SCENE 33: -
(Asubuhi ya
siku ya pili yake, kuna ubaridi ulioambatana na umande, Christina anafika
katika jumba alimomuachana Angelina)
Christina :( anamuamsha
kwa kumpiga teke) oya unalala lala nini hapa?
Angelina :( anaonekana
ni dhaifu sana) nina njaa…tangu nimekuja sijala, nisamehe nimekosa
Christina :( anacheka
Kwa dharau) pole kwa kuumwa njaa Angelina
(Kuna mtu anaingia)
Christina: baby…karibu nilijua huji Leo
Mtu :( Ni
baba mzazi wa Raymond)
Angelina :( anashangaa
Sana maana tangu ametekwa hakuwahi kumuona mtu wa pili, anashangaa kumuona baba
mzazi wa Raymond) baba Raymond???!!!
Christina :(
anambusu mdomoni)
Mr. Bembele: hajafa tu huyu takataka
Christina: nilitaka uje tumuue Kwa pamoja (anaacheka Kwa kejeli)
Mr. Bembele :( anamuangalia
Christina kisha anambusu) Ni lazima afe maana ameshajua siri yetu ya muda Mrefu
Sana lakini pili sitaki mwanangu aoe takataka…nataka akuoe wewe baby ili
niendelee kukuona sio mbaya tukila baba na mtoto (anacheka sana) asante mpenzi wangu kwa kuniambia kuhusu Raymond na
huyu kinyago nataka nimuue kabla Raymond hajaamua maamuzi ya kijinga
Christina :( anacheka
Sana) oh baby jamani (anamuangalia Angelina)
sijui Raymond ameona nini kwa huyu takataka
Angelina :( anasikitika
Sana) mnachofanya sio sahihi nyinyi ni wakwe (anasikitika sana)
Christina: unasikitika nini?
Mr. Bembele: anasikitika kuwa anaenda kufa muda si Mrefu
(anatoa bastola na kutaka kumpiga)
(Kuna mtu anakuja Kwa nyuma na kumuamuru aache kufanya anachotaka
kufanya)
Mtu: embu subiri
(Christina na
Mr. Bembele wanageuka na kuangalia ni nani wanakuta ni Raymond)
Christina :( Kwa
mshangao) Raymond
Raymond: hujakosea…ni mimi
Christina: what are you doing here?
Raymond :(
anacheka kidogo) kumbe ndo mchezo wenu…
Christina :( anashangaa
Sana) what are you doing here? Umejuaje nipo huku?
Raymond :(
anamuwahi Angelina) my queen
Angelina :( anaonekana
ni dhaifu sana na mwili wake una vidonda vingi sana)
Raymond: nyinyi wawili…ni watu wa ajabu sana...Nimekuja
muda Mrefu ilibidi nisimame niangalie vitendo vyenu vya aibu…sikutegemea kama
Christina ungefika muda ukatembea mpaka na baba yangu mzazi? ili iweje…kwahiyo
kumbe ulipokuwa unaniambia kuwa unanipenda kumbe bado ulikuwa unanidanganya? (anasikitika sana)
Christina :( amepigwa
butwaa na haamini anachokiona)
Raymond: Na wewe baba…kumbe ndo maana unataka
nimuoe Christina ili uendelee kumuona
Mr. Bembele :( hana
cha kusema amebaki kimya Kama kuku aliyemwagiwa maji)
Raymond: mnataka kumuua mwanamke pekee anayenipenda
Kwa dhati
Christina :( anajikuta
anaona aibu)
Raymond: by the way naomba nikujibu swali lako wewe
Christina…umeniuliza nimejuaje kuwa uko hapa…Jana baada ya kuongea na wewe
sikuondoka nikabaki palepale kwenu, nilijificha tu…nikalala ndani ya gari langu,
alfajiri ilipofika nilishtuliwa na mlio wa gari lako nikaamka na kukufuata
hapa…
Christina :( anabaki
anashangaa)
Raymond: nampenda Sana Angelina na ukweli
utakaobaki kuwa hivyo…she is my queen na jinsi nilivyoona leo sidhani kama
nitawahi kukurudia hata kwa dawa…nakuchukia sana Christina…nakuchukia sana Mr.
Bembele
(Mr. Bembele na Christina wanabaki wamepigwa butwaa)
Raymond: now if you excuse me…I need to take my
queen to the hospital… (Anambeba Angelina)
Angelina :( Kwa
sauti ya chini) nasikia njaa…
Raymond: nitakupa chakula malkia wangu (anatoka nje na kuelekea kwenye gari lake,
anamuweka vizuri kisha anapanda na yeye na kuliondoa gari kwa kasi sana)
(Huku ndani Kwa Christina na Mr. Bembele)
Mr. Bembele: Loh!!!Aibu gani hii mwenzenu
Christina: baby…don’t worry sio kwamba eti
anakuchukia kweli ni hasira
Mr. Bembele: usiniite baby wako maana Mimi sio baby
wako Christina, sijui imekuwaje mpaka nikaingia kuzini na wewe
Christina :( anamshangaa)
nini kimekupata baby mbona sikuelewi?
Mr. Bembele: mwanangu amenitamkia kuwa hanipendi na
yote sababu yako Christina
Christina: sasa Mimi nimefanyaje wewe baba...Kwani Mimi
ndo nilikutongoza? Si wewe na tamaa zako ndo zilikufanya ukanifata
Mr. Bembele: Kwa aibu hii ya Leo sidhani Kama
nitaendelea na wewe Christina
Christina: unaniachaje na mimi nina mimba yako?
Mr. Bembele: itoe sipo tayari kuipoteza familia
yangu niliyoijenga kwa Zaidi ya miaka 30 kwa ajili ya uhusiano wa miaka
miwili…sipo tayari naenda hospitali sijui ni hospitali ipi ila nataka kuongea
na mwanangu najua nimemuumiza sana baba yangu…na ninajua anaweza kumwambia mama
yake sitaki kuwapoteza mke na mwanangu kwa ajili yako Christina
Christina: umenipotezea muda Sana
Mr. Bembele: umejipotezea muda mwenyewe yaani wewe
kwa akili zako ulihisi nitakuoa au nitamuacha mke wangu na kuja kwako? ulidhani
nitamuacha Raymond wangu na kuja kwako…nimefanya kosa kuchangia mwanamke na
mwanangu na kwa hilo ni lazima nimuombe msamaha mwanangu na kumuomba asimwambie
mama yake
Christina: miaka miwili Bembele…
Mr. Bembele: hata Kama ingekuwa kumi…sipo tayari
kumuacha Glory wangu na kuja kwako wewe Christina najua Gloria wangu ni mzee
nampenda hivyo hivyo kuanzia leo sitaki tena mahusiano na wewe kwa muda wote
huo ambao tumekuwa tukiwadanganya watu naomba uishie hapa sitaki tena
Christina :(
anaongea Kwa jazba Sana) Nina mimba yako
Mr. Bembele: itoe I do not care
Christina: you bastard!!!Umenichezea Kwa miaka
miwili Leo hii unaniacha kirahisi hivi?
Mr. Bembele: wewe ulidhanije? kwamba naweza
kumuacha wife kizembe na kuja kwako? naipenda familia yangu na hakuna hata kitu
kimoja ambacho kinaweza kututenganisha, sasa endelea na maisha yako…hata hivyo
nimekulipa sana…nimekununulia magari ulikuwa unnaenda kutalii bure sehemu
yoyote uliyopenda sasa unadhani sijakulipa kwa huduma ulizokuwa unanipa?
Christina :( anasikitika)
wanaume
Mr. Bembele: ndo hivyo sasa…naomba niondoke Na
usinitafute tena nitakuwa busy na familia yangu
Christina :( machozi
yanamlenga)
Mr. Bembele :(
anaondoka zake)
Christina:(anabaki Analia)nimekosa pote…sio kwa
mwana na sio kwa baba…nimefanya nini?tamaa ningejua ningekaa na Raymond…kwa
tukio hili hata nifanyaje Raymond hatanirudia…loh,nimekwisha mimi jamani zile
raha zote zimeisha na nimebaki na Peter wangu asiyekuwa na pesa wale wenye pesa
hawatanitaka tena,nimekosea mimi jamani(anajiinamia)dah..tamaa
hizi jamani loh,Christina umeaibika wewe,umalaya umekuponza loh(anafuta machozi ghafla)No…hujashindwa
Christina…hakuna mtu anayekuacha mpaka wewe mwenyewe upende kumuacha,pambana
mtoto na baba wote ni wako na hakuna atakayekupokonya HAYUPO!!!!sio huyo Angelina
wala sio huyo bibi kizee sijui Glory wewe ndo utaamua utataka kumuacha nani na
lini na sio wao waamue…sasa wewe babu kizee na wewe Raymond msidhani mniweza
mimi Christina(anaamka na kuanza
kutembeatembea na kujigamba)siachwi naacha,na kwa nyinyi wawili nitaamua
nitamuacha nani na nitabaki na nani na sio nyie kunipangia eti mnaniacha
mnaongelea familia wakati mnanitongoza
hamkuwa na hizo familia?jibu ni kwamba mlikuwa nazo ila bado mkanifuata
na kunipa ahadi kemkem kuwa mtanitunza leo limevumbuka hili mnajiweka
pembeni,NO,NO siachwi kizembe mimi nitapambana mpaka kieleweke..(Anabeba mkoba wake kisha anatoka nje,
anapiga hatua chache kisha analiangalia lile jumba kwa nje)Bembele
aliniahidi kuninunulia hili jengo halafu leo ananikataa..Nitahakikisha
ananinunulia (anaondoka zake)
0 Comments