SCENE 37: -
(Asubuhi ya siku nyingine tena Raymond yupo ofisini
kwake, amekaa anawaza kitu Fulani lakini ghafla anajisikia vibaya na kuanza
kulia kama kuugulia)
Raymond
:( anaugulia) Ahhh….
Glory
:(anakuja anakimbia) boss…
Raymond:
mama (anashika tumbo)
Glory:
unaumwa wapi?
Raymond:
tumbo linauma sana…ah(anainama)
Glory:
twende ukalale huku tukuhudumie
Raymond
:(kwa sauti ya chini kabisa) muite Angelina
Glory:
sina namba yake boss
Raymond:(anampa simu yake) itafute humu
Glory
:( anaichukua harakaharaka na kutafuta
namba ya Angelina anapiga anapoona anapiga)
(Simu inaita)
Angelina
:(anapokea) my dear
Glory:
hello Angelina
Angelina:
wewe nani jamani? mbona unaongelea kwenye simu ya Raymond?
Glory:
mimi ni secretary wa Raymond njoo huku ofisini kwetu Raymond anaumwa sana
Angelina
:(anashtuka) Mungu wangu jamani nini
tena?
Glory:
tumbo na linamuuma sana...yaani linaonekana linamuuma sana jamani…fanya haraka
sana
Angelina:(anakata simu na kukimbilia nje anatafuta bodaboda)
Mungu wangu jamani mbona hata bodaboda hazipiti
(bodaboda inapita)
Angelina:(anaita) kaka…nipeleke
Dereva:
wapi…
Angelina:
twende tu…nitakuambia huko mbeleni
Dereva:(anaanza kuendesha na kuiondoa mara moja)
(Upande wa kina Raymond)
Raymond
:( anatoka ofisini kwake)
Glory:
boss ungekaa kutulia hapahapa
Raymond:
niache tu huku sio kuumwa jamani acha watu wanione jamani nisije nikafia ndani
humu
Glory:
haya ngoja nikusaidia
(Wanatoka)
Raymand
:(anashika tumbo) mama…(anaugulia)
Pendo:(anamuona) boss…(anakuja)boss nini?
Rachel
:(anakuja pia)
Raymond:
aah tumbo…
Pendo:
ngoja nimuite Edmond
Raymond:
nimeshampigia
(Edmond anafika akiwa na Catherine)
Edmond:
nini tena Mond…
Raymond:
naumwa tumbo vibaya…nahisi nakufa jamani nimeona niwaite wapendwa wangu wote…
Edmond:
sasa si msaidieni jamani yupo hospitali ila hakuna msaada wowote inakuwaje?
(Angelina anafika)
Angelina:
jamani…Raymond yupo wapi? (kwa pendo na Rachel) shikamooni
Pendo
na Rachel: marahaba
Angelina:(anamuona Raymond anamuendea) Raymond
nini tena?
Raymond
:(anainuka na kupiga goti moja)
Angelina
:(anashangaa) Raymond…
(Edmond na Catherine wanashangaa sana)
Raymond:
Angelina
Angelina
:(anaogopa sana) kuna nini?
Raymond:
nimejifanya naumwa ili uje ofisini…tulipanga mimi, secretary, pendo na Rachel
tulipanga tangu asubuhi…nimekuvuta huku ili nikuombe uwe mke wangu… (anatoa mkebe kutoka mfukoni mwake)
siumwi hata kidogo ni pozi tu tumetumia…kukuvuta…huku nimeona hapa ni sehemu
sahihi kufanya hili
Angelina
:( anatabasamu)
Edmond
:( anacheka) yaani wewe
Angelina:
jamani Raymond
Raymond
:( anaufungua mkebe) Angelina naomba
uwe mke wangu
Angelina:
sawa…nakubali
Raymond:(anamvalisha pete inayoonekana ni ya thamani
sana)
(watu wanashangilia sana)
Angelina:(anacheka huku anaiangalia pete ile)
Raymond:(anamkumbatia Angelina) nakupenda sana
mke wangu mtarajiwa
Catherine:(anafurahi sana)
(watu wanawapongeza sana)
Edmond:(anamuita Raymond pembeni) Mond…embu njoo
Raymond:(anamfuata) vipi are you not happy for me
Mond...?
Edmond:
iam very happy for you Mond ubaya ni kwamba unajichanganya?
Raymond:
kivipi?
Edmond:
wewe ni mchumba wa Christina au umesahau?
Raymond:
wewe ndo umesahau my friend…mimi na Christina tumeshaachana siku nyingi sana
Edmond:
amekubali
Raymond:
inabidi akubali hana ujanja hapo
Edmond:(kimya kidogo kama anawaza kitu) haya
lakini kama umeamua hivyo…by the way mnapendezeana sana
Raymond:
eti eeh(anacheka)asanteeeee
(wanarudi walipo wengine)
Pendo
na Rachel :(wanaishangaa sana pete ya Angelina)
Glory:
basi mtaishangaa…nimeichagua mimi hiyo
Pendo:
hujaulizwa mama
Catherine:(anacheka) jamani kama amefanya hivyo
asiseme?
Rachel
:( anacheka) anajishaua tu…ila boss
sasa hivi kajua kuchagua
Glory:
Sana
Edmond:(anawaangalia huku anatabasamu) hatimaye
mmefanikiwa na mipango yenu hongereni sana
(Watu wote waliopo pale wanaonekana ni wenye
furaha mara baada ya tukio fupi lililotokea)
Rachel:
harusi lini?
Raymond:
hivi karibuni
(watu waliopo hapo wanashangilia)
0 Comments