SCENE 36: -
KESHO YAKE ASUBUHI
(Raymond ameamka ila hafanyi chochote Zaidi ya kumuangalia Angelina,
baada ya kujigeuzageuza hatimaye Angelina nae anaamka)
Raymond:za asubuhi?
Angelina:(anajinyoosha)
Mungu wangu nililala chumbani kwako?
Raymond:(anatabasamu)
kwani vibaya?
Angelina: vibaya ndio...Mungu wangu…jana tuliruhusu
hisia zetu zitutawale
Raymond: sio dhambi…na wala sio vibaya
Angelina: Mungu wangu…halafu umechelewa sana kazini
Raymond: sitaenda kazini…nitawaambia kuwa naumwa
Angelina: kwanini?
Raymond: nataka kukaa na wewe
Angelina:(anacheka)
jamani
Raymond: asante Angelina
Angelina: asante ya nini?
Raymond: kwa kila kitu kuja katika maisha
yangu…sasa naona nuru nilikuwa naona giza sasa naona mwanga wa kutosha...asante
pia hata kwa kunipa nafasi ya kuwa mwanaume wa kwanza kwako
Angelina:(anatabasamu
kidogo)
Raymond: asante pia kwa Imani yako nakuthamini sana
Angelina
Angelina:(anaona
aibu)
Raymond: usione aibu bwana
AAngelina:(anachukua nguo zake kisha anashuka
kitandani)
Raymond: unaenda wapi?
Angelina: naenda kuandaa chai
Raymond: I love you…nakupenda Angelina
Angelina:(anaona
aibu anaondoka zake anaingia chumbani kwake)
Raymond:(anabaki
anatabasamu)
Angelina :(yupo
chumbani kwake) hapana Angelina ulichofanya sio kizuri yaani umekubali
kufanya tendo linalofanywa na wanandoa kabla ya ndoa? inamaana umekuwa mjinga
namna hiyo?
Raymond :(bado
amekaa chumbani kwake) najua hukutaka ila jana hisia zilikuzidi nguvu mke
wangu
Angelina :( akiwa
jikoni) Mungu wangu nimekosea Sana…nikibeba mimba je? Nitamwambia nini mama
jamani?
Raymond :( yupo
chumbani) ngoja nikamuone anafanya nini? (anashuka kitandani na kwenda jikoni)
Angelina: Mungu wangu…kwanini nilijisahau?
Raymond:(anafika)
ulijisahau nini mama?
Angelina: Raymond tumekosea sana nisingejisahau
Raymond:(anatabasamu)
hapana wala sio mbaya baby
Angelina: hapana Raymond hatukutumia hata kinga
Raymond:(anacheka) He!!!wewe kwahiyo unadhani nina
UKIMWI?
Angelina: hapana jamani mi naogopa mimba…wadogo
zangu wananitegemea sana
Raymond: tulia…huna UKIMWI labda mimba (anajificha uso)
Angelina: hapana kwakweli sitaki mimba
Raymond:ni mambo ya kawaida hayo kwa watu
wanaopendana ni lazima mambo hayo yatokee
Angelina: nilikuambia tusubiri mpaka tutakapokuwa
tayari yaani baada ya ndoa
Raymond: nitakuoa
Angelina: unasema tu kunitia moyo
Raymond: hapana sisemi kukupa moyo ninasema kwakuwa
nina uhakika
Angelina: ulimvalisha pete Christina ukamuacha
sembuse mimi
Raymond: usijilinganishe na Christina hamuwezi
kufanana
Angelina: kivipi?
Raymond: wewe ni bora sana na wewe ni mzuri sana
kuliko Christina
Angelina sawa haina shida kwahiyo unaniambiaje?
Raymond: tulia mpenzi usiogope …tupo pamoja
Angelina:(anatulia) haya bwana ila kama
unanidanganya Raymondo anajua
Raymond: usijali mpenzi
(Wanakumbatiana)
Raymond:
nakupenda mpaka nakupenda tena… (anatabasamu)
0 Comments