SCENE 34: -
(Majira ya
saa sita mchana, Raymond, Edmond na Catherine wapo hospitali wakisubiri kusikia
hali ya Angelina inavyoendelea, wamekaa huku kila mmoja wao anaonekana ana
mawazo sana ila zaidi Raymond)
Edmond:(anamshika
bega) tulia Mond, atakuwa sawa
Raymond: wewe unasema tu maana kwanza umemkuta ana
afadhali kidogo…hajala siku karibia tatu hali yake sio nzuri…ana vidonda mwili
mzima na sijui kama umeviona hivyo, walikuwa wanampiga usiku na mchana, kama
dozi
(Mr. Bembele anawasili mahala hapo)
Raymond:(anakunja
uso ghafla na kuangalia pembeni)
Edmond: vipi? mbona umegeuka ghafla (anaangalia mlangoni anamuona Mr. Bembele)
oh baba...shikamoo
Mr. Bembele:(kwa
upole) marahaba baba…
Edmond:(anashangaa
sana)
Raymond: unafanya nini hapa Mr. Bembele?
Catherine:(kwa
Mr. Bembele) shikamoo baba
Mr. Bembele: (kwa
Catherine) marahaba mama hujambo?
(Edmond na Catherine
wanaangaliana)
Mr. Bembele:(kwa
Raymond) naomba tuzungumze mwanangu
Raymond: mimi sio mwanao…sio mwanao kabisa Mr.
Bembele maana kama ningekuwa mwanao sidhani kama ungenifanyia yale uliyoyafanya
Mr. Bembele: nisamehe mwanangu jamani nimekosa
sitarudia tena
Raymond: maji yakishamwagika hayazoleki
Edmond: Mond?
Raymond: wewe niache tu Mond…huyu mzee
alichonifanyia ni Mungu mwenyewe anajua kwanini alifanya hivyo
Edmond: amefanyaje?
Raymond:(kimya
kidogo) acha tu… (anaenda kusimama
mbali kidogo na wote)
Mr. Bembele:(anamfuata)
mwanangu…baba yangu (anamshika bega)
Raymond: Don’t touch me please!!!by the way Go to
your lover
Mr. Bembele: mwanangu…ningetaka kubaki huko
ungeniona huku? nimekutafuta mpaka nimekupata
Raymond: najua kuna vitu unanidai (kwa hasira) haki ya Mungu ningekuwa na
uwezo ningevirudisha vyote ubaya ni kwamba siwezi sasa naomba uniache nisije
nikaongea maneno mabaya ukanipa laana wewe baba wewe…katika hali ya kawaida
kweli baba unatembea na mwanamke niliyetembea nae…yaani tunachangia baba…baba,
Ee Mungu dunia inaenda wapi hii? baba na mwana tunaingiliana?
Mr. Bembele: nisamehe sana baba yangu nisamehe
mwanangu nakuomba baba yangu
Raymond: hapana…hapana…wewe nenda tu na sitaki kukuona
tena
Mr. Bembele: usimwambie mama yako nampenda mke
wangu
Raymond: siwezi kumwambia mama yangu upuuzi huo
ataumia sana…
Mr. Bembele:(anashusha
pumzi) asante mwanangu…mpenzi wako anaendeleaje?
Raymond:(anashangaa) mpenzi wangu gani?
Mr. Bembele: Angelina
Raymond:(anashangaa
kisha anacheka kidogo) umeanza lini kumpenda Angelina wewe si ulikuwa
unamwita takataka?
Mr. Bembele: sitamuita tena
Raymond:(anaguna
kidogo) okay bado sijajua maendeleo yake dokta katuambia tukae hapa nje
atatuambia
Mr. Bembele: najua mimi ndo chanzo cha matatizo
yake
Raymond:(anakaa
kimya)
Mr. Bembele: nitalipa bili yote
Raymond: usijisumbue…nitalipa, Mimi ndo nimemleta
hapa kwahiyo nitalipa mimi
Mr. Bembele:na mimi ndo nimesababisha yote haya
Raymond:no need…halafu Zaidi usijifanyishe kuwa una
mapenzi na malkia wangu ili nisiseme chochote kwa mama, usijali ndugu yangu
sitamwambia mama wala hakuna atakayejua kuwa wewe na Christina mna mahusiano
Mr. Bembele: tulikuwa na mahusiano ila kwa sasa
nimeyavunja nawapenda sana wewe na mama yako
Raymond: kwahiyo unataka nikupigie makofi kuwa
hongera umefanya vyema baba
Mr. Bembele: Raymond nitafanya kila kitu ili
mwanangu unisamehe nitatoa mahari kwa kina Angelina mwanangu utamuoa Angelina
mwanangu nisamehe baba
Raymond: stop (anaangalia
mlangoni) mama anakuja…na sijui utamjibu nini akikukuta hapa
Mr. Bembele:(anakaa
kimya)
(Mrs.Bembele
anawafikia)
Mrs.Bembele: vipi?
Mr. Bembele: poa…za huko?
Raymond: shikamoo mama
Mrs.Bembele: marahaba mwanangu mzuri (kwa Mr. Bembele) za huko nzuri, Raymond
amenipigia simu ameniambia Angelina amepatikana lakini hali yake ni mbaya sana,
kwahiyo nikaamua kuja hapa kumuona
Raymond:(anamuangalia
baba yake)
Mr. Bembele:(anajitahidi
kuwa wa kawaida) okay haina shida
Mrs.Bembele: pamoja na hayo yote sikutegemea
kukukuta huku
Mr. Bembele:(anashikwa
na kigugumizi)
Mrs.Bembele: sitaki kujua sana maana nyinyi ni damu
moja labda mmeoneana huruma mkaamua kuja kupeana ushirikiano… (anacheka kidogo) kwahiyo Angelina yuko
wapi?
Raymond: bado hajatoka chumba cha matibabu...
Mrs.Bembele: sawa…Mungu amsaidie atoke salama
Mr. Bembele: Glory, nakupenda sana mke wangu
Mrs.Bembele:(anashangaa
kidogo) umekuwaje? kwani huu ni muda wa kuambiana nakupenda jamani…anyway (anacheka huku anamuangalia Raymond)
nakupenda pia mume wangu
Raymond:(anacheka
kidogo)
Mrs.Bembele: (kwa
Raymond) bora baba umecheka maana ulivyokuwa umenuna(anaguna)
(Daktari
anatoka)
Daktari: hali ya mgonjwa imeimarika kidogo
(watu wote waliopo hapo wanashusha pumzi)
Raymond: tunaweza kumuona?
Daktari: karibuni (anawaruhusu kisha anaondoka)
(wanaingia
chumba alicholazwa Angelina)
Raymond:(anambusu
shavuni) pole my queen
Mrs.Bembele: pole mama
Catherine na Edmond: pole Angelina
Mr. Bembele: pole Angelina
(wanashangaa)
Angelina:(kwa shida) asanteni
Raymond: utapona…
Angelina:(kwa
sauti ya chini sana) asante
(wanaendelea kumfariji huku kila mmoja wao akionyesha
huruma kwa majeruhi huyo)
0 Comments