SCENE 38
(Raymond anafika nyumbani kwa
wazazi wake akiwa anaonekana ana furaha sana juu ya kitu Fulani)
Raymond:(anagonga
mlango) hodi…
Mrs.Bembele:(anakuja kufungua mlango) karibu
Raymond:(anamkumbatia
mama yake kwa furaha)
Mrs.Bembele: wewe nini? mbona sikuelewi?
Raymond: she said yes…
Mrs.Bembele: nani?
Raymond: Angelina mama…she is now my fiancée
Mrs.Bembele:(anamvutia
sebuleni) wewe ongea taratibu baba yako akisikia atatunyonga au umesahau
Raymond: ah mama(anatembeatembea)sijali yeye anawaza nini…nachojua ni kwamba
nimemvalisha pete ya uchumba mpenzi wangu na sasa ni mchumba wangu na
ninampenda sana
Mrs.Bembele: hongera mwanangu yaani unaonekana una
furaha wewe
Raymond: sana mama…yaani mpaka nahisi nataka kupaa
kwa furaha hii mama, iam so happy mama
(Mr. Bembele
anakuja)
Mrs.Bembele: baba yako huyo…
Mr. Bembele:(anamuangalia
Raymond kwa aibu kubwa sana)
Raymond:(anaona
amwambie hapohapo) nimemvalisha pete ya uchumba Angelina natarajia kumuoa
Mrs.Bembele:(anaziba
mdomo kwa mikono yake miwili) wewe Raymond…
Mr. Bembele: sawa haina shida
Mrs.Bembele:(anapigwa
butwaa) makubwa…leo imekuwaje baba Raymond umekubali
(Raymond na baba yake wanaangaliana chinichini)
Mrs.Bembele: yaani unajua sikuelewi kabisa
Raymond:(anamuangalia
baba yake kwa jicho la hasira sana)
Mrs.Bembele: eti umekubali Raymond amuoe msichana
wake wa kazi au mimi nimesikia vibaya
Mr. Bembele: sasa kama ameamua mimi ni nani kupinga
Mrs.Bembele: lakini si ulisema mwanao hatakiwi kuoa
takataka leo amekuja kukuambia kuwa amechumbia umemjibu haraka na bila kupinga
kuna nini hapo?
Mr. Bembele: kwani mke wangu wewe unataka kuwepo
nini hapo?
Mrs.Bembele: ndo uniambie wewe…kuna nini mbona hizi
siku mbili tatu sikuelewi umekuwa mpole unawahi kurudi nyumbani na zile simu
zako za mpaka saa sita usiku umeacha yaani umekuwa mume mwema kweli
Mr. Bembele: Nimeona tu nifanye hivyo kama ni vibaya
nitaacha na kuendelea jinsi nilivyokuwa nafanya
Mrs.Bembele: hapana sijamaanisha nataka uache mume
wangu ila nashangaa anyways… (anamuangalia
Raymond) hongera mwanangu kwa kuchumbia(anacheka)kwa
mara ya pili
Raymond: asante mama
Mrs.Bembele: nilijua tu utapigana mpaka umuoe huyu
mwanamke
Mr. Bembele: inamaana ulikuwa unajua kuwa Raymond
anatembea na msichana wake wa kazi?
Mrs.Bembele:(huku
anatabasamu) ndio aliniambia tangu hata bado hajamtamkia kuwa anamtaka
Mr. Bembele:(hatii
neno)
Mrs.Bembele: unajua mume wangu kwa mara ya kwanza
nilimuona mtoto wetu kuwa kweli amependa
Mr. Bembele: aisee…basi kakua
Raymond:(anatabasamu
kinafki mbele ya mama yake)
Mrs.Bembele:(anaguna) unajua mimi nafurahi nini?
leo hamjagombana
Mr. Bembele:(anatabasamu)
hautaona tunagombana tena…sasa hivi tutaelewana...nitamsaidia hata ile ndoto
yake ya kujenga nyumba kwa ajili ya watoto yatima…
Raymond:(anashangaa)
unasema kweli au unanitania?
Mr. Bembele: nasema kweli kabisa...na unaweza kuwa
na marafiki wowote unaowataka
Mrs.Bembele: maajabu haya leo mimi (anacheka huku anapiga makofi) eeh
jamani niacheni niende nikapike leo mume na mwanangu wamekuwa marafiki jamani (anaenda jikoni)
Raymond:(anajitupa
kwenye sofa kama mzigo)
Mr. Bembele: mwanangu naomba unisamehe kwa yote
niliyowahi kukufanyia…
Raymond: nitakusamehe yote ila sitakusamehe hilo la
kutembea na mwanamke aliyekuwa mchumba wangu
Mr. Bembele: ndo maana nakuomba msamaha
mwanangu…usimwambie mama yako…haki ya Mungu tena nimeachana na Christina yaani
siku hiyohiyo umetukuta mwanangu…nampenda sana mama yako mwanangu jamani
Raymond: uwe umeachana nae au hujaachana nae baba
hilo mimi sijui na wala sijali na unajua hivyo
Mr. Bembele: basi fanya kwa ajili ya familia yetu
mwanangu…tupo watatu tu…jamani tukiachana na kutengana unadhani itakuwaje?
Raymond:(anavuta
pumzi ndefu) kwahiyo unataka kuniambiaje baba?
Mr. Bembele: mimi ni baba yako lakini je umeshawahi
kuniona nakuomba msamaha kwa chochote?
Raymond: hapana
Mr. Bembele: sasa naomba uone kuwa ninajuta kosa
langu ni kweli baba na mtoto kuchangia mwanamke au mwanaume ni laana na ndo
maana nimetubu naomba unisamehe baba
Raymond:(anakaa
kimya huku anaonekana kuna kitu anatafakari)
Mr. Bembele: usimwambie mama yako unajua nampenda
mama yako sana na akija kujua kuwa nimewahi kuwa na Christina ataondoka na
kudai talaka hata mpaka mahakamani…nampenda sana mke wangu na ndo maana
nimeshaachana na Christina hata ukimuuliza leo hii atakuambia kuwa tuliachana
siku ile ile
Raymond: nikikuuliza dad…kwanini ulifanya vile na
unasema kuwa unatupenda sisi familia yako? je upendo ndo uko hivyo kusaliti
wapendwa wako?
Mr. Bembele: hapana mwanangu unajua ile ilikuwa tu
ni tamaa…kuna siku niligombana na mama yako sana tu nikaona kuondoa stress
nitafute mwanamke mwingine
Raymond: ukaona utembee na Christina mwanamke ambae
alikuwa analala na mimi
Mr. Bembele: baba ilikuwa tamaa tu mwanangu…kwa
wakati huo Christina ndo alikuwepo hapo…alikuwa kama amenitegea tu...
Raymond: naelewa kuwa ilikuwa ni tamaa kwa mara
moja kwanini uliendelea nae?
Mr. Bembele: ndo maana nakwambia ni ujinga wangu tu
wala sio kwamba mke wangu ana kasoro yoyote maskini…mke wangu mwenyewe
mzuri…yaani na hivi kazaa mara moja…Mrembo kweli mke wangu
Raymond:(anajikuta
anacheka) sawa…sitamwambia mama kitu chochote…iwe siri yetu
Mr. Bembele: sawa…asante… (kimya kidogo) enhe!!tunaenda kutoa mahari lini kwa kina Angelina?
Raymond:(anashangaa)
hivi ulikuwa upo serious uliposema kuwa ni sawa mimi kumuoa Angelina
Mr. Bembele: sikuwa nakudanganya mwanangu…nimechoka
kugombana na wewe huku ndo ulivyo…una rafiki unampenda kweli ni maskini, sasa
hivi umependa msichana wako wa kazi, wajukuu zangu watatoka kwa mama maskini (anacheka kidogo) sina ujanja
mwanangu…nimekubaliana na wewe…kesho njoo ofisini kwangu na yule rafiki yangu
nani vile Desmond?
Raymond: Edmond
Mr. Bembele: yes…njooni mnitembelee
Raymond: hadi raha…dad asante
Mr. Bembele: usijali mwanangu sitaki tugombane tena,
kwanza malkia wetu hapendi anaumia kweli si huwa unamuona ee
Raymond: kweli
Mr. Bembele: tusimuudhi tumpe amani jamani
Raymond: haswaaa
(Wanaendelea kuongea wakati Mrs.Bembele anaendelea
kuandaa chakula kwa ajili ya mwanae na mume wake)
0 Comments