisho jamani tuoane unataka kuniacha Raymond wangu
Raymond :(
anakaa kwenye sofa) by the way Christina Mimi na wewe tuna mazunguzo marefu
Christina :( ananyanyuka
kwenye kiti na kwenda kukaa nae kwenye sofa) kuhusu nini mume wangu
Raymond: muafaka wa mahusiano haya tuliyonayo
Christina: yamefanya nini jamani?
Raymond: nataka tuachane Christina…nakuomba
Christina: kisa nini Raymond (machozi yanamlenga) Kama kuhusu usaliti si nishakuomba msamaha
yaishe Raymond… (Machozi yanamtoka)
nisamehe Raymond mpenzi...jamani si usahau baby hay ani mapito tu jamani
kipenzi (anajaribu kumkumbatia)
Raymond; Christina please
Christina: haki ya Mungu tena Raymond nitajifunza
kupika nitakuheshimu sitakaa kila saa naanzisha ugomvi na wewe, Raymond…nisamehe
mwenzio
Raymond: hapana Christina hata mimi kukuacha sio
kwamba napenda ila Christina hatuwezi kuwa pamoja tena Zaidi kama mke na mume,
mawazo yetu hata ndoto zetu hazifanani
Christina: nakuahidi mume wangu (anapiga magoti mbele yake) nitabadilika
usiniache Raymond…nakuomba baba…nisamehe (anakunja
mikono Kama mtu anaeomba kanisani) usiniache Raymond, nakuomba baba
Raymond :( kimya
kidogo huku anamuangalia usoni na anaonekana kama mtu anaetafakari jambo Fulani)
Christina: nisamehe baba yaishe, ndoa yetu
imeshatangazwa
Raymond: nyanyuka…
Christina :( ananyanyuka)
Raymond: nakupa nafasi ya pili, naomba ujirekebishe
Christina: nitafanya hivyo Raymond
Raymond: futa machozi (anamtolea tishu) acha kulia
Christina :(
anamkumbatia) nakupenda Raymond wangu tafadhali kamwe usije ukaniacha mume
wngu wewe ni wangu milele na milele mpaka pale kifo kitakapotutenganisha
Raymond: ukiniahidi kuwa utaacha tabia yako ya
uzinzi, maana kwa wanaume hujambo Christina na pia ukiniahidi kuwa utaniheshimu
basi tutakuwa pamoja siku zote
Christina: mengine tuvumiliane tu
Raymond: jirekebishe
(Kimya kidogo
huku Raymond anarudi kukaa kwenye kiti alichokuwa amekaa mwanzoni)
Christina :( anamkaribia)
kwahiyo baby...Umenisamehee
Raymond: ndio embu naomba tujaribu tena huu
uhusiano tuone unaenda wapi
Christina: sawa mpenzi nakuahidi kuwa sitakuangusha
kamwe
Raymond: naomba iwe kweli na si vinginevyo naomba
sana, kama haitakuwa hivyo itanilazimu kukuacha bila kukupa nafasi ya pili
Christina: sawa nimekuelewa mume wangu naahidi
nitakuwa na wewe na nitakuwa msikivu pia usijali kwa hilo
Raymond: sawa haina shida…
Christina: twende shopping my love
Raymond: yaani wewe unaona kabisa ndo kwanza
asubuhi na nina kazi nyingi sana hapa, halafu wewe unafikiria tu shopping embu
jaribu kubadilika halafu hiyo tabia yako ya matumizi makubwa ya pesa jaribu kuibadilisha
sio nzuri
Christina: Na wewe mtoto wa kisukuma unapenda kweli
kukasirika sijui kwanini yaani utaniudhi bwana
Raymond: sio kukasirika nakwambia tu wala sijakasirika
Christina: poa kwakuwa una kazi nyingi ngoja
nikuache
Raymond: poa baadae
Christina :( anasimama
kisha anambusu mdomoni) baadae baby...
Raymond: poa…
Christina :(
anaondoka zake)
Raymond :(
anabaki anaendelea na kazi zake) huyu mwanamke huyu yaani sijui tu maana
dah!!!sio kwa uvivu na kupenda pesa huko…eeh…(anafumba macho)Mungu nisaidie nipate mwanamke ninayemtaka kila siku
nakuomba hicho hicho maana mpaka sasa
umenipa kila kitu kasoro mwanamke atakayenifaa atakayenisaidia kuzifikia ndoto
zangu ,nataka mwanamke mwenye hofu yako Mungu wangu na si vinginevyo,nataka
mwanamke asiye kunywa pombe,mwenye kujua kuujenga mji na si kujifikiria
mwenyewe,Mungu nataka mwanamke asie mzinzi,nataka mwanamke mwenye mapenzi ya
dhati na mimi na si mapenzi na pesa na mali za familia yangu,Mungu ulisema
ombeni nanyi mtapewa bisheni nanyi mtafunguliwa,kama ulivyowafungulia Paulo na
Sila gerezani naomba Mungu na mimi unifungulie hivyohivyo,nina kila kitu naomba
mwanamke Mungu wangu…naomba mke Mungu wangu Christina sio mwanamke ninayemtaka
nilisema tangu siku ile namfumania christina sio mwanamke kwanza haniheshimu
saa nyingine ananitukana mbele za watu (anafumba
macho kama mtu anayesikilizia maumivu Fulani) embu fikiria mimi Raymond natukanwa
na mwanamke mbele za watu saa nyingine kwasababu nimemnyima pesa au sina pesa
huyu ni mwanamke kweli Mungu wangu embu niangalie na mimi
Sekretari :( anagonga
mlango)
Raymond: karibu…pita mlango uko wazi
Sekretari :(
anaingia) habari za kazi boss
Raymond: salama kwema
Sekretari: nimeleta faili uliloniagiza
Raymond: Asante tafadhali kaendelee na kazi
nikimaliza kuliangalia nitakuita
Sekretari: sawa boss (anaondoka zake)
0 Comments