SCENE 31:-
(Siku
inaonekana kwenda ukingoni, jua kwa mbali linaanza kuzama na taratibu watu
wanarudi makwao kupumzika mara baada ya mizunguko ya siku nzima, Raymond nae
anajisogeza taratibu kurudi nyumbani kwake, akiwa njiani kuna maswali
anajiuliza sana)
Raymond: Angelina tangu asubuhi ile nimetoka
kuongea nae, sijamsikia kabisa sijui kuna nini, na hivi leo nilikuwa nina kazi
nyingi sikupata kabisa nafasi ya kuja kupata chakula cha mchana na mpenzi wangu,
au atakuwa bado amekasirika kuhusu ile juzi? anyways ngoja nifike nyumbani
nitamuuliza vizuri, hatuwezi kushindwana nae (anaendesha gari lake na baada ya hatua chache anafika nyumbani, anapiga
honi kuomba kufunguliwa geti)
(Hakuna anayetokeza)
Raymond :( anajaribu
Kwa mara nyingine)
(Hakuna majibu)
Raymond :(
wivu unaanza kumpanda) isiwe kuwa wapo ndani pamoja wanafanya Yao…haki ya
Mungu nitamuua Ramadhani (anashuka na
kwenda kufungua geti mwenyewe)
Ramadhani :(
anatokea akiwa amevaa bukta Na vesti)
Raymond :( anajikuta
anapandwa hasira) wewe Ramadhani ulikuwa wapi muda wote?
Ramadhani: nilikuwa naoga boss wangu
Raymond: una uhakika? Angel yuko wapi?
Ramadhani: mi si nilijua upo nae boss
Raymond: nipo nae kivipi?
Ramadhan: tangu ameondoka asubuhi hajarudi
Raymond: unajua unachokiongea Mimi sikielewi
unamaanisha nini Angel hajarudi toka asubuhi?
Ramadhan: haki ya Mungu tena nakuambia…alitoka
kwenda sokoni na akaniaga kuwa anaenda sokoni ila atakuja ofisini kwako
kukusalimia…hakurudi nikajua labda ndo kaja huko kwako
Raymond: hapana hakuja…
Ramadhani: leo hujarudi nyumbani hiyo ikanifanya
niamini upo nae
Raymond :(
anaonekana kuchanganyika) Mungu wangu ngoja nimpigie dada yake (anajaribu kumpigia Catherine) Catherine
(Simu inaita mwisho inapokelewa)
Raymond: shemeji…. mdogo wako yupo huko?
Catherine: hapana…kwema lakini Shem?
Raymond: kwema
Catherine: amekimbia tena? Huku hayupo
Raymond :( anaweka
mikono kichwani ishara ya kuchanganyikiwa) Mungu wangu…atakuwa wapi huyu
jamani?
Catherine: kwani vipi? Kakimbia au?
Raymond: hapana…yaani sijui
Catherine: ngoja niwasiliane na familia yake
Raymond: si watachanganyikiwa Sana?
Catherine: sasa asipokuwepo kwangu unadhani atakuwa
wapi?
Raymond: Mungu wangu…sijui basi sawa waulize au
sijui tuache kwanza mama yake si unajua ana presha tusije tujasababisha makubwa
Catherine: yaani…anyway sawa…ngoja nitafute njia
kujua Kama amefika nyumbani au lah naweza kwenda kumuuliza hata rafiki yake
Raymond: yupo hapa hapa Dar?
Catherine: hapana…
Raymond: okay shemeji fanya unavyoweza
Catherine: sawa…ila naomba utulie
Raymond: sawa shemeji yangu (anakata simu)
Ramadhani: sasa sijui yuko wapi?
Raymond :( anaonekana
amekosa nguvu kabisa) wewe hukumgundua labda Kwa habari ya marafiki?
Ramadhani: hapana kwanza alikuwa hana marafiki
Zaidi ya yule dada uliyemuaweka Kwa ajili ya kumtengeneza nywele kila mara
akihitaji kutengeneza nywele…
Raymond: labda kaenda Kwa huyo dada
Ramadhani: labda
Raymond :(
anaiangalia namba ya yule dada na kuipigia)
(Simu inaita Kwa sekunde kadhaa kisha inapokelewa)
Raymond: nambie mambo vipi?
Dada: poa boss kwema?
Raymond: dah…kwema
Dada: nambie boss wangu
Raymond: Angel upo nae?
Dada: hapana boss…sijamuona tangu siku ile nimekuja
kumsuka siku ambayo mlikuwa mna mtoko jioni yake
Raymond: dah!!Poa hamna noma, Asante (anakata simu na kumgeukia Ramadhani) dah
hayupo…Angel jamani upo wapi mpenzi wangu…
Ramadhani: labda alichukia ile juzi mlipogombana
Raymond: hapana mbona tulikuwa vizuri hata mpaka Leo
asubuhi?
Ramadhan: sasa imekuwaje?
Raymond :( anajisikia
kuchoka) Mungu wangu
Ramadhani :( analeta
kiti haraka na kumpa akae) boss kaa tafadhali usije ukaanguka
Raymond :(
Machozi yanamlenga) sijui kakimbia na mwanaume mwingine
Ramadhani: boss acha kuwaza huko jamani…atakuwepo
tu sehemu tu…au karudi kwao labda kakumbuka
Raymond: labda... yaani sijui mwenzenu...Sijui ana
shida gani (anaonekana kuchanganyikiwa)
Ramadhani: tulia boss
Raymond :( anajiinamia)
sijawahi kupenda mwanamke Kama ninavyomependa huyu mwanamke jamani...Yaani hata
Christina sikuwahi kumpenda hivi, can you imagine huzuni iliyo moyoni mwangu
sasa hivi sijui Kama yupo au kakimbia na mwanaume au katekwa, au kauawa sehemu
(machozi yanaanza kumtoka) sijui yuko
wapi
Ramadhani: boss (anampigapiga kifuani) jikaze wewe ni mwanaume unatakiwa ujikaze na
haya yote najua inatia huzuni hujui mwanamke wako yuko wapi ila hauna budi
kujikaza
(Simu ya Raymond
inaita na haraka anapokea)
Raymond: shemeji…
Catherine: nimempigia rafiki yake nyumbani hayupo
Raymond: Oh My God!!!
Catherine: tulia shemeji yangu atapatikana tu
Raymond: hapa sijui yuko wapi, sijui hata Kama ni
mzima au kafa, sijui kama kala au hajala na kama amekula nini, yaani sijui chochote
jamani Angel (Analia)
Catherine: shemeji tulia jamani na usiwaze huko
atapatikana tu, ngoja nije (anakata simu)
Ramadhani: tulia
Raymond :( anaonekana
Kama mtu aliyechanganyikiwa) Ramadhani jamani…mwenzenu Angel wangu yuko
wapi…Angelina wangu malkia wa himaya yangu uko wapi kipenzi changu
Ramadhani: boss, Angelina atapatikana
(Raymond anasikitika Sana, na hajizuii kulia
kukosekana kwa Angelina kumemchanganya sana)
0 Comments