SCENE 35: -
(Majira ya saa tatu na nusu usiku, Raymond na Angelina wapo nyumbani
wanaonekana wametulia na wana Amani, wanaangalia runinga huku wameegemeana kwa
mapenzi makubwa)
Raymond:(anamvuta
Angelina na kumlaza kifuani kwake)
Angelina:(bila
kubisha anamlalia)
Raymond: pole kwa mateso uliyoyapata hizi siku
mbili tatu
Angelina: asante nimeshapoa
Raymond: niliogopa sana nikawa najiuliza sijui
nitawahi kukuona tena malkia wangu
Angelina:(anacheka
kidogo) Mungu ni mwema nimerudi na nipo nawe
Raymond: kweli Mungu ni mwema…na fadhili zake ni za
milele
Angelina: hakika
Raymond:(anakaa
kimya huku anamuangalia sana) uliishije huko?
Angelina:(anaguna
kidogo) acha tu ndugu yangu yaani niliishi kwa shida kweli yaani hawakunipa
chakula wala maji, kila wakija walikuwa wananipiga sana
Raymond:(anasikitika sana) aisee walikutesa…roho
zao ni mbaya sana
Angelina: niliona ni muujiza siku ulipokuja
Raymond: nilikaa nje ya nyumba ya kina Christina
usiku mzima
Angelina: kweli unanipenda
Raymond: (anamuangalia
sana) inamaana huamini mpaka leo kuwa nakupenda mpenzi wangu?
Angelina: nami nakupenda sana
Raymond: asante…nataka nikuoe...hii staili ya
kulala kila mtu chumba chake nimeichoka nataka tuwe tunalala wote
Angelina: tutalala wote tukioana
Raymond; nataka nikuoe mapema iwezekanavyo
Angelina: sawa Raymond mimi nipo tayari kuoana na wewe
Raymond: hata mimi…nakupenda Angelina sijui umenipa
nini sijawahi kumpenda mwanamke hivi tangu nimeyajua mapenzi
Angelina:(anacheka)
huwa inatokea...hata mimi nakupenda sana Raymond yaani siwezi kuishi bila wewe
naomba usije ukaniacha kamwe katika maisha yako
Raymond: sitathubutu…. umeniweza baby…yaani
umeniweza mpaka ukaniweza tena baby
Angelina:(anacheka)
Raymond:(anashindwa
kujizuia, anambusu mdomoni)
Angelina:(anasogea pembeni) hapana Raymond wakati
bado
Raymond: nakubusu tu wala sina nia nyingine
Angelina: sisi sote ni watu wazima na tuna hisia
tunaweza kupitiwa
Raymond: exactly baby sisi sote ni watu wazima
unachoogopa ni nini?
Angelina: mama yangu ananitegemea sana siruhusiwi
kujisahau
Raymond: wewe…sio kujisahau bwana…ni mapenzi
tu…nakuahidi hakuna kitakachoharibika…hata ukibeba mimba nimeshakuahidi kuwa
nitakuoa
Angelina: hapana Raymond…
Raymond: tafadhali...mahusiano yetu ni ya muda sasa
kwanini hutaki?
Angelina: tangu mwanzo tulikubaliana kuwa utasubiri
mpaka tutakapofunga ndoa
Raymond: ndoa ipo jikoni Angelina naapa
sitakufanyia ukatili kwa kukataa mimba au chochote kile
Angelina: hapana Raymond mi naenda kulala tutaongea
kesho
Raymond: okay usiku mwema
Angelina:(anaingia
chumbani kwake anajifunika shuka mpaka juu kisha anazima taa)
Raymond: Angelina hataki kabisa kuniamini na Zaidi
sijui anaogopa nini penzi letu limeshakuwa na linastawi vizuri anachoogopa ni
nini?
Angelina:(anatoka chumbani kuelekea jikoni)
Raymond:(anamfuata) Angelina
Angelina:(anajikuta anamkumbatia ghafla)
Raymond:(anamkumbatia
pia) sisi ni wapenzi, wenye malengo sio vibaya kufanya mapenzi
Angelina: lakini ni dhambi
Raymond:(ananyamazisha
kwa kuweka mdomo wake kwenye midomo ya Angelina)
(wanapitiwa na hisia za miili yao na wanajikuta wanaruhusu hisia zao
ziwatawale)
Raymond:(anambeba
Angelina na kumpeleka chumbani kwake)
Angelina:(haonyeshi
ubishi)
Raymond:(anamlaza kitandani na anarudi anafunga
mlango)
0 Comments