SCENE 32: -
(Usiku huohuo,
Raymond anafika nyumbani Kwa wazazi wake akiwa anaonekana amelia sana maana
macho yake ni mekundu sana na yamevimba, anapofika mama yake anamuona kwa
dirishani hivyo anatoka nje kumpokea)
Mrs.Bembele: baba…umenipigia simu unalia Sana,
mwanangu nini?
Raymond: Angelina…
Mrs.Bembele: kafanyaje? Tena? (Anaingiwa wasiwasi)
Raymond: sijui yuko wapi tangu asubuhi hajulikani
alipoenda, nimemtafuta pote mama hayupo, sasa sijui yuko wapi Na anafanya nini,
sijui yupo Kwa mwanaume…Mimi sielewi
Mrs.Bembele: usiweke wivu baba Na ndo kinachokuliza,
wivu
Raymond: mama yote, wivu na wasiwasi anaweza kuwa
yupo kwa mwanaume, lakini pia anaweza kuwa yupo kwenye matatizo
(Baba Raymond anatokea ndani)
Mr. Bembele: kuna nini hapa?
Mrs.Bembele :( anamfuta
mwanae machozi)
Mr. Bembele: Analia nini huyo?
(Raymond na
mama yake wanakaa kimya)
Mr. Bembele: hamjibu sio? Labda hamjasikia
swali…Analia nini huyo? (Kwa Raymond)
Wewe Raymond unalia nini?
Raymond :(
anakaa kimya)
Mr. Bembele: nauliza tena
Mrs.Bembele: msichana wake amepotea
Mr. Bembele: kwahiyo Kama amepotea yeye Analia
kwanini…ni ndugu yako?
Raymond :( kimya)
Mr. Bembele: au mna ajenda gani au hawara yako?
Maana Christina ameniambia umeachana nae sasa isije ikawa umemuacha Christina
kuambatana na huyo maskini Raymond sitakuelewa
Raymond: ndio ni mpenzi wangu…nampenda sana na ndio
nina huzuni hapatikani na wala sijui alipo
Mrs.Bembele: Raymond!!!
Mr. Bembele: Unasemaje???? Nahisi sijasikia vizuri
embu ongea tena…umesemaje?
Mrs.Bembele: jamani acheni kugombana yaani kila
mkionana mnagombana tu
Mr. Bembele: sikukusomesha uje utembee na takataka
kama huyo housegirl wako, na wala sikukupa kazi na kukujengea nyumba ya
kifahari uje utembee na takataka
Mrs.Bembele: baba Ray
Raymond: una bahati wewe ni baba yangu
Mr. Bembele: ungenifanyaje...Yaani huna adabu wewe
ni wa kuniambia hivyo eti ndio ni mpenzi wangu, una mchumba Raymond na tayari
nimeshatoa mahari sitatoa mahari kwa takataka nyingine
Raymond :(
anaondoka zake huku Analia Sana)
Mrs.Bembele: mwanangu
Mr. Bembele: muache aende…halafu wewe ingia ndani
haraka
Mrs.Bembele :( anaingia
huku anaonekana ana huzuni Sana)
Mr. Bembele :(
anamfuata kwa nyuma)
(Raymond anapanda gari lake na kuliondoa kwa kasi sana, anaonekana kuwa
ana hasira sana, analiendesha gari mpaka nyumbani kwa kina Christina.anapofika
anakaribishwa vizuri sana na mama pamoja na shangazi yake Christina)
Mama: karibu baba…
Raymond: Asante…shikamoo mama
Mama: marahaba baba…tupo
Raymond :(
Kwa shangazi) shikamoo
Shangazi: marahaba baba karibu
Raymond: Asante…namuulizia Christina
Mama: yupo chumbani kwake…
Raymond: naomba uniitie
Shangazi: pita tu mbona ulikuwa unaingia tu
Raymond :( anaona
asibishane na mtu anaelekea chumbani kwa Christina, baada ya hatua mbili tatu
anafika mlango wa chumba cha Christina) hodiiii
Christina: karibu (ananyanyuka kivivu anaenda kufungua mlango) karibu (anashangaa kumuona Raymond)
Raymond: habari yako
Christina: marahaba…
Raymond: nimekuambia habari yako
Christina: ah salama jamani karibu
Raymond :( anamuangalia
kwa umakini) mbona kama umeogopa na kupagawa kuniona
Christina: wasiwasi wako tu wala sina wasiwasi sema
tu sikutegemea kukuona
Raymond: isiwe kesi (anasimama kimya kwa muda)
Christina: karibu (anamruhusu kuingia)
Raymond: Christina
Christina: abee...
Raymond: Angel yuko wapi?
Christina :( anacheka
kidogo) wewe Raymond Mimi nitajuaje mitoko yake? Siishi nae mimi kwahiyo
nitajuaje …sijui alipo
Raymond: are you sure?
Christina: iam sure Raymond I mean nitajuaje mpenzi
wako ana madanga gani…Kama haonekani labda kaenda kwa madanga
Raymond :(
anamuangalia Sana)
Christina: ndo hivyo Kama haonekani basi kaenda kwa
wanaume zake
Raymond: mbona unaongea Kwa uhakika Zaidi utakuwa
umempeleka nini? Au unajua alipo
Christina: eeh…eeh...Samahani kaka tena wewe na
huyo mwanamke wako mnikome, eti chochote kibaya kikimtokea mimi…yeye ni mtu
mzima anapoteaje kwa mfano, si atakuwa ameamua kutoweka…mimi usiniulize maswali
ya kijinga
Raymond: poa Asante kwa muda na ushirikiano wako
Christina :( huku
anaangalia pembeni) karibu
Raymond :(
anaondoka)
Christina :( anabaki
anafyonza)
Raymond :( anafika
nje walipo mama na shangazi yake Christina)
Mama: vipi baba
Raymond: asanteni…Mimi naondoka
Shangazi: haya karibu
Raymond :( anaondoka)
Mama: macho yamemvimba au namuona vibaya…yaani
anaonekana amelia Sana
Shangazi: atajijua
Mama: sijui ana shida gani
Shangazi: wewe anakuhusu nini? Kwani ndugu yako?
Mama:
kwakweli hayanihusu…ngoja nikae kimya mie (anakaa
kimya)
Shangazi
:( anabaki kimya pia)
0 Comments